Sunday, October 1

Afisa mkuu wa Kenya aliyeshambuliwa na al-Shabab azikwa

Mwili wa Mariam El Maawy hatimaye wazikwa jini NairobiHaki miliki ya pichaFACEBOOK
Image captionMwili wa Mariam El Maawy hatimaye wazikwa jini Nairobi
Hali ya uzuni iligubika nyumba ya aliyekuwa katibu mkuu katika wizara ya nguvu kazi Mariam El Maawy ,ambapo maafisa wa serikali walijumuika na familia yake kuomboleza kifo cha afisa huyo kabla ya kumzika katika makaburi ya Waislamu ya Langata jijini Nairobi.
Katibu huyo ambaye amemwacha mtoto mmoja alisifiwa kuwa mfanyikazi wa serikali aliyejitolea ambaye alifariki akiwa kazini katika kaunti ya Lamu baada ya gari alimokuwa ndani kutekwa na wapiganaji wa al-Shabab.
Mwanawe Leila El Maawy ,akimuomboleza mamake alisema kuwa alimpoteza mzazi na rafiki.
''Alijitolea sana kuimarisha familia yake ,bibi yangu...kwangu mimi tutampenda sana.Iwapo angekuwa hapa angeuliza: Hii yote ni yangu.Ni mtu ambaye alipenda wengine zaidi na hakutarajia malipo kwa kila kitu alichowafanyia watu, alisema Leila akibubujikwa na machozi.
Natumai nitakuwa nusu ya mamaangu tu.Tulikupenda sana mama na tutakuenzi''.
Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya waliohudhuria mazishi hayo walikuwa waziri wa maswala ya nchi za kigeni Amina Mohammed, waziri wa Ulinzi Rachel Omamo, Jacob Kaimenyi, Dan Kazungu na Najib Balala.
Bi El Maawy alifariki nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia shambulio la wapiganaji wa al-Shabab mnamo Julai 13.
Alshabab walimpiga risasi na kumjeruhi katibu huyo katika bega na miguu baada ya kumteka nyara katika eneo la Milihoi katika barabara ya Mpeketoni Lamu.
Mpwa wake ambaye alikuwa akijifunza urubani na ambaye walikuwa pamoja alifariki wakati wa shambulio hilo lakini Bi Maawy aliokolewa na kundi la wanajeshi wa Kenya KDF pamoja na wale wa GSU.
Kundi la maafisa wa usalama lilimkimbiza katika hospitali ya Mpeketoni.
Baadaye alisafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu.
Wakati wa shambulio hilo, wapiganaji hao walidhibiti gari alimokuwa katibu huyo ambalo lilikuwa na watu sita kabla ya kutoroka katika kichaka.
Ndege ya KDF ililifuata gari hilo na kufanikiwa kumuokoa afisa huyo.
Maafisa wawili wa polisi pia walifariki wakati wa shambulio hilo huku wengine wawili wakitekwa na wapiganaji hao.
Siku ya shambulio hilo, katibu huyo alikuwa amehudhuria mkutano kuhusu bandari ya Lamu, barabara ya Sudan kusini, Ethiopia katika kituo cha Huduma mjini Lamu akielekea Witu.

No comments:

Post a Comment