Monday, March 12

Mazungumzo kati ya Serikali, Airtel yaanza

Dar es Salaam. Mazungumzo kati Serikali na kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza leo Machi 12, 2018.
Mazungumzo hayo yanalenga kutafuta suluhu ya mmiliki halali wa kampuni ya Airtel ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini.
Katika mazungumzo hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Serikali inawakilishwa na mwenyekiti wa kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
Upande wa Bharti Airtel unawakilishwa na mwanasheria mkuu wake, Mukesh Bhavnani.
Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu leo Machi 12, 2018 imesema mazungumzo hayo yana lengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili na kuimarisha sekta ya mawasiliano Tanzania. 
Desemba mwaka jana uliibuka utata kuhusu mmiliki halali wa Airtel, Serikali ikisema ndiyo mmiliki halali kwa sababu ubinafsishwaji wa kampuni hiyo haukufuata utaratibu madai ambayo yalikanushwa na Bharti Airtel.

TMA yatahadharisha mvua kubwa mikoa 11


Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa kuendelea katika maeneo ya mikoa 11 nchini.
TMA imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.
Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka hiyo inabainisha kuwa kuanzia leo Machi 12 hadi 13 ,2018 kunatarajiwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.
“Hali hii inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua, wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanatakiwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa, TMA inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejesho kila itakapobidi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Siri ya wanawake kufanikiwa katika viwanda Afrika: Wanawake watatu wasimulia

Wanawake watatu
Haki na usawa kwa ndio mambo makuu yanayoshinikizwa duniani wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake wiki hii.
Kwa kawaida siku hii huwa ni fursa ya kuchukua hatua, kufanya mabadiliko, kushinikiza, kuhimiza na kuwawezesha wanawake wa nyanja zote kujitambua uwezo wao.
Licha ya kwamba wanawake wanachangia ukuaji wa uchumi kote Afrika, ukandamizaji unatatiza nafasi wanazoweza kuwa nazo.
Kutokana na kuendelea kukithiri kwa umaskini, wanawake wengi wanajipata katika ajira zenye vipato vya chini na wanakuwa na nafasi finyu ya kujiendeleza.
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, ili kuyatimiza, malengo ya maendeleo endelevu kama sehemu ya ajenda ya mwaka 2030, kuna haja ya kulisaidia bara la Afrika katika kushinikiza ustawi endelevu wa kiviwanda na unaojumuisha kila mtu.
Na hiyo ni kumaanisha hakuna atakaye achwa nyuma, hususan wanawake.
Baadhi ya mataifa ya Afrika yanapania kuwa na nchi zilizoendelea kiviwanda, lakini kwa mara nyingi idadi kubwa ya wanawake wanaonekana kususia kujitosa katika sekta hiyo. Je ni kwanini?
Tumezungumza na wanawake watatu kutoka Afrika Mashariki ambao ni miongoni wanawake wengi waliolivuka daraja hili na kupata ufanisi. Siri yao ni gani?
Bertilda Niyibaho
Image captionBertilda Niyibaho, mmiliki wa kiwanda kinachozalisha unga unaotokana na uyoga

Bertilda Niyibaho - Mjasirimali nchini Rwanda:

Bi Niyibaho Bertilda ni mjasiriamali aliye na kiwanda kinachozalisha unga unaotokana na uyoga kufwatia mradi kabambe alioanzisha wa kuimarisha lishe bora miongoni mwa jamii.
Biashara yake imepanuka na kuvuka mipaka ya Rwanda.
Huku akionyesha kiwanda chake, ambayo sehemu kubwa ni maabara na sehemu nyingine inatumiwa katika kurutubisha zao la uyoga, anasema akianza alikuwa mkulima tu wa kawaida: "Nilianza shughuli zangu nikitengeneza pombe ya kienyeji itokanayo na ndizi, lakini nikaja kuona kwamba mabaki ya ndizi na mabaki ya mazao mengine yanatupwa tu kiholela ilhali yangeweza kuzalishwa mambo mengine yakawa na manufaa kwa jamii, basi nikajitosa katika kulima uyoga."
Sehemu ya kiwanda cha bi Niyibaho inatumiwa katika kurutubisha zao la uyoga
Image captionSehemu ya kiwanda cha bi Niyibaho inatumiwa katika kurutubisha zao la uyoga
Kiwanda chake kilikua na akaanza kutengeneza unga wa uyoga na mazao mengine. Biashara yake imekuwa kadri muda ulivyosogea na imepanuka na kuvuka mipaka.
Kwa sasa yeye husafirisha bidhaa zake hadi Tanzania, Kenya, Uganda na hata Burundi. Licha ya ufanisi huu anasema hakukosa changamoto:
"Shida niliyo nayo ni kwamba, bidhaa zangu zikifika huko mfano Uganda zinabandikwa leseni ya kwamba zilitengenezwa Uganda!
"Binafsi nilifuatilia nikatembelea wale wanaolangua bidhaa zangu nikashangaa nilipokuta kwamba wameandika eti 'Made in Uganda!'
Changamoto nyingine anasema ni kukosa uungwaji mkono wa serikali na kupata leseni ya ubora wa bidhaa kumwezesha kupenya katika masoko ya Ulaya na Marekani.
Jennifer Bash Tanzania
Mkurugenzi wa kampuni ya Alaska
JenniferHaki miliki ya pichaHISANI
Jennifer Bash ni mkurugenzi wa kampuni ya Alaska nchini Tanzania.
Kampuni yake imejikita katika kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo yanayo zalishwa na wakulima wa Tanzania, wengi wao wakiwa ni wanawake.
Kampuni hii pia inajishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za vyakula kama mayai, mchele, mafuta ya Alizeti, unga wa sembe na dona.
Je ni ipi siri ya ufanisi wake katika sekta ya viwanda? Jenifer anaamini kwamba mtaji sio kikwazo kwa kuwa wazo ndio mtaji.
'Mara nyingi watu wanakua na mawazo makubwa lakini washindwa kuyafanyia kazi wakidhani wanahitaji mtaji mkubwa kufanyia kazi wazo lao.

'Ubunifu ni muhimu'

Wakati kuwaza makubwa ni vyema, lakini tukubali kuanza na kidogo ili kufikia makubwa kulingana na mazingira yanayotuzunguka'.
Jennifer anasema ubunifu wa uendeshaji wa biashara ni jambo muhimu kwenye kufanikisha biashara yeyote ili kupata wateja.
Alaska Tanzania imebuni soko lake kwa kujikita kwenye programu iitwayo 'Mama Alaska" ambayo inamuwezesha mama ntilie (Mama Lishe) kupata bidhaa za Alaska kwa urahisi na bei nafuu.
Pia inawawezesha wakulima kupata elimu ya kukuza biashara yao na kuona thamani ya kile wanachokifanya kwa kuboresha huduma zao na kutengeneza mnyororo mpya wa thamani.

Lorna Rutto - Kenya

Mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa Ecopost

LornaHaki miliki ya pichaHISANI
Lorna Rutto ni mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa EcoPost, kampuni ambayo imekuwa ikitumia taka za plastiki kuunda bidhaa mbalimbali zikiwemo boriti za kutumiwa kwenye nyua na mabango.
Kampuni yake huunda pia bidhaa mbalimbali za kutumiwa katika ujenzi.
Lorna amepokea tuzo nyingi Kenya na kimataifa na alikuwa miongoni mwa wanawake vijana 20 wenye nguvu Afrika walioorodheshwa na jarida la Forbes.
Alipokuwa anaanzisha Ecopost, alikumbana na changamoto nyingi hasa katika kutafuta mtaji.
"Tulitazamwa kama biashara iliyo na hatari nyingi tukilinganishwa na biashara nyingine sokoni. Benki zilitaka taarifa za akaunti za benki kuthibitisha kwamba biashara yetu ilikuwa inafanya vyema ilhali tulikuwa tu ndio tunaanza," anasema.
"Tulitakiwa pia tunatakiwa kutoa dhamana ya mkopo lakini hatukuwa na chochote."
Waliwasilisha maombi katika mpango wa Enablis- uliofadhiliwa na Wakfu wa Safaricom na wakashinda na hapo wakafanikiwa kupata mtaji.
Kando na fedha, walikabiliwa pia na tatizo la mitambo ya kutumia ambayo walihitajika kuiagiza kutoka nje ya nchi, pamoja na wafanyakazi wenye ufundi uliohitajika kuendesha mitambo hiyo.
Gharama ya uzalishaji ilikuwa pia juu - gharama ya umeme, malighafi, kulipia leseni na kadhalika.
"Hatukupokea pia usaidizi kutoka kwa serikali na wanaounda sera. Wajasiriamali hasa walio katika sekta ya viwanda wanahitaji kichocheo na usaidizi pamoja na mazingira mahsusi ili kufanikiwa," anasema Bi Rutto.
Anasema amegundua kwamba "fursa zipo kila pahali".
"Niliigundua fursa yangu katika kutumia tena taka. Taka si taka hadi zitupwe. Kazi yote pia ni ya heshima. Nimejifunza pia kwamba ni muhimu kuwa mbunifu, kuvumbua na kuendelea kujiboresha kila wakati," anasema.
"Safari yangu haijakuwa rahisi lakini nimejifunza kutokata tamaa kamwe. Nimegundua pia kwamba kuomba usaidizi inapobidi ni muhimu," anasema Bi Rutto.

'Ni muhimu kuomba usaidizi'

"Wanawake wengi hufikiria kwamba kuomba usaidizi ni dalili ya udhaifu; ukweli ni kwamba ni ishara ya nguvu. Kupata washirika wafaao ni muhimu pia. Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, shirikiana na wengine."
Ushauri wake kwa wanawake ambao wangependa kufanikiwa katika viwanda ni kwamba lazima utafute soko la bidhaa zako kwanza.
"Ningewahimiza wanawake wawe wabunifu na kuvumbua mambo na pia kuingia katika sekta ambazo zimetawaliwa na wanaume kwa muda mrefu mfano viwanda wakiona kuna fursa.
"Usiige tu wengine au kuchagua biashara iliyo rahisi. Soko limejaa wahusika wengi na kuna changamoto katika kutafuta nafasi ya ukuaji."
Baadhi ya watu huogopa kutofanikiwa lakini Bi Rutto anasema ni muhimu kujiamini mwenyewe.
"Kuwa na ujasiri na anza bila kukawia. Usizuiwe na chochote, usizuiwe hata na mtaji. Ningewashauri wanawake kuacha na fedha walizo nazo na kuzitumia vyema."
Anasema katika kuanzisha biashara au kiwanda, ni vyema kufikiria mchango wa biashara hiyo kwa jamii.
"Moja ya yaliyosaidia ukuaji wa Ecopost ni nia yetu ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii, tukihifadhi mazingira pia."

Afrika wiki hii kwa picha: 2-8 Machi, 2018

Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii.
Skauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya AlhamisiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSkauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya Alhamisi
Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0
Huyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionHuyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.
Mechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).
Wacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.
Mwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua kwa huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.
Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMuigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.
Hali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini MoroccoHaki miliki ya pichaEPA
Image captionHali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini Morocco
Familia hii ni moja kati ya maelfu ya Watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea UgandaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionFamilia hii ni moja kati ya maelfu ya watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea Uganda
Siku ya Jumatatu, Wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra LeoneHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSiku ya Jumatatu, wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra Leone
Uchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)
Nchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.
Kikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionKikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.

Trump kushtakiwa na mcheza filamu za utupu kwa kukiuka makubaliano

Rais Donald Trump amekana shutuma kuwa alikuwa na uhusiano na Stormy DanielsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Donald Trump amekana shutuma kuwa alikuwa na uhusiano na Stormy Daniels
Mcheza filamu za utupu Stormy Daniels anamshtaki Rais Donald Trump kwa kile kinachoitwa ''hush agreement'' ambayo ni makubaliano ya kutozungumzia mahusiano yao.
Daniels anadai kuwa yeye na Bwana Trump walikuwa na mahusiano tangu mwaka 2006, lakini alikana shutuma hizo.

Kwa nini habari hii ni muhimu?

Stormy Daniels ni nani?
Stormy Daniels alizaliwa Stephanie Clifford, Louisiana mwaka 1979.
Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu.
Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, 'Storm' na jina la kinywaji aina ya Whisky , 'Jack Danniels'.
Unaweza kumtambua kwenye filamu ya 'The 40-Year-Old Virgin' na 'Knocked Up' na video ya muziki wa kundi la Maroon Five 'Wake up call' .
Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani.
Stormy Daniels jina halisi ni Stephanie Clifford, anadai alikutana na Donald Trump mwaka 2006Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionStormy Daniels jina halisi ni Stephanie Clifford, anadai alikutana na Donald Trump mwaka 2006

Anadai nini?

Mwezi Julai mwaka 2006, Bi Daniels anasema alikutana na Trump kwenye michuano ya hisani ya Golf huko Lake Tahoe, eneo la kujivinjari la kati ya California na Nevada.
Katika mahojiano yake na jarida la In Touch Weekly' mwaka 2011 na kuchapishwa mwezi Januari, alisema Trump alimualika chakula cha jioni na kuwa alikwenda kukutana naye kwenye chumba chake cha hoteli.
''Alikuwa amejibwaga kwenye kochi, akitazama televisheni'', alisema kwenye mahojiano hayo, ''alikuwa amevaa nguo za kulalia''.
Bi Daniels anasema walifanya mapenzi kwenye chumba cha hoteli (Mwanasheria wa Trump amesema Trump amekana shutuma hizo)
Kama madai ya mwanadada huyo ni ya kweli, haya yote yangekuwa yametokea miezi minne tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto wa Trump mdogo, Barron.
Donald Trump, Melania Trump na Barron Trump mwezi Januari mwaka 2007Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump, Melania Trump na Barron Trump mwezi Januari mwaka 2007
Bi Daniels alisema Trump alimwambia anaweza kumshirikisha kwenye kipindi chake cha Televisheni, The Apprentice.
Amedai kuwa aliangalia sinema ya maisha halisi ya Papa na rais huyo ajaye.
Michael Cohen anaripotiwa kumlipa Stormy Daniels dola 130,000 mwaka 2016Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMichael Cohen anaripotiwa kumlipa Stormy Daniels dola 130,000 mwaka 2016
Baada ya hapo anasema waliendelea kuwasiliana kwa miaka kadhaa, Bi Daniels anasema mara ya mwisho kuwasiliana ilikuwa mwaka 2010, wakati alipoahirisha kugombea useneta.
Hata hivyo tetesi kuhusu uhusiano wao zilianza kujionyesha mwezi Novemba 2016 wakati wa uchaguzi wa urais.
Jarida la Wall Street liliripoti siku kadhaa kabla ya kura kuwa bi.Daniels alikuwa kwenye mijadala kwenye kipindi cha asubuhi cha televisheni ya ABC ''Good Morning America'' kueleza yote kuhusu mahusiano yake, kabla ya kuyakata ghafla mazungumzo.

Kwa nini hii ni habari kwa sasa?

Mwezi Januari, Jarida la Wall Street lilichapa makala iliyodai kuwa Wakili wa Trump, Michael Cohen, alimlipa dola za Marekani 130,000 mwanadada huyo mwezi Oktoba mwaka 2016, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi.
Jarida linasema pesa hizo zilikuwa ni sehemu ya makubaliano ambayo hayakufahamika,ambayo alisema hakuweza kujadili masuala yake mbele ya Umma.
Ripoti nyingi zilitolewa kuhusu hayo lakini shutuma zilikanushwa vikali wakati wakielekea kwenye uchaguzi, maafisa wa Ikulu wameeleza.
Rais Trump alighadhabishwa na namna ambavyo Sarah Sanders alikuwa akijibu maswali kuhusu Bi.DanielsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Trump alighadhabishwa na namna ambavyo Sarah Sanders alikuwa akijibu maswali kuhusu Bi.Daniels
Bwana Cohen alikana madai ya kumlipa pesa mwanadada huyo, katika taarifa yake kwenye jarida na kuita shutuma hizo kuwa hazina maana.Na wamekua wakipinga hilo kwa miaka kadhaa.
Lakini mwezi Februari alitangaza kuwa alimlipa Bi.Daniels pesa.
Katika taarifa aliyoitoa kwa New York Times, Bwana Cohen alisema si kampeni za Trump wala Taasisi yake iliyojua chochote kuhusu malipo,ambayo aliyatoa kutoka mfukoni mwake mwenyewe. Alisema hakurejeshewa pesa.
''Malipo kwa Bi Daniels yalikuwa yamefuata sheria'', haikuwa mchango wa kampeni wala si kwa matumizi ya kampeni.
Muda mfupi baada ya makala ya jarida hilo, Bi Daniels alizindua kampeni yake aliyoiita ''Make America Horny Again'' akisafiri kwenda South Carolina kwenye vilabu vya dansi za utupu wakati wa sherehe za maadhimisho ya kuapishwa kwa Donald Trump.
Meneja wa klabu,Jay Levy alisema alihitaji huduma yake, hiyo ilikuwa siku moja baada ya Jarida la the Wall Street kuchapisha makala kuhusu malipo ya dola za kimarekani 130,000.
Kipeperushi kuhusu sherehe hizo kilikuwa kina mzaha kusu mahusiano. Kikieleza ''alimuona moja kwa moja'' ''unaweza kumuona pia''.

Kinachoendelea sasa

Bi Daniels siku ya Jumanne alisema anamshtaki Trump, akidai kuwa hakuweka saini makubaliano yao ya kutoyaweka wazi mahusiano yao.
Mwanasheria wake, Michael Avenatti, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuhusu mashtaka yakihusishwa na nyaraka zilizowasilishwa kwenye mahakama ya California.
Siku iliyofuata, ripoti zilisambaa zikisema Rais Trump alishinda kizuizi dhidi ya Bi Daniels.
Amri hiyo ya kizuizi ilimpa marufuku Bi Daniels kutoa taarifa za siri, kuhusu kinachoelezwa kuwa uhusiano wake na Trump.
''Kesi hii ilishafanyiwa suluhisho, kama kitafanyika chochote mbali na hicho, nitafikisha kwa mshauri wa nje wa Rais'' alieleza katibu wa habari wa Ikulu Sarah Sanders siku ya Jumatano.
Mwanasheria wa Daniels amesema kuwa kauli hiyo ya Ikulu ni ''kichekesho''.
Shirika la habari, CNN liliripoti Alhamisi kuwa Rais Trump amekasirishwa na kauli ya Sanders, kwani ni mara ya kwanza kwa mtu kutoka Ikulu kuashiria kuwa Trump alikuwa kwa namna yeyote akijihusisha na Bi Daniels.

Maoni ni yapi kuhusu hayo?

Mbunge wa Congress kutoka South Carolina, Mark Sanford ni mmoja kati ya wachache waliotoa maoni, aliliambia gazeti la Washington Post kuwa madai hayo ''yanafedhehesha mno''.
Wabunge wa Democrats Ted Lieu na Kathleen Rice, wanaowakilisha jimbo la California na New York wamelitaka shirika la upelelez FBI kuchunguza malipo yaliyofanywa na Cohen kwa Bi Daniels.

Ina maana gani kwa Trump?

Shutuma hizi zimekuja wakati mgumu kidogo kwa maafisa wa White house, na hazioneshi dalili yoyote ya kuisha.
Mbali na kuwepo kwa uchunguzi kuhusu mahusiano yake na Urusi, maafisa wa Trump wamekuwa kwenye kikaango.
Hali hii ni kama inaleta kivuli cha aliyekuwa rais wa Marekani. Kumbuka Bill Clinton alikumbwa na tishio la kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye baada ya kusema uongo kuhusu uhusiano wake na staffer Monica Lewinsky.
Lanny Davis, mwanasheria aliyekuwa mshauri wa Rais Clinton, siku ya Jumatano aliwashutumu viongozi wa Republican kwa ''kusema uongo'' kwa namna wanavyomtendea Rais Trump tofauti na walivyofanya kwa Clinton.