bunduki
Monday, March 12
Afrika wiki hii kwa picha: 2-8 Machi, 2018
Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii.
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Skauti wa Kike wa Kenya ni miongoni mwa mamilioni ya watu waliosheherekea siku ya Wanawake duniani siku ya Alhamisi
Haki miliki ya picha
EPA
Image caption
Mashabiki wa Gor Mahia ya Kenya wakienda nyumbani kwa mbwembwe kuiona timu ya Tunisia club Esperance katika Michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika walitoka sare ya 0-0
Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Huyu ni shabiki wa Al Ahly ya Misri akiwa amewasha moto kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo timu yake ilishinda 4-0 dhidi ya Mounana Gabon.
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Mechi hii ilichezwa kwenye kituo cha kutunza wahamiaji nchini Libya.Ilikutanisha Timu ya Senegal(Kijani) na Cameroon(rangi ya chungwa).
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Wacheza mieleka wa Dambe wa Kaskazini mwa Nigeria wakipimana nguvu kusini mwa Lagos. Dambe ni aina ya mchezo wa kupigana.
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Mwanakikundi wa sanaa ya sarakasi wa Kibera nchini Kenya, akipumua kwa huku akitoa moto mdomoni wakati wa maonyesho jijini Nairobi Jumatano.
Haki miliki ya picha
GETTY IMAGES
Image caption
Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o alitumia uzi wa dhahabu kupamba nywele zake kwa mtindo kutoka Rwanda wakati wa sherehe za Oscar siku ya Jumapili.
Haki miliki ya picha
EPA
Image caption
Hali ya hewa ya baridi iliyokumba Ulaya Mashariki wiki hii pia kulikuwa na hali ya kuanguka kwa barafu katika milima ya Atlas nchini Morocco
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Familia hii ni moja kati ya maelfu ya watu waliokimbia machafuko Mashariki mwa Congo.Wametumia boti kuvuka Ziwa Albert kuelekea Uganda
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Siku ya Jumatatu, wanaume na wanawake walionekana wakitafuta dhahabu mjini Makeni, Sierra Leone
Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Uchaguzi wa siku ya Jumatano ulikuwa wa amani, isipokuwa maandamano yalishuhudiwa nje ya Jengo la Ofisi ya wapinzani la Sierra Leone Peoples Party (SLPP)
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Nchini Ivory Coast, kulikuwa na maandamano yanayodaiwa kupinga vitendo vinavyoelezwa visivyo haki vya watoa huduma za mazishi.
Haki miliki ya picha
EPA
Image caption
Kikundi cha wahamiaji wa Eritrea nchini Israel wakiwa wanapata picha ya pamoja kwa kuwa wanaondoka kwenye Kituo cha Holot nchini Israel, Kituo hicho kilicho katikati mwa Jangwa kinatarajiwa kufungwa lakini kwa sasa ni kituo huria ambapo wanaoshikiliwa wanakuwa huru kuondoka saa za mchana na kurejea usiku.Shirika la habari la Ulaya limeripoti.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment