Friday, August 25

ATE YAZINDUA TUZO ZA KUMPATA MWAJIRI BORA KWA MWAKA WA 2017

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

CHAMA cha Waajiri Nchini (ATE)  kimezindua rasmi Tuzo ya Mwajiri Bora kwa mwaka 2017 ikiwa ni katika kulenga tathmini mchango wa rasilimali watu ili kuwawezesha kushiriki katika utendaji wa masuala mbalimbali ya kibishara.

ATE ina jumla hya wanachama washiriki 1400 kutoka sekta binafsi na wengine 6000 wasio wanachama wa moja kwa moja wanaotoka makampuni ya biashara na baadhi ya mashirika ya umma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuoz hizo zilizoanza mwaka 2005 zikijulikana kam EYA, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE  Dkt Aggrey Mlimuka amesema kwamba tuzo ya mwajiri bora wa mwaka inalenga zaidi katika kuwatambua wanachama wake waliofanya vizuri katika kuweka mikakati bora ya kutathimini usimamizi wa rasilimali watu na shughuli za kibiashara.

Dkt Mlimuka amesema kuwa tuzo hizi zimehamasisha makampuni wanachama kuweka juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi wa mikakati ya makampuni yao kujenga  nguvu kazi yenye ujuzi, furaha, ushindani na yenye kushiriki kikamilifu katika uzalilishaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa ATE  Dkt Aggrey Mlimuka  akielezea maboresho mbalimbali waliyoyafanya katika nyanja za kumpata Mwajiri bora wa mwaka 2017 na kuzindua rasmi kuanza kumsaka mshindi wa mwaka huu kutoka kwa washiriki wanachama 1400 wa ATE, Kushoto ni Mratibu wa tuzo za Mwajiri bora Joyce Nangai na Mkurugenzi usimamizi wa fedha na utawala Dr Amrose Kessy.
Mkurugenzi Mtendaji wa TanzConsult Prof Beatus Alois Thomas akizungumzia namna watakavyotumia dodoso mbalimbali zitakazotumika kumpata Mwajiri bora kwa mwaka 2017 ikiwa ni mara ya pili kuweza kusimamia toka kuzishwa kwa tuzo hizo nchini.

Tuzo za mwaka huu zimeweza kuboreshwa katika mahitaji hasa ya kibiashara na naadhi ya vigezo vimeboreshwa  na zikijikita hasa kataika nyanja za Afya, uwiano wa kazi na maisha, waajii wanaochochea na kuwajali wafanyakazi wake, mahusiano mazuri baina ya waajiri na waajiriwa, kuwekeza katika teknolojia pamoja nadhana ya utofautishwaji na ushirikishwaji.

Upatakinaji wa mshindi wa tuzo wa mwajiri bora wa mwaka utasimamiwa na TanzConsult chini ya Prof Beatus Alois Thomas na usimamizi wa pili wa matukio mpaka kilele cha sherehe ambapo zinatarajiwa kufanyika Desemba 08 mwaka huu wakitarajiwa mgeni rasmi kuwa mmoja wa viongozi wakuu wa kitaifa.

Dkt Mlimuka aliweza kusema kuwa kwa mwaka watakuw ana tuzo za aina mbili, moja ikiwa ni kwa ajili ya makampuni binafsi na nyingine ni kwa mashirika ya serikali ili kutoa fursa na kwa upande wao kuweza kushiriki katika tuzo hizo.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini.

Shirika la Sukari la nchini Cuba linauwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.

Waziri Mkuu alikutana na Bw. Lled jana (Alhamisi, Agosti 24, 2017), wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

Waziri Mkuu alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro), Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera  ambavyo vyote vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi kitakachosalia kitauzwa nje.

Kwa upande wake Bw. Lled alisema sera za Cuba haziruhusu shirika kwenda kuwekeza nje ya nchi na badala yake wanaruhusiwa kuzisaidia nchi zinazohitaji kujenga viwanda hivyo kwa kutoa ushauri na usimamizi wa ujenzi wa miradi hiyo.

Alisema Shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika usimamizi na kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya viwanda vya kuzalisha sukari na kwamba walishatoa huduma kama hiyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil na Bolivia.

Katika hatua nyingine, Bw. Lled alisema mbali na uzalishaji sukari pia shirika hilo kupitia viwanda vyake vya sukari wanazalisha vyakula vya mifugo, asali ambayo inatumika katika viwanda vya kutengeneza vinywaji vikali pamoja nishati ya umeme.

Alisema miwa ya kuzalishia sukari katika viwanda vyao wanaipata kutoka kwenye vikundi vya ushirika wa kulima wa miwa vilivyoko katika mikoa yote nchi nzima kasoro mkoa wa Havana na PaƱar del Rio na kwa mkulima mmoja mmoja ambao kwa pamoja hukusanya miwa katika vituo ambavyo hupeleka kiwandani.

Hata hivyo alisema kuwa viwanda vyao vinanunua miwa kwa bei tofauti kulingana na ubora wa miwa na kwamba shirika lao linawasaidia wakulima kwa kuwaelimisha namna bora ya kulima pamoja na kuwaazima mashine za kuvunia wakati wa mavuno. Miwa yote nchini Cuba inavunwa kwa kutumia mashine.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAAA, AGOSTI 25, 2017.

HOSPITALI YA AGA KHAN KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI KWA WALIOKAKAMAA VIUNGO NOVEMBA 3-5 MWAKA HUU.


Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akiwasihi wananchi wenye matatizo ya viungo vilivyo kakamaa  wajitokeze katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa viungo ambavyo vimekakamaa kutokana na Kupata ajali za Moto, ajali za barabarani pamoja na ukatili wa Majumbani. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha  Upasuaji, Athar Ali.
Mkuu wa Operesheni wa Hospitali ya Aga Khan, Sisau Konte akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na namna wanatakavyofanya upasuaji wa Viungo vilivyokakamaa kutokana na ajali za moto pamoja na ajali za barabarani. Kulia ni  Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha  Upasuaji, Athar Ali.
Meneja masoko na Mawasiliano wa Hospitali ya Aga Khan, Olayce Lotha akifafanua jambo mblele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya upasuaji wa viungo vilivyokakamaa utakao kuwa unafanyika katika hospitali ya Aga Khani jijini Dar es Salaam wajitokeze kwani matibabu hayo yatakuwa hayana gharama yeyote upasuaji utakaoaza Novemba 3hadi 5 mwaka huu. Kulia ni  Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

HOSPITALI ya Aga Khan  hapa nchini imeeandaa mpango maalumu kwaajili ya upasuaji wa viungo vilivyokakamaa kutokana na  ajali za moto, ajali za barabarani pamoja na ukatili naofanyika majumbani upasuaji huo utaanza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Edwin Mrema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa mpango huo utaaza Novemba 3 hadi Novemba 5 mwaka huu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaa na kwa wakazi wa Mikoani waweze kujisajili katika Hospitali yeyote ya Aga Khani na wanaoweza kusafiri na kufika katika Hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam ambako kunatolewa hiyo huduma.

MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na  waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikagua kwa kujaribu kuziendesha Pikipiki  hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
.Muonekano wa pikipiki hizo.
 Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.

Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.

Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.

Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.

Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi msamariamwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika kwenye Hotel wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabainu Askari hao.

Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo hivyo votendeke kwenye Mkoa wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki vitendeke.

Makonda kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.

Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.

13 wafaa katika makabiliano na polisi India

Magari kadhaa yameteketezwa moto huko PanchkulaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMagari kadhaa yameteketezwa moto huko Panchkula
Yamkini watu 13 wameuwawa kaskazini mwa India, baada ya ghasia kutokea, mara baada ya mahakama moja nchini humo, kumhukumu Guru mmoja anyemiliki dhehebu lake na anayejiita mtu mzuri, kwa kosa la kuwabaka wanawake.
Idara ya polisi inasema kuwa baadhi ya waumini wa mtu huyo wanaodaiwa kufikia milioni moja, walianzisha ghasia ya kuwarushia polisi kila aina ya silaha ikiwemo mawe, mara tu mahakama ilipotoa hukumu nhiyo.
Duru kutoka mji wa Panchkula zinathibitisha kuwa watu hao 13 kweli wamefariki, huku wawili wakiwa katika hali mahututi.
Gurmeet Ram Rahim Singh anasemekana kuwa na waumini wanaofikia milioni moja, India
Image captionGurmeet Ram Rahim Singh anasemekana kuwa na waumini wanaofikia milioni moja, India
Hii ni kwa mjibu wa taarifa kutoka makao makuu ya Polisi katika jimbo la Panchkula, kaskazini mwa India.
Awali kulikuwa na hofu ya kutokea fujo, baada ya kiongozi huyo wa kidini:- Gurmeet Ram Rahim Singh, alipopatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono waumini wake wawili wa kike, katika kesi hiyo ya mwaka 2002.
Makumi kwa maelfu ya wafuasi wa Guru huyo wakimiminika mjini ChandigarhHaki miliki ya pichaMANOJ DHAKA
Image captionMakumi kwa maelfu ya wafuasi wa Guru huyo wakimiminika mjini Chandigarh
Kisa hicho kinadaiwa kufanyika katika makao makuu ya kiongozi wa kundi hilo la Dera Sacha Sauda, iliyoko katika mji wa Sirsa, Kaskazini mwa India.
Ramani ya India
Image captionRamani ya India

Yingluck Shinawatra ''atoroka Thailand''

Yingluck ShinawatraHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYingluck Shinawatra
Aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra ''ametorokea ngambo'' kulingana na duru wakati ambapo anatarajiwa kuhusu kesi inayomkabili ya uzembe.
Duru katika chama chake zinasema kuwa alichukua uamuzi huo wa kuondoka kwa ghafla, muda mfupi kabla ya kuwasili mbele ya mahakama ya juu kuhusu mashtaka ya kuzembea.
Mawakili wake wameambia mahakama kwamba alishindwa kuhudhuria kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Lakini aliposhindwa kuwasili , mahakama ilitoa agizo la kumkamata na kufutilia mbali dhamana yake.
Majaji pia waliahirisha uamuzi huo hadi Septemba 27.
Bi Yingluck amekana kufanya makosa yoyote katika mradi huo ambao uliigharimu Thailand mabilioni ya madola.
Iwapo atapatikana na hatia baada ya makosa hayo ya miaka miwili, anaweza kufungwa jela hadi miaka 10 na kupigwa marufuku katika siasa.
Duru katika chama cha bi Yingluck zimeambia Reuters kwamba aliondoka Thailand lakini hakutoa maelezo ya kule aliko.

Manji ana kesi ya kujibu




Mfanyabiashara maarufu, Yusufali Manji 

Mfanyabiashara maarufu, Yusufali Manji  
By Tausi Ally, Mwananchi mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu, Yusufali Manji amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na anatarajia kuwaita mashahidi 15 kumtetea.
Ni katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka ameridhika kuwa mshtakiwa huyo ana haki ya kujitetea na kuita mashahidi.
Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo alidai kuwa mteja wake atajitetea kwa njia ya kiapo na wana mashahidi 15.
Pia aliomba hati ya wito (samasi) kwa ajili ya kuwaita mashahidi hao. Kesi imeahirishwa hadi Agosti, 30 na 31,2017 ambapo Manji atajitetea.
Awali upande wa mashtaka ulisema ungeita mashahidi wasiozidi 10 kutoa ushahidi lakini watatu ndiyo waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo.
Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa kuwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Manji alikana kuwa siyo kweli 'No amekosea' na kwenye kesi hiyo anawakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Mosses Kimaro na yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini bondi ya Sh 10 milioni.

JK, Mkapa wakutana wakiijadili Afrika


Dar es Salaam. Marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wamekutana kwa mara ya kwanza katika jukwaa moja wakiwa nje ya nchi wakihudhuria mkutano unaoratibiwa na Uongozi Institute kwa kushirikiana na Taasisi ya Mbeki.
Mkutano huo unaomalizika leo unafanyika Johannesburg Afrika Kusini na kuhudhuriwa na marais kadhaa wastaafu.
Hii ni mara ya kwanza kwa marais hao kushiriki tukio la pamoja wakiwa nje ya nchi tangu Rais Kikwete aondoke marakani mwaka 2015. Ingawa viongozi hao wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za kimataifa lakini hawajawahi kukaa jukwaa moja wakiwa nje ya nchi.
Marais wengine wastaafu wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olusegun Obasanjo na Hassan Sheikh Mohamud aliyekuwa rais wa Somalia.
Picha za video zinazorusha mkutano huo zimewaonyesha marais hao wakiwa katika jukwaa moja wakipiga picha baada ya kumaliza majadiliano ya sehemu ya kwanza.
Katika upigaji picha, Rais Kikwete ameonekana akiwa ameketi mwanzo akiwafuatiwa na rais wa Nigeria, Obasanjo na kisha kufuatiwa na Mahamud wa Somalia. Rais Mkapa ameketi nafasi ya nne akifuatiwa na kiongozi mwingine ambaye hakuweza kutambulika mara moja na mwishoni aliketi Rais Thabo Mbeki ambaye taasisi yake ndiyo mwenyeji wa mkutano huo.
Mara baada ya kumalizika kwa shughuli ya upigaji picha, Rais Kikwete alionekana akijadiliana jambo kwa karibu na Rais Obasanjo na kisha viongozi hao waliteremka kutoka jukwaani.
Wakati akielekea kwenye eneo lake Kikwete aliwasalimia wageni kadhaa ndani ya mkutano huo na baadaye alielekea sehemu aliyokuwa amesimama aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue na kuonekana akimsisitizia jambo na kisha akaondoka.
Viongozi hao wamekuwa wakijadiliana kuhusu masuala ya demokrasia, utawala bora na jinsi ya kuzisaidia nchi za Afrika kusonga mbele kimaendeleo.

Wakili ashauri kesi ya Kitilya ifutwe

Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji wa Mitaji na

Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma), Harry Msamire Kitilya 
Dar es Salaam.  Wakili Majura Magafu ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuulazimisha upande wa mashtaka kuifuta kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Mwenyekiti wa Kampuni ya Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (Egma), Harry Msamire Kitilya na wenzake ama waiondoe wenyewe kwa uungwana wao.
Ombi hilo, aliliwasilisha leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, mara baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa kudai upelelezi haujakamilika na kwamba bado hawajapokea awamu ya pili ya nyaraka kutoka Uingereza.
Baada ya kutolewa maelezo hayo, Magafu alisema umefika wakati maelekezo yanayotolewa na mahakama yaheshimiwe na kuheshimiwa.
Magafu alidai kuwa mahakama haifungwi mikono kuulazimisha upande wa mashtaka kuifuta kesi hiyo ama waifute wenyewe kwa uungwana wao.
Kwa sababu washtakiwa hao awali walikuwa na dhamana na walikuwa wakiripoti kila walipohitajika Takukuru.
"Nadhani utaratibu huo unaweza kutumika na upande wa mashtaka watakapokamilisha upelelezi wawalete mahakamani,"alieleza Magafu.
Alibainisha kuwa tangu upande wa mashtaka useme umekwisha pokea awamu ya kwanza ya nyaraka toka Uingereza, ni miezi sasa na imekuwa hadithi kuwa vya awamu ya pili bado havijafika. Hivyo aliiomba mahakama kutumia mamlaka yake kuifuta.
Wakili Msigwa alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unavuka mipaka na kwamba si kuwa Jamhuri imelala, inahangaika kufanya mawasiliano na upande zote.
Hakimu Mkeha alimueleza Magafu kuwa anafahamu mahakama haina mamlaka kwenye kesi hiyo na akaiahirisha hadi Septemba 9, 2017.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni maofisa wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.  Washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo Agosti, 17, 2016.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Mfungwa auawa kwa kutumia sumu mpya Florida, Marekani

Mark AsayHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMark Asay alikiri kumuua McDowell, lakini akakanusha kutekeleza mauaji hayo mengine.
Mzungu mtetea ubabe wa wazungu ambaye akliwaua watu kwa sababu ya asili yao miaka 30 iliyopita ameuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu.
Mark Asay ndiye mzungu wa kwanza katika historia ya jimbo la Florida kuuawa kwa sababu ya kumuua mtu mweusi, kwa mujibu wa shirika linalofuatilia utekelezaji wa hukumu ya kifo.
Asay, 53, alipatikana na hatia ya mauaji ya watu wawili mwaka 1987 katika eneo la Jacksonville.
Aliuawa saa 22:22 GMT (saa saba na dakika 22 Afrika Mashariki).
Ilikuwa mara ya kwanza kwa sindano yenye sumu mpya kutumiwa kumuua mfungwa.
Jopo la mahakama liliamua Asay aliwaua waathiriwa wake - Robert Lee Booker, mtu mweusi, na Robert McDowell, 26, mzungu wa asili ya Kilatino - kwa kuwapiga risasi usiku ambao alikuwa ametoa matamshi ya ubaguzi wa rangi.
Waendesha mashtaka walisema Asay alikuwa amemchukua McDowell, aliyekuwa amevalia kama mwanamke, akashiriki naye ngono, lakini akampiga risasi baada ya kugundua jinsia yake halisi.
Tangu kurejeshwa kwa hukumu ya kifo mwaka 1976, watu weusi 20 wameuawa kwa makosa ya kuwaua wazungu.
Asay aliuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu aina ya etomidate ambayo haijawahi kutumiwa awali Marekani.
Sumu hiyo sasa itaanza kutumiwa badala ya sumu aina ya midazolam ambayo imeacha kutumiwa kwa sababu ya kuwasababishia dhiki watu waliohukumiwa kuuawa wakati wanapouawa.
Etomidate ilichanganywa na sumu nyingine mbili - rocuronium bromide na potassium acetate - kabla ya Asay kudungwa.
Katika mahojiano na kituo kimohc acha habari, Asay alikuwa amesema kwamba hataki kuishi jela maisha yake yote.
Mfungwa huyo alikuwa na chale zenye kuonyesha ubabe wa wazungu. Alikiri kumuua McDowell, lakini akakanusha kutekeleza mauaji hayo mengine.
Alikuwa mungwa wa kwanza kuuawa Florida katika kipindi cha miaka 18.

Mwanamke ajishindia $758m kwenye jackpot Marekani

Mavis Wanczyk
Mshindi wa pesa nyingi zaidi kuwahi kujishindiwa na mtu binafsi katika shindano la bahati nasibu Amerika Kaskazini - jumla ya $758.7m (£590m) - amejitokeza kuchukua zawadi yake, na ni mwanamke.
Mavis Wanczyk, 53, mama wa watoto wawili, alinunua tiketi yake ya ushindi katika kituo cha mafuta Chicopee, Massachusetts.
Mshindi huyo, ambaye namba zake za bahati zilikuwa 6, 7, 16, 23 na 26, na 4 - ameambia wanahabari kwamba tayari ameacha kazi.
Zawadi ya juu zaidi ya jackpot katika shindano la bahati nasibu ya kampuni ya US Powerball kuwahi kutolewa ilikuwa $1.6bn, lakini ilienda kwa washindi watatu ambao waligawana pesa hizo Januari 2016.
Wasimamizi wa mashindano ya bahati nasibu jimbo la Massachusetts waliambia wanahabari kwamba tiketi ya mwanamke huyo ambayo ilishinda Jumatano imethibitishwa kuwa halisi.
"jambo ninalotaka kufanya kwa sasa ni kuketi na ktuulia," alisema Bi lWanczyk.
Pride petrol station in the city of ChicopeeHaki miliki ya pichaWBZ-TV)
Image captionTiketi ya ushindi ilinunuliwa katika kituo hiki cha mafuta Chicopee, Massachusetts
"Ni ndoto kuu ambayo imetimia."
Amewaambia wanahabari kwamba alichagua namba zake kwa kutumia tarehe za kuzaliwa za jamaa zake.
Bi Wanczyk, kuhusu kazi yake aliyoifanya kwa miaka 32 katika kituo cha matibabu, amesema: "Niliwapigia simu na kuwaambia sitafika tena kazini."
Aliongeza kwamba "nitaenda na kujificha kitandani mwangu".
Waandishi walimwuliza iwapo anapanga kujizawadi kwa vitu vizuri, mfano gari la kifahari.
Lakini Bi Wanczyk amejibu kwamba alinunua gari jipya chini ya mwaka mmoja uliopia, kwa mkopo, na sasa anapanga kulipa kiasi kilichosalia.
Afisa mmoja wa mashindano ya bahati nasibu laimweleza mwanamke huyo kama "mkazi wa kawaida sana wa Massachusetts".
Watu wakisubiri kununua tiketi za bahati nasibu Hawthorne, CaliforniaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWatu wakisubiri kununua tiketi za bahati nasibu Hawthorne, California
Aliongeza kwamba anaonekana kama mwanamke mwenye bidii sana na kwamba bila shaka ana furaha isiyo na kifani.
Mwenye kituo cha petroli cha Pride, kilichopokea zawadi ya $50,000 inayotolewa kwa duka linalouza tiketi ya ushindi Bob Bolbuc amesema atatoa pesa hizo kwa hisani.
Malipo ya zawadi hiyo ya Jackpot, ambayo yanaweza kufanywa kwa awamu mara 29 kwa mwaka, au mara moja, yanakadiriwa kuwa karibu $443m baada ya kutozwa ushuru.
Mwenyekiti wa kampuni ya Powerball Charlie McIntyre amesema kupitia taarifa kwamba kuna tiketi nyingine sita - zilizouzwa Connecticut, Illinois, Louisiana, New Mexico, Pennsylvania na visiwa vya Virgin Islands - ambapo kila mmoja alishinda $2m.
Tiketi nyingine zilishinda $1m.
Maafisa wa mashindano ya bahati nasibu Massachusetts awali walisema tiketi hiyo iliuzwa Watertown, Boston lakini baadaye wakasahihisha hilo Alhamisi asubuhi.
Haijabainika kosa hilo lilitokea vipi.
Uwezekano wa kushinda jackpot hiyo ulikuwa moja kati ya 292.2 milioni.