Waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Mohammed Javad Zarif amesema kuwa anatumai Marekani itafutilia mbali makubaliano ya kimataifa yanayoizuia Iran kuendelea na mipango yake ya Kinyuklia.
Bunge la Marekani mwezi ujao litaanza mkakati wa kuiweka vikwazo Iran iwapo rais Trump atasema kuwa Iran imeshindwa kuafikia makubaliano yaliowekwa.
Katika mahojiano na magazeti mawili ya Uingereza ,bwana Zarif alikuwa na matumaini kwamba Ulaya wataafikia makubaliano hayo.
- Iran yaitahadharisha Marekani kuhusu vikwazo
- Marekani yaiwekea Iran vikwazo
- Iran yatimua meli ya Marekani
- Meli ya Marekani yaionya ile ya Iran
Amehoji kwamba iwapo Marekani itaendelea kuliwekea vikwazo vipya taifa hilo, Ulaya italazimika kuwapatia kinga ya kesheria wawekezaji wake nchini humo.
Amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Iran huenda ikaiwekea masharti Marekani.
Amesema kuhusu rais Trump: Nadhani ameweka sera ya kutoeleweka na sasa amebadilika na kuwa mtu asioaminika .Amekiuka makubaliano ya mkataba hauo.
Bwana Zarif amesema kuwa chaguo la Iran litategemea na makubaliano ya jamii ya kimataifa na Marekani .
''Iwapo Ulaya, Japan, Urusi na China zitaamua kuiunga mkono Marekani basi nadhani huo utakuwa mwisho wa mkataba huo.Ulaya inafaa kuongoza''.
Wanachama wa muungano wa Ulaya wamesema kuwa watachukua hatua ya kuwalinda kisheria wawekezaji wao iwapo Marekani itaiongezea vikwazo Iran.
Lakini pamoja na Marekani wameikosoa Iran dhidi kuhusu vitendo vyake katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment