Sunday, October 1

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, RAMO MAKANI AFUNGUA KONGAMANO LA MAONESHO YA UTALII YA KARIBU KUSINI.


Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kleruu wakifuatilia maada inayowasilishwa kuhusiana na Mradi wa SPANEST jinsi inavyoshirikisha wananchi katika masuala ya uhifadhi mara baada ya kufunguliwa kwa kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa. (Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, (katikati) wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jamhuri David, wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya Waandaji wa kongamano mara baada ya kufungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa (Picha na Lusungu Helela- MNRT).




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani, amefungua kongamano la maonesho ya utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwa mara ya pili mjini Iringa.

Kongamano hilo limefanyika kwa muda wa siku moja katika Ukumbi wa Chuo cha Walimu wa Kleruu likiwakutanisha wasomi na wahadhiri kutoka vyuo vikuu nchini, wanafunzi pamoja na wadau wa utalii wanaofanya shughuli za kiutalii likiwa na lengo la kutathmini na kuangalia namna mikoa ya Nyanda za Juu Kusini inavyoweza kunufaika kutokana na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.

Sambamba na kongamano hilo, maonesho hayo yanaendelea kufanyika hadi Oktoba 2 katika viwanja katika viwanja vya Kichangani yakiwa yamewakutanisha Wajasiriamali wadogo 350 kutoka kona zote za mikoa hiyo.Akizindua Kongamano hilo Naibu Waziri Makani amewataka wananchi kuanza kuutupia macho utalii wa nje ya hifadhi kwa kuwa watalii wengi kwa sasa hawaji kuangalii wanyamapori pekee.

Amesema watalii wa siku hizi wamechoka kuangalia wanyamapori wanataka kujifunza kuhusu utamaduni wetu pamoja na vyakula vyetu vya kiasili.Mbali na kuwa na utajiri wa makabila tofauti tofauti, Makani alisema Nyanda za juu Kusini imejaliwa kuwa na vivutio vya Malikale ambayo bado havijatangazwa vya kutosha.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga alisema Iringa inasifika kwa kuzalisha wataalamu wa tasnia ya utalii kutokana na uwepo wa chuo Kikuu cha Tumaini kuwa ndo chuo cha kwanza kutoa shahada ya Utalii lakini imekuwa nyuma kiutalii akitolea mfano wa hoteli zinazojengwa ni za chini ya kiwango licha ya watalaam kuwepo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, David Jamhuri alisema mkoa umejipanga kuhakikisha kuwa fursa za utalii kwa mikoa ya Nyanda za juu Kusini zinafunguka kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa wa kwanza kunufaika kutokana namipango waliyojiwekea

Pia aliwataka viongozi wa Kiserikali kila wanapopata nafasi ya kuzungumza na wananchi watumie fursa hiyo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Muongoza watalii wa Kampuni ya Chabo Tours, Serafino Liduino aliitaka Serikali kuanza kuona umuhimu wa kutoa mafunzo mashukeni ili kutengeneza kizazi kinachojua thamani ya kuhifadhi mazingira ili vivutio asilia viendelee kuwepo kutokana na tishio la mabadiliko ya tabia ya nchi yanajitokeza kwa sasa.

CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO


Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 
SERIKALI ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 29.4 kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu ya ufundi stadi, utalii wa kijiolojia na kukarabati wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong. 
Bw. Doto James alisema kuwa kiasi cha Shilingi bilioni 22.4 cha msaada huo kitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera, ambacho kitakapo kamilika kitadahili zaidi ya wanafunzi 400. 
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” alisema Bw. James 
Alieleza kuwa kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. 
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” alisema Bw. James 
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James alibainisha kuwa katika makubaliano ya msaada huo, Jamhuri ya watu wa China, itatoa kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Dar es Salaam. 
“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Alifafanua Bw. James 
Bw. Doto James alisema kuwa kiasi kingine cha shilingi  milioni 300 kitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha. 
Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa 
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo” aliongeza Bw. Doto James. 
Aliishukuru China kwa ushirikiano wake wa dhati na Tanzania tangu miaka ya 1960 na kwamba mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuipiga jeki Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Gou Haodong, amesema kuwa nchi yake inatarajia kwamba ujenzi wa Chuo Cha Ufundi VETA huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa. 
Kuhusu masauala ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, alisema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea. 
“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii elfu 20 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” aliongeza Mhe. Haodong 
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo alisema kuwa hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.77 na kukuza ajira nchini. 
Ameitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyowekezwa kuwa ni pamoja na mradi wa miundombinu ya mtandao (Tanzania ICT Broadband backbone), Bomba la gesi la kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi wa kuboresha miundombinu ya Bandari, barabara na madaraja. 
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, ambaye alisema kuwa msaada wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA mkoani Kagera kitaongeza watalaamu watakaosaidia kuendeleza sekta ya viwanda nchini.

KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKINGA AFUNGUA KONGAMANO LA WAZEE MJINI DODOMA

CYBER SECURITY DAY AT COURTYARD HOTEL IN DAR ES SALAAM OCTOBER 20, 2017


HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM



Uturuki yafungua kambi kubwa ya kijeshi Somalia

Kambi ya Kijeshi ya Uturuki nchini SomaliaHaki miliki ya pichaFACEBOOK/SOMALIA
Image captionKambi ya Kijeshi ya Uturuki nchini Somalia
Uturuki imefungua kambi kubwa ya kijeshi mjini Mogadishu, Somalia.
Hii itakuwa kambi yake kubwa kabisa ya mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.
Kambi hiyo itayokuwa kando ya bahari, ina uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Somalia, zaidi ya 1500 kwa wakati mmoja
Lengo ni kulipa nguvu jeshi la Somalia, kupambana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.
Wanajeshi zaidi ya 20,000 wa Umoja wa Afrika na wengine wa kigeni, wanapigana na Al Shabaab hivi sasa.
Kuna kambi kadhaa za majeshi ya kigeni nchini Somali.

Marekani na China kuijadili Korea Kaskazini

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson na mwenzake wa China Wang Yi
Image captionWaziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson na mwenzake wa China Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yuko mjini Beijing kufanya mazungumzo na viongozi wa China.
Ajenda kuu katika mkutano huo ni mzozo katika rasi ya Korea.
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni
Utawala wa Trump unaamini China ina umuhimu mkubwa, katika juhudi za kuishurutisha Korea Kaskazini kusitisha uundaji wa silaha zake za Nuklia
China imeonyesha kujitolea kwake katika utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya taifa hilo.
Siku ya Alhamisi, Beijing ilitangaza kuwa mashirika ya Korea Kaskazini yanayoshirikiana na China hayana budi kufungwa.
Ziara ya Tillerson inakuja huku Rais Trump akitarajiwa kutembelea taifa hilo baadaye mwezi Novemba.

Iran: Tunataraji Marekani itaturuhusu tuendelee na mpango wa Kinyuklia

Waziri mkuu wa Iran Javad ZarifHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaziri mkuu wa Iran Javad Zarif
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Mohammed Javad Zarif amesema kuwa anatumai Marekani itafutilia mbali makubaliano ya kimataifa yanayoizuia Iran kuendelea na mipango yake ya Kinyuklia.
Bunge la Marekani mwezi ujao litaanza mkakati wa kuiweka vikwazo Iran iwapo rais Trump atasema kuwa Iran imeshindwa kuafikia makubaliano yaliowekwa.
Katika mahojiano na magazeti mawili ya Uingereza ,bwana Zarif alikuwa na matumaini kwamba Ulaya wataafikia makubaliano hayo.
Amehoji kwamba iwapo Marekani itaendelea kuliwekea vikwazo vipya taifa hilo, Ulaya italazimika kuwapatia kinga ya kesheria wawekezaji wake nchini humo.
Amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Iran huenda ikaiwekea masharti Marekani.
Amesema kuhusu rais Trump: Nadhani ameweka sera ya kutoeleweka na sasa amebadilika na kuwa mtu asioaminika .Amekiuka makubaliano ya mkataba hauo.
Bwana Zarif amesema kuwa chaguo la Iran litategemea na makubaliano ya jamii ya kimataifa na Marekani .
''Iwapo Ulaya, Japan, Urusi na China zitaamua kuiunga mkono Marekani basi nadhani huo utakuwa mwisho wa mkataba huo.Ulaya inafaa kuongoza''.
Wanachama wa muungano wa Ulaya wamesema kuwa watachukua hatua ya kuwalinda kisheria wawekezaji wao iwapo Marekani itaiongezea vikwazo Iran.
Lakini pamoja na Marekani wameikosoa Iran dhidi kuhusu vitendo vyake katika eneo hilo.

Afisa mkuu wa Kenya aliyeshambuliwa na al-Shabab azikwa

Mwili wa Mariam El Maawy hatimaye wazikwa jini NairobiHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionMwili wa Mariam El Maawy hatimaye wazikwa jini Nairobi
Hali ya uzuni iligubika nyumba ya aliyekuwa katibu mkuu katika wizara ya nguvu kazi Mariam El Maawy ,ambapo maafisa wa serikali walijumuika na familia yake kuomboleza kifo cha afisa huyo kabla ya kumzika katika makaburi ya Waislamu ya Langata jijini Nairobi.
Katibu huyo ambaye amemwacha mtoto mmoja alisifiwa kuwa mfanyikazi wa serikali aliyejitolea ambaye alifariki akiwa kazini katika kaunti ya Lamu baada ya gari alimokuwa ndani kutekwa na wapiganaji wa al-Shabab.
Mwanawe Leila El Maawy ,akimuomboleza mamake alisema kuwa alimpoteza mzazi na rafiki.
''Alijitolea sana kuimarisha familia yake ,bibi yangu...kwangu mimi tutampenda sana.Iwapo angekuwa hapa angeuliza: Hii yote ni yangu.Ni mtu ambaye alipenda wengine zaidi na hakutarajia malipo kwa kila kitu alichowafanyia watu, alisema Leila akibubujikwa na machozi.
Natumai nitakuwa nusu ya mamaangu tu.Tulikupenda sana mama na tutakuenzi''.
Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya waliohudhuria mazishi hayo walikuwa waziri wa maswala ya nchi za kigeni Amina Mohammed, waziri wa Ulinzi Rachel Omamo, Jacob Kaimenyi, Dan Kazungu na Najib Balala.
Bi El Maawy alifariki nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia shambulio la wapiganaji wa al-Shabab mnamo Julai 13.
Alshabab walimpiga risasi na kumjeruhi katibu huyo katika bega na miguu baada ya kumteka nyara katika eneo la Milihoi katika barabara ya Mpeketoni Lamu.
Mpwa wake ambaye alikuwa akijifunza urubani na ambaye walikuwa pamoja alifariki wakati wa shambulio hilo lakini Bi Maawy aliokolewa na kundi la wanajeshi wa Kenya KDF pamoja na wale wa GSU.
Kundi la maafisa wa usalama lilimkimbiza katika hospitali ya Mpeketoni.
Baadaye alisafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu.
Wakati wa shambulio hilo, wapiganaji hao walidhibiti gari alimokuwa katibu huyo ambalo lilikuwa na watu sita kabla ya kutoroka katika kichaka.
Ndege ya KDF ililifuata gari hilo na kufanikiwa kumuokoa afisa huyo.
Maafisa wawili wa polisi pia walifariki wakati wa shambulio hilo huku wengine wawili wakitekwa na wapiganaji hao.
Siku ya shambulio hilo, katibu huyo alikuwa amehudhuria mkutano kuhusu bandari ya Lamu, barabara ya Sudan kusini, Ethiopia katika kituo cha Huduma mjini Lamu akielekea Witu.

10 wafariki baada ya ndege ya kijeshi kuanguka DR Congo

Picha ya ndege ya kijeshi ilioanguka
Image captionPicha ya ndege ya kijeshi ilioanguka
Ndege ya kijeshi imeanguka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwaua abiria wote.
Maafisa wa maswala ya angani wamesema kuwa zaidi ya watu 10 wamefariki baada ya ndege hiyo kufeli kupaa vizuri kutoka uwanja wa ndege wa N'djili katika mji mkuu wa Kinshasa na kuanguka katika makaazi ya Nsele.
Haijabainika iwapo kuna watu wowote waliouawa ama kujeruhiwa ardhini.
Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kinshasa amesema kuwa ndehe hiyo ilikuwa ikibeba mizigo na kwamba haikuwa na abiria wowote.
Ripoti nyengine zinasema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuawa.

Kampuni ya China yawanusuru tembo wanne Tanzania

Ndovu waliokwama wanusuriwa Tanzania
Image captionNdovu waliokwama wanusuriwa Tanzania
Kampuni ya ujenzi ya China Sinohydro imewapeleka wahandisi wake na tingatinga katika eneo la kuhifadhi wanyama pori la Rungwe katikati ya Tanzania ili kuwaokoa tembo watano waliokwama katika shimo.
Ndovu wanne wakiwemo watoto wawili waliokolewa lakini ndovu mmoja mkubwa alifariki kutokana na ukosefu wa maji kulingana na chombo cha habari cha China Xinhua.
Kulingana na duru kutoka kwa kampuni ya Sinohydro, baadhi ya wakaazi wa manyoni eneo la Singida waliwaita wafanyikazi wa kampuni hiyo kuwasaidia tembo hao yapata kilomita 40 kutoka katika hifadhi hiyo.
Saa moja baadaye, waokoaji hao wa China waliwasili katika eneo hilo na kuanza uokoaji baada ya kupata ruhusa kutoka kwa gavana wa eneo hilo na wasimamizi wa hifadhi hiyo.
Ndovu wavamia chuo kikuu cha Dodoma Tanzania
Kulingana na Xhinua wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa wanyama hao walianguka katika shimo hilo walipokuwa wakitafuta maji.
Shimo hilo lilikuwa dogo na kuwalazimu ndovu hao kuanza kusukumana kwa hofu.
Baada ya saa tano za kazi ngumu ya kuwanusuru, ndovu mmoja mkubwa na watoto wake walikuwa wa kwanza kutolewa katika shimo hilo.
Ndovu wengine wawili walifuatia baadaye lakini mmoja mkubwa akaaga dunia.

Marekani yadai kuwasiliana na Korea Kaskazini ''moja kwa moja''

Rais Xi Jinping wa China na waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex TillersonHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Xi Jinping wa China na waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson
Marekani inawasiliana na Korea Kaskazini ''moja kwa moja'', kulingana na waziri wa maswala ya kigeni Rex Tillerson.
Bwana Tillerson alisema kuwa Washington ilikuwa unachunguza uwezekano wa mazungumzo na Pyongyang, ''kwa hivyo subirini''.
''Tunawasiliana na Pyongyang'', alisema wakati wa ziara ya China.Hatuko katika hali mbaya''.
Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni lakini haikujulikana kwamba walikuwa wakiwasiliana.
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiangamiza Korea Kaskazini , akisema kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-Un, ''anahatarisha maisha yake'' hatua iliomshinikiza rais huyo wa Korea Kaskzini kutoa taarifa akiapa kumnyamazisha kwa vita rais huyo wa Marekani aliyemtaja kuwa ''mtu mwenye akili punguani''.
Korea Kaskazini iliendeleza cheche hizo za maneno siku ya Jumamosi , ikitoa taarifa iliomtaja rais Trump kuwa mzee mwenye akili punguani anayehatarisha maisha yake kwa kuitisha shambulio la nyuklia ambalo litaiangamiza Marekani.
Cheche hizo za maneno zinajiri kufuatia majaribio ya mara kwa mara ya makombora na Pyongyang inasema kuwa mnamo Septemba 3 ilifanikiwa kulifanyia majaribio bomu la hydrogen linaloweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu.
Majaribio hayo yalishutumiwa na jamii ya kimataifa , huku Umoja wa Mataifa ukiiwekea vikwazo Korea Kaskazini kwa lengo la kuishinikiza kusitisha utengezaji wa makombora.
Bwana Tillerson yuko nchini China akikutana na rais Xi Jinping na maafisa wengine akitumai kuwashawishi kutekeleza vikwazo hivyo.
Wiki hii China iliwaambia wafanyibiashara wa Korea Kaskazini wanaotekeleza operesheni zao ndani ya taifa hilo kufunga bishara zao.
Hatahivyo China bado inaunga mkono majadiliano na Korea Kaskazini.

OJ Simpson aachiliwa kutoka gerezani huko Nevada, Marekani

image of OJ being released from Nevada prison, wearing all denim signing a document on a tableHaki miliki ya pichaNEVADA DEPARTMENT OF CORRECTIONS
Image captionOJ Simpson aachiliwa kutoka gerezani huko Nevada, Marekani
Aliyekuwa nyota wa kandanda na muigizaji nchini Marekani OJ ameachiliwa kutoka gerezani kwa msamaha baada ya kutumikia kifungo cha mika 9 kwenye gereza la Nevada.
Amekuwa gerezani kwa makosa ya wizi wa mabavu kwa kutumia silaha hatari na mashtaka mengine 10 ya mwaka 2o17 kwenye hoteli moja huko Vegas.
Mwaka 1995 aliondolewa mashtaka ya kumuua aliyekuwa mke wake Nocole Brown Simpson na rafiki wake Ron Goodman
Video zilizochapishwa kwenye mtandao wa Facebook zilionyeha akisaini stakabadhi na akiondoka kituo cha Lovelock Correctional Center mapema Jumapili.

Injini ya ndege ya abiria ya Air France, yaharibika angani

Abiria waliona injini iliyoharibika kupitia dirisha la ndege na wakapiga picha
Image captionAbiria waliona injini iliyoharibika kupitia dirisha la ndege na wakapiga picha
Ndege moja kubwa ya abiria ya AirFrance, muundo wa Airbus 380, imelazimika kutua kwa dharura baada ya injini yake moja kuharibika vibaya, ndege hiyo ikiwa angani.
Ndege hiyo superjumbo ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles- Marekani kutoka mji mkuu wa Ufaransa- Paris, ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.
Bawa la ndege halikuharibika vibaya, hatua iliyosababisha ndege hiyo kutua uwanjani vyema
Image captionBawa la ndege halikuharibika vibaya, hatua iliyosababisha ndege hiyo kutua uwanjani vyema
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, lakini abiria walisalia ndegeni kwa saa kadhaa, baada ya ndege hiyo ya abiria kutua.
Wakati wa kisa hicho, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 496 na wafanyikazi 24. Hayo ni kwa mjibu wa msemaji wa Air France spokesperson, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
Njia ya ndege hiyo angani
Image captionNjia ya ndege hiyo angani
David Rehmar, mekanika wa zamani ambaye alikuwa abiria katika ndege hiyo, ameiambia BBC kuwa, kutokanana na uchunguzi wake, kisa hicho huenda kilitokana na kushindwa kwa feni ya injini ya ndege hiyo.
Anasema kuwa kulitokea ghafla, baada ya mlio mkubwa kusikika, ambayo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria.