Thursday, November 9

Kizza Besigye atumia medani kuwakwepa polisi


Kampala, Uganda. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ametumia medani kukwepa mtego wa polisi waliokuwa wamkamate baada ya kukaidi agizo lao.
Awali, mwanasiasa huyo alikaidi agizo la polisi waliomwamuru kuondoka katika eneo la viwanja vya Kuanda lililopo Manispaa ya Gulu.
Licha ya polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu, Besigye hakuwa tayari kuondoka.
Baada ya tafrani kupamba moto, Besigye alibadilisha gari na kupanda lingine aina ya Toyota Prado ambalo awali lilitumiwa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama chake cha FDC.
Kabla ya hatua hiyo, Besigye alikuwa ndani ya gari lake huku polisi wakiendelea kurusha mabomu ya kutoa machozi kwa lengo la kutaka kiongozi huyo kutoka ndani ya gari.
Baada ya kuona juhudi za kumwondoa zimeshindikana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Aswa aliwaamuru askari kulikamata gari lake na kulipeleka kituo cha Guru.
Askari walipojaribu kuzuia gari la kiongozi huyo, alikuwa tayari ameondoka eneo la tukio akielekea mjini Kampala.
Katibu wa uenezi wa chama cha  FDC, Kelly Komakech aliliambia gazeti la Daily Monitor kuwa polisi hawakujua gari lililombeba Besigye na jinsi lilivyoondoka.
“Besigye aliondoka na kuwashinda askari. Walijaribu kumfuata lakini hawakuweza,” alisema.
Hata hivyo, msemaji wa polisi, Jimmy Okema alipuuza madai ya polisi kupigwa chenga na Besigye akisema walikubaliana kiongozi huyo aondoke katika eneo hilo.
Mwanasiasa huyo aliyewania urais kwa mara nne alikuwa ameambatana na viongozi wengine kadhaa wa chama chake kwa ajili ya mkutano ambao polisi walisema haikuwa halali.

Nec yakamilisha vifaa vya kupigia kura



Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa maandalizi ya vifaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani unaofanyika katika kata 43 yamekamilika na awamu ya pili ya vifaa vitaanza kusafirishwa kesho Ijumaa kwenda katika kata husika.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Kailima Ramadhani, amesema leo Novemba 9  kwamba vifaa vitakavyosafirishwa kuanzia ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo, makarani waongozaji pamoja na  mfano wa karatasi za kupigia kura.
Amesema  awamu ya kwanza ya kusafirisha vifaa ulifanywa na tume wakati wa mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi ambayo yalifanyika mjini Dodoma ambavyo vilitumika wakati wa uteuzi wa wagombea udiwani katika kata zote.
“Napenda kuwahakikishia umma kwamba tume imejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huu na maandalizi ya kupeleka vifaa katika husika yako vizuri na awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa itapaelekwa Ijumaa ,”amesema  Ramadhani.
Amesema awamu ya tatu ya usafirishaji wa vifaa itahusisha  vifaa vichache ambavyo ni karatasi za kupigia kura pamoja na fomu za kutangazia washindi ngazi ya kituo na ngazi ya kata.
Naye Mkurugenzi wa Manunuzi, Ugavi na Logistiki wa NEC Eliud Njaila, amesema kwamba NEC imepeleka vifaa vya kutosha katika vituo vyote 893  vilivyoko katika kata 43 na hakutakuwa na upungufu wowote.
Amesema  kwamba katika awamu ya pili ya upelekaji wa vifaa, wameweka na mfano wa karatasi za kupigia kura ili wadau ambavyo ni vyama vya siasa vijiridhishe kuhusu karatasi hivyo zitakavyokuwa pamoja na kufanya uhakiki wa majina wa wagombea wao.
“Tunaamini kwamba vyama vya siasa vitahakiki majina ya wagombea wao kwa kila kata ili kama kuna masahihisho wayalete mapema na NEC iweze kufanya masahihisho haraka wakati wa kuchapa karatasi halisi za kupigia kura,” amesema Njaila.

Simba anayeumwa ngiri afanyiwa upasuaji Ngorongoro

Madaktari wa wanyama wakimfanyika upasuaji
Madaktari wa wanyama wakimfanyika upasuaji Simba aliyekuwa na uvimbe mwilini mwake katika hifadhi ya Ngorongoro, Arusha jana.Picha na (WMU) 
Arusha. Madaktari wa Mifugo wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) kwa kushirikiana na wataalam wa Taasisi ya wanyamapori (TAWIRI) wametumia  saa matatu  kumfanyia upasuaji simba ambaye ni mgonjwa.
Simba huyo, ambaye alikuwa eneo la creta Ngorongoro,  amekuwa akiumwa na muda mwingi kukaa peke yake ambapo taarifa za awali zilieleza huenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ngiri ambao umemsababishia uvimbe.
Upasuaji huo ulianza majira ya saa saba mchana hadi saa 10 ulikuwa ukiendelea kwa ufanisi mkubwa na mara baada ya kukamilika na madaktari kujiridhisha na afya wa simba hiyo, ataachiwa kujiunga na wenzake.
Ofisa Idara ya uhusiano katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Nickson Nyange alikiri leo  kuanza kufanyiwa upasuaji simba huyo na kueleza hadi majira ya saa 10 ulikuwa unaendelea.
"Muda huu madaktari na watafiti wanaendelea na upasuaji kuokoa maisha ya simba huyu, ambaye amekuwa ni mmoja wa vivutio vya utalii katika hifadhi yetu" Amesema
Hata hivyo, amesema  madaktari na maofisa wa Mamlaka ya Ngorongoro na Tawiri  kesho, watatoa taarifa kamili za kitaalamu juu ya ugonjwa uliokuwa unamkabili Simba huyo.
Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk Maurus Msuha  alikuwa kwenye kikao na kueleza angetoa taarifa hiyo mara baada ya kikao hicho kukamilika.

Mbunge atuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wa rafiki yake



Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini 
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini  
Dodoma. Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini ameomba Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga ahusishwe katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa Tundu Lissu.
Selasini ametoa ombi hilo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Novemba 9,2017 jioni akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/19 na mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka 2018/19.
Mbunge huyo wa Rombo akichangia amesema mbunge huyo alishahusishwa na mauaji ya mpenzi wa mpenzi wake, hivyo ni vyema akahusika na uchunguzi huo.
Baada ya mbunge huyo kueleza hayo, Mlinga aliomba kwa Spika ampe taarifa Selasini akisema katika kipindi cha uhai wake hajawahi kuhusishwa na mauaji.
“Ninamheshimu sana mheshimiwa Selasini. Tangu nizaliwe sijawahi kuhusishwa na kifo cha mpenzi wa rafiki yangu namuomba alete ushahidi katika Bunge hili ni nani alinihusisha,” alisema Mlinga.
Mwenyekiti wa Bunge, Nagma Giga alimuuliza Selasini kama anapokea taarifa hiyo lakini mbunge huyo aliendelea kushikilia msimamo wake akisema suala hilo liliandikwa katika gazeti la Dira.
“Nimemsikia na huo ni mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu. Gazeti la Dira liliandika vizuri sana kuwa mpenzi wako alikusaliti. Wewe na kundi la vijana wenzako mkaenda kumuua. Liliripotiwa polisi na limeripotiwa kwenye magazeti na hujawahi kukanusha hadi leo,” alisema.
Selasini alisema, “Ningeiomba Serikali katika uchunguzi wa nani waliohusika kutaka kudhulumu maisha ya Tundu Lissu, huyu ambaye ameshatajwa kwamba alihusishwa na mauaji uchunguzi uanzie kwake,” alisema.
Mbunge huyo wa Rombo alisema asubuhi wakati Mlinga alipoomba mwongozo wa Spika, mwongozo wake ulijaa kejeli na kumhusisha Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na mauaji ya albino.
Katika mwongozo huo, Mlinga alihoji hatua ya Mbowe kutaka wachunguzi wa kimataifa kuchunguza tukio la Lissu aliyejeruhiwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na kuhoji ni kwa nini hakuwahi kutaka wachunguzi hao katika mauaji ya albino.
Mlinga alisema kwa kuwa kuna taarifa kuwa wapo wanasiasa wanahusika na mauaji ya albino basi Mbowe naye ni mhusika na pia akasema ni kwa nini hakuhoji mauaji ya watu wa Kibiti na Rufiji.
Hata hivyo, Spika Job Ndugai alisema kwake haoni kama kuna mwongozo na kuelekeza shughuli za Bunge ziendelee kwa wachangiaji kuanza kuchangia mpango huo.
Asubuhi katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Mbowe alimuomba waziri mkuu akubali wachunguzi wa kimataifa waje nchini kuchunguza tukio la kushambuliwa Lissu ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema bado vyombo vya kiuchunguzi nchini havijashindwa kuchunguza tukio hilo na akawahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi unaendelea.

Polisi watakiwa kupambana na ugaidi


Dar es Salaam. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka polisi wanawake kupambana na vitendo vya kiuhalifu ikiwemo uchochezi, wizi wa mitandao, ujangili ugaidi na utakatishaji wa fedha haramu.
Hayo ameyasema leo Novemba 9  akifunga maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao wa polisi wanawake yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha taaluma ya Polisi Kurasini.
Makamu wa Rais amesema suala la  kuwepo kwa ulinzi  ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.
Amesema  kwamba  kuwepo kwa polisi wanawake kumeleta mtazamo tofauti katika jamii, watu wamekuwa wakiona polisi ni rafiki wa umma.
Amewataka polisi kufuata sheria katika matukio yote ya unyanyasaji wa kijinsia badala ya kuwaacha kwenda kuyatatua kifamilia.
" Unakuta mtu kanyanyaswa kijinsia anapofika kituoni polisi wanasema hiyo ni aibu mkayamalize kifamilia amesema  Samia "
Katika vita ya unyanyasaji wa kijinsia amewataka polisi kushirikiana kutoa elimu bila kujali jinsia kwani vita hiyo sio ya wanawake tu.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamadi Masauni aliwapongeza polisi kwa mshikamano pamoja na ujasiri waliouonyesha.
Masauni amewahakikishia polisi kuwa kila kitakachopatikana Serikalini atahakikisha kinagawanywa kwa usawa ili kuhakikisha polisi wanafanya kazi kwa ufanisi.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi mstaafu na mlezi wa mtandao huo  Saidi Mwema alisema alipokuwa mkuu wa jeshi hilo alipanga kubadilisha muundo wa jeshi hilo.
Alisema "nilipofanya ziara Afrika ya kusini na kuona muundo wao nilivutiwa nao sana na niliporudi  nchini  nilianzisha mfumo huo"
Naye mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Alvaro amesema katika jeshi la Umoja wa Mataifa wapo pia polisi wanawake na wengine kutoka Tanzania.
Hivyo nawapongeza kwa ujasiri na umoja wenu kwa kudhubutu ili kufikia malengo ya usawa wa kijinsia.
Katika maadhimisho yalipambwa na vikosi mbalimbali vikiongozwa na polisi wanawake ikiwemo gwaride, kuendesha pikipiki na farasi, kikosi vya makomandoo pamoja na vyakutuliza ghasia.

SERIKALI YAZINDUA NDEGE MAALUMU ITAKAYOFANYA DORIA KATIKA ENEO LA BAHARI KUU KUDHIBITI UVUVI HARAMU

Serikali imezindua mkakati unaolenga kutokomeza uvuvi haramu kwa kuanzisha operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua safari ya ndege ya kutoka nchini Mauritius iliyotua hapa nchini, kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufanya doria ya majini, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imejipambanua juu ya ulinzi wa rasilimali za nchi, ikiwamo meli ya uhakika ya majini, licha ya kukumbwa na dhoruba kubwa.

Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana wameunganisha nguvu kwa pamoja kati yao na Ukanda wa nchi za Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.

“Tunaruhusu ndege ya doria leo, ili kuongezea nguvu njia za kudhibiti wavuvi haramu, tulianza kwa njia ya bahari na sasa ni kwa njia ya anga.

“Changamoto ya uvuvi haramu ni kubwa, mtu anapiga bomu kwenye matumbawe anafanya uharibifu ambao kuyatengeneza tena yanachukua zaidi ya miaka 100, huku yeye akiharibu kwa dakika tano, ” alisema Ulega.

Ulega alisema uharibifu huo ndiyo unachangia kuwatia umasikini wavuvi wengi kwa sababu siyo rahisi kupata samaki karibuni na kulazimika kwenda mbali ambako siyo rahisi kufika bila kuwa na vyombo maalumu.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hamad Rashid alisema atashauriana na marais wa pande zote mbili kuangalia namna ya kurudisha Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico) na Shirika la Uvuvi Zanzibar (Zafico).

Alisema mashirika hayo yakifanya kazi kwa kushirikiana wananchi watapata fursa ya kufurahia matunda yatokanayo na utajiri uliomo baharini.

“Katika mwendelezo wa kupambana na uvuvi haramu na kulinda bahari ya Hindi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilifanya mazungumzo ya kuingia ubia na Serikali ya China na tayari kuna meli 10 zinafanya doria.

“Serikali pia imeagiza boti 500 watakazopewa wavuvi ili wazitumie kuvua kisasa, pia inasimamia ujenzi wa soko la samaki la kisasa na namna bora ya kuhifadhi samaki awe katika hali yake ile ile hadi anamfikia mlaji, ” alisema Rashid.

Alisema uvuvi haramu siyo tu janga kwa kuondoa rasilimali za bahari, pia ukiachwa uendelee unaweza kuwa chanzo cha biashara nyingine haramu ikiwamo usafirishaji wa watu, biashara ya dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Nae Katibu mkuu Uvuvi Dk Yohana Budeba alisema ndege hiyo itafanya doria ya anga kwa siku nne.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu Hosea Mbilinyi alisema ndege hiyo licha ya kuzunguka angani ikifanya doria, ina uwezo wa kupiga picha na kueleza kinachoendelea.

Alisema doria hiyo ni ya kikanda ambayo inahusisha nchi nane zikiwamo Tanzania Kenya, Msumbiji, Ushelisheli, Reunion, Comoro, Mauritius na Madagascar.

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu, leo jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu mara baada ya kuikagua ndani.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega pamoja na viongozi mbalimbali wakiangalia ndege maalumu ya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed naNaibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa zawadi kwa marubani wa ndege hiyo. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu yajamii. 

JAMII YATAKIWA KUACHA ITIKADI ZA VYAMA KATIKA KULETA MAENDELEO


MBUNGE Wa viti maalum Mkoa Wa Iringa, Ritta Kabati ametoa wito kwa jamii kuondoka na itikadi za kisiasa pindi linapokuja suala la maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza na wazazi na walezi wa shule ya msingi Igeleke wakati wa ukarabati wa madarasa ya shule hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni ahadi yake ya kukarabati shule za msingi zenye miundo mbinu mibovu na zamani, Kabati alisema kuwa suala la ujenzi wa madarasa hauna siasa.

Alisema kuwa maamuzi ya kukarabati shule za msingi lengo ni kuyaweka mazingira bora ya kusomea wanafunzi na kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uchakavu wa majengo.Kabati alisema kuwa imekuwa kawaida pindi mtu akitaka kufanya maendeleo mambo ya siasa yanaingizwa ila kwa serikali hii ya hapa kazi lazima tufanye kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa maamuzi kufanya shughuli za kijamii hasa katika elimu ni kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyo bora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo kama ilivyo kanda za Kaskazini ambapo elimu ni kipaumbele cha kwanza.

“Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi na kuondoa kasumba ya watu wengi wafanyakazi wa ndani ni kutoka mkoani hapa”alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule.Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi walio tayari kuleta maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo”
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akikabidhi saruji kwa uongozi wa shule kabla ya kuanza ukarabati katika shule ya msingi Igeleke.

CHAMA CHA LABOUR CHA UINGEREZA CHAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTENDAJI WAKE.

Chama cha Labour cha nchini Uingereza kimepongeza juhudi za Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa utendaji mzuri katika kulinda na kugawanya rasilimali kwa watu wake.

Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na Viongozi wa Labour Party katika Mkutano na vyama mbali mbali vya kisiasa vikiwemo vya Kiafrika vya SWAPO, ANC na CCM, uliofanyika Uingereza kama anavyoeleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa, Kanali (Mstaafu) Ngemela Lubinga katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

“Chama cha Labour kinataka haki sawa kwa wote, kwa hiyo kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia rasilimali na kuhakikisha rasilimali zetu zinazoibiwa zisiibiwe tena, kimewapa faraja,” alisema Lubinga.
Lubinga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inasimamia rasilimali kitendp ambacho kitaleta maandeleo kwani hakuna maendelo yanyowezakupatikana bila usimamizi wa rasilimali.

“Chama cha Labour kinapigana kuhakikisha wananchi wake wanapata makazi bora, hivyo suala la Accacia ambao walikuwa wakifanya vitendo visivyoendana na hali halisi ya rasilimali hasa kwetu sisi walengwa kimewafurahisha sana na kuona kuwa mazungumzo yamekamilika katika mazingira ya kukubaliana namna ya rasilimali hizo zinavyotumika kuwanufaisha watanzania,”alisema Lubinga.

Kuhusu mwelekeo wa uchumi, Kanali (Mstaafu) Lubinga amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua na utakuwa wa kuvutia kwani juhudi za makusudi zinafanyika hivyo amewataka wanachi wawe na subira.

Ameongeza kuwa wazazi wawaandae watoto wao kufanyakazi na wasiwaachie tu kwenda wanavyotaka. Ametoa mfano kuwa mtu akiona mtoto wake amenunua gari la kifahari inabidi amuulize fedha ametoa wapi za kununua gari hilo wakati mshahara wake unajulikana na ni mdogo.Amewataka watanzania wawe wavumilivu kwani mabadiliko huleta kiwewe kwa wat na yakishaleta matokeo chanya, watu hao husahau walioleta maendeleo hayo.

Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza miaka miwili tangu iingie madarakani tarehe 5 Novemba, 2015. Katika kipindi hiki watanzania wameshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikianzishwa na kutekelezwa, mfano ujenzi wa barabara,madaraja, ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa reli ya kisasa, (standard gauge), utengenezaji wa madawati na elimu bure kwa elimu ya msingi na mwisho nidhamu ya kazi imerejea katika utumishi wa umma.

Magufuli na Museveni waweka jiwe la msingi la bomba la mafuta Uganda

Rais Museveni wa Uganda na Rais Magufuli walisaini mkataba wakuanza mradi wa bomba la mafuta ghafi mwezi Mei
Image captionRais Museveni wa Uganda na Rais Magufuli walisaini mkataba wakuanza mradi wa bomba la mafuta ghafi mwezi Mei 2017
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Rais hao wawili wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wakiwa katika kijiji cha Luzinga, jirani na mpaka wa Mutukula.
Pia wamefungua kituo cha forodha chenye huduma zote muhimu kurahisisha safari kati ya nchi hizo mbili.
Rais Magufuli anafanya ziara Uganda kwa siku tatu.
Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima -Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu dola za marekani bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000. Bomba linatarajia kukamilika mwaka 2020.
Mradi huo utakao gharimu dola za kimarekani bilioni 3 unajengwa kwa ushirikaino wa serikali za nchi hizo mbili na washirika na unatariji kutoa ajira zaidi ya 30,000.

Nyaraka za Paradiso: Maswali kuhusu uchimbaji madini Afrika

Katanga mineHaki miliki ya pichaPREMIERES LIGNES
Image captionTimbo la Katanga nchini DR Congo
Moja ya makampuni makubwa zaidi duniani ilimpa mkopo wa dola milioni 45 mfanyabiashara ambaye awali alikuwa ametajwa kwenye ufisadi, na kumuomba atafute leseni za kuchimba madini katika taifa moja maskini eneo la Afrika ya kati, uvujaji unaojulikana kama "Nyaraka za Paradiso" umefichua.
Kampuni ya Glencore ya Uswisi ilitoa mkopo huo kwa bilionea raia wa Israel Dan Gertler, dalali maarufu ambaye alikuwa na uhusiano na watu wa vyeo vya juu katika serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo mwaka 2009.
Bw. Gertler aliombwa kutafuta makubaliano mapya kwa kampuni moja ya uchimbanji madini ambayo Glencore ilikuwa na hisa nyingi.
Yeye na Glencore wanakana kufanya lolote baya.
Glencore walikubali kumlipa Dan Gertler dola milioni 534 ili kununua hisa zake zote nchini DR Congo mwezi Februari mwaka huu.
Ufichuzi huo mpya ulitolewa kwenye Paradise Papera, ambao ni uvujaji wa zaidi ya nyaraka milioni 13.4.
Glencore, mfanyabiashara wa Israel na migodi DR CONGO
Image captionGlencore, mfanyabiashara wa Israel na migodi DR CONGO
Taifa la Jamhuri ya Demoksrasi ya Congo imekumbwa na ghasia na ufisadi kwa miongo kadhaa hali ambayo imesababisha karibu nusu ya watu wake kabaki hali mbaya ya umaskini.
Lakini madini mengi ya nchi hiyo ni ya thamani ya milioni ya dola kila mwaka kwa wale wanaoweza kuyafikia.
Moja ya kampuni hizo ni Glencore, kampuni moja kubwa na madini ya Uswisi.
Kwa vipimo inachukua nafasi ya 16 kati ya kampuni kubwa zidi duniani.
Kwa miaka mingi Glencore imehusika na uchimbaji wa madini nchini DR Congo hasa kwa uzalishaji wa shaba nyekundu.
Kampuni hiyo inasema kuwa imewekeza dola bilioni dola 50 nchini DRC.
Miaka kumi iliyopita ilikuwa na asilimia 8.52 ya hisa katika kampuni inayojulikana kama Katanga ambayo ilikuwa na kibali cha kuchimba shaba nyekundi kusini mwa nchi.
Mwezi Juni mwaka 2008 bodi ya kampuni ya Katanga ambayo ilikuwa na afisa wa wa cheo cha juu ilikumbwa na habari ambazo hazikuwa nzuri
Glencore ni nani
Image captionGlencore ni nani
Serikali ya DRC chini ya Rais Joseph Kabila ilitaka kujadili upya leseni za uchimbaji madini.
Makubaliano yake ya kwanza yalikuwa ni dola milioni 135.
Nyaraka zilizo kwenye Paradise Papers zinaonyesha jinsi bodi ya Katanga ilihisi kuwa matakwa ya mamlaka za DRC hayangekubalika.
Kwa mara ya kwanza ni rahisi kujua jinsi wakurugenzi waliamua kuomba msaada wa mfanyabiashara raia wa Israeli Dan Gerter.
Glencore ilikuwa tayari imewekeza dola milioni 150 katika kampuni ya Katanga na pesa hizo zingepotea ikiwa haingechimba madini.
Kampuni iliyomilikiwa na serikali ya Gécamines, ilikuwa inataka dola milioni 585, ili Glencore iruhusiwe kuchimba madini ya shaba nyekundu
Wakati kama huo Glencore ilikubali kuipa mkopo kampuni iliyokuwa kwenye visiwa vya British Virgin Islands kwa jina Lora Enterprise dola milioni 45.
Lora Enterprises ilikuwa ikidhibitiwa na familia ya Gertler.
Makubalino ya mkopo huo yalikuwa ni ikiwa Bw. angeshindwa kufanikiwa kupata leseni mpya ndani ya miezi mitatu, Glencore ilikuwa na haki ya kurejesha mkopo huo.
Paradise Papers zinasema kuwa Bw Gertler alifanikiwa kwa haraka, Gecaminis ikaunguza pesa ilizokuwa ikiomba hadi dola milioni 140 na kuikolea katanga dola milioni 445.

Mahakama ya ICC kuchunguza uhalifu uliotokea Burundi

Mahakama ya ICC kuchunguza uhalifu uliotokea BurundiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMahakama ya ICC kuchunguza uhalifu uliotokea Burundi
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC huko The Hague, imewaamrisha waendesha mashtaka kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu madai ya uhalifu dhidi ya binadamu ulitokea nchini Burundi.
Majaji walisema kuwa kuna sababu za kuchunguza uhalifu huo ukiwemo mauaji na mateso uliofanywa na serikali na makunde yenye uhusiano na serikali.
Burundi ilijiondoa kutoka ICC mwezi uliopita lakini mahakama ya ICC inasema kuwa inaweza kuchunguza uhalifu ulitokea hadi wakati huo.
Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa mamia ya watu waliuawa wakati wa ghasia zilizoibuka baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu mwaka 2015.

Binti shujaa mbunifu wa Emoji iliyo na Hijab

Emoji ya Hijabu iliyobuniwa na binti wa miaka 15 wa Saudi Arabia
Image captionEmoji ya Hijabu iliyobuniwa na binti wa miaka 15 wa Saudi Arabia
Binti mmoja ambaye ni mwanamitindo wa kibinafsi ambaye ametajwa kama "mwanaharakati wa emoji" Rayouf Alhumedhi ameandikisha historia ya digitalI, kwa kuundwa kwa mchoro uitwao emoji ili kuwakilisha wanawake wanaovalia vazi la heshima kwa wanawake waislamu la hijab.
Rayouf anasema kuwa alichoshwa kwa kushindwa kujitambua katika majukwaa ya kimataifa katika picha na alama zake za vidole: ''Kujihisi kutengwa, sio uhalisia wa kweli.....ni kama jambo ambalo ningependa liwepo au ninaloweza lifanyike'.
Hadi pale kampuni ya Apple, ilipotoa emoji hiyo, sikujua ninavyohisi,....
Mimi nina kwenda kuwa mwenye furaha kubwa. Naweza hata kufa kwa furaha niliyo nayo....!"
Aliambia idhaa ya BBC ya The Cultural Frontline, kuhusu namna, kupitia kazi ya uchoraji wa grafiki na ubunifu wa kisasa, kupitia mtindo wa Aphee Messer, emoji hiyo ya hijabi ikazaliwa.
Msichana huyo raia wa Saudia anayeishi Ujerumani, amebuni emoji hiyo ya ijab kwa wanawake waislamu.
Rayouf Alhumedhi, ana umri wa miaka 15, na ametuma pendekezo hilo lake hadi kwa The Unicode Consortium, shirika moja la kibinafsi lisilohitaji faida yoyoye, ili emoji hiyo mpya ipigwe msasa, liundwe na kunakifishwa kabla ya kuanza kutumika.
Ikiwa itaidhinishwa, bila shaka itaanza kutumika mwaka huu wa 2017.
Kuna tofauti gani kati ya hijab, niqab and burka?
Mataifa kadhaa ya Bara Ulaya yanaendelea na mjadala wa mavazi ya kiislamu yanayofunika uso
Image captionMataifa kadhaa ya Bara Ulaya yanaendelea na mjadala wa mavazi ya kiislamu yanayofunika uso
Mapendekezo hayo yanatukia wakati ambapo mataifa kadhaa ya Bara Ulaya yanapoendelea kujadili swala la mavazi ya kiislamu yanayofunika uso, kutumika kwa namna yoyote ile.
Mjadala huo unafanyika, chini ya Uhuru wa ibada, usawa wa kijinsia mingoni mwa wanawake, utamaduni wa kisasa na hofu ya kuongezeka kwa ugaidi duniani hasa wahanga wa kujitoa kufa.