Simba huyo, ambaye alikuwa eneo la creta Ngorongoro, amekuwa akiumwa na muda mwingi kukaa peke yake ambapo taarifa za awali zilieleza huenda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ngiri ambao umemsababishia uvimbe.
Upasuaji huo ulianza majira ya saa saba mchana hadi saa 10 ulikuwa ukiendelea kwa ufanisi mkubwa na mara baada ya kukamilika na madaktari kujiridhisha na afya wa simba hiyo, ataachiwa kujiunga na wenzake.
Ofisa Idara ya uhusiano katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Nickson Nyange alikiri leo kuanza kufanyiwa upasuaji simba huyo na kueleza hadi majira ya saa 10 ulikuwa unaendelea.
"Muda huu madaktari na watafiti wanaendelea na upasuaji kuokoa maisha ya simba huyu, ambaye amekuwa ni mmoja wa vivutio vya utalii katika hifadhi yetu" Amesema
Hata hivyo, amesema madaktari na maofisa wa Mamlaka ya Ngorongoro na Tawiri kesho, watatoa taarifa kamili za kitaalamu juu ya ugonjwa uliokuwa unamkabili Simba huyo.
Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk Maurus Msuha alikuwa kwenye kikao na kueleza angetoa taarifa hiyo mara baada ya kikao hicho kukamilika.
No comments:
Post a Comment