Thursday, July 20

Taarifa

Kwa mujibu wa Chadema media
Mbunge wa Ubungo Mh. Saed Kubenea anahitajika kuripoti Polisi siku ya leo tarehe 20. 07. 2017 kutoa maelezo kwa malalamiko yaliyofunguliwa na Prof. Ibrahim Lipumba
Kuitwa kwake kumekuja baada ya wiki iliyopita kufanya mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ya Mkiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na viongozi wa CUF inayoongozwa na Mkiti wa Kamati ya Uongozi Julius Mtatiro na Katibu Mkuu Maalim Seif na kutangaza operesheni inayoitwa Operesheni Ondoa Msaliti Buguruni (OMB).
Operesheni hiyo itaendeshwa kwa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA

MAPACHA WALIOUNGANA MARIA NA CONSOLATA MWAKIKUTI WAPONGEZWA KWA KUFAULU MTIHANI WA KIDATO CHA SITA


Na Francis Godwin, Iringa
SERIKALI ya wilaya ya Kilolo na mbunge wa kilolo Mhe. Venance Mwamoto wamewapongeza kwa zawadi za maandalizi ya chuo kikuu mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (19) waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu. 
Wakikabidhi zawadi hizo kwa mapacha hao jana mbele ya walezi wao wa kituo cha Nyota ya asubuhi ambako wanaishi Maria na Consolata, Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, Mhe.Mwamoto ambao waliongozana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilolo Bw. Alloyce Kwezi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto walisema wamevutiwa na ufaulu wa mapata ambao ni yatima hivyo wamelazimika kuwaanzishia maandalizi ya chuo mapema zaidi kwa lengo la kuwawezesha kuanza chuo kwa wakati.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Kwezi alisema kwa kufanya kwao vizuri kumeongeza heshima kubwa kwa wilaya ya Kilolo ambayo ndio iliyoongoza kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mkoa wa Iringa wenye shule 25 huku wilaya hiyo ikiongoza kimkoa kwa kuwa na shule Pomerini ndio iliibuka ya kwanza kwa shule zote 25. 
Hivyo alisema moja kati ya mkakati wa Halmashauri ya Kilolo ni kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mitihani mbali mbali pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo ili kuifanya wilaya hiyo kuwa mbele kwa kila jambo . 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema kuwa pamoja na wilaya kutoa msaada huo kwa watoto hao mapacha kama sehemu yao ya maandalizi ya chuo bado milango ipo wazi kwa wadau wengine walioguswa na watoto hao kuzidi kuwasaidia kwani wao wenyewe wameonyesha nia ya kuendelea na masomo na kuwa mfano kwa baadhi ya jamii ambayo imekuwa ikiwaficha watoto wenye ulemavu kwenda shule .
 “ Wametuowezesha wilaya yetu kufanya vizuri kweli! Tunawapongeza wao ,walimu na wadau wote wa elimu zaidi wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika mitihani hiyo.
"Kilolo ilikuwa ikitazamwa sana kuona nini matokeo ya  Maria na Consolata ila bila viongozi na wadau wengine wa elimu kujitoa kwa ajili yao yawezekana wasingefanya vizuri …..tupo pamoja nao na tutaendelea kuwa pamoja zaidi hadi chuo “ Mkuu huyo wa wilaya alisema.
Aliongezea kuwa moja kati ya mahitaji yao makubwa kwa sasa ni nyumba yao maalum kwa ajili ya kuishi pindi watakapokuwa chuo kwani wao wanahitaji nyumba maalum ambayo ni rafiki zaidi na aina ya ulemavu waliokuwa nao . 
Mbunge wa Kilolo Mwamoto mbali ya kuwapongeza mapacha hao bado alitaka wananchi wote wenye watoto wenye ulemavu kuiga mfano wa mapacha hao na hatapendezwa kuona watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ile wanafichwa majumbani . 
Pia alisema moja kati ya mkakati wake kuona mazingira ya shule mbali mbali katika wilaya ya Kilolo yanakuwa rafiki na kuwataka wananchi kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ,maabara ili kuepukana na changamoto ya miundo mbinu ya elimu pamoja na kwenda sawa na serikali ya Rais Dkt John Magufuli ya uboreshaji wa elimu .
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto wakiongea na watoto hao
mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapa zawadi ya laptop  mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mito
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mablanketi

TANZIA: MAMA WA MZAZI MWENZA WA MWANAMUZIKI DIAMOND PLATNUMZ AFARIKI DUNIA LEO


Mama mzazi wa Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz, Halima Hassan (kulia) amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akidaiwa kusumbuliwa na maradhi ya moyo na figo.

Zari amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..
AMEN.

VODACOM YAOGEZA MUDA WA TOLEO LA HISA ZAKE



MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AHIZIMIZA USHIRIKIANO KUKABILI UKATILI DHIDI YA ALIBINO


Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. George  Masaju ametoa wito  kwa Asasi zisizo za kiserikali ( NGO)    kushirikiana na kufanya kazi kwa  karibu na Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali    ili  kupitia ushirikiano huo kukomesha   na hatimaye kumaliza kabisa  changamoto zinazowakabili  watanzania wenye albinism.
Mwanasheria Mkuu ametoa  wito huo  leo  ( Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi  Ikponwosa Ero,  Mtaalamu Huru wa Baraza la  Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa kuhusu  watu wenye albinism
“  Ningependa  kutoa shukrani zako kwa kuamua kuja Tanzania  na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali,  hii ni fursa  muhimu kwako    ya kupata taarifa sahihi na rasmi kuhusu  jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili  vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu wenye  albinism” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu
Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe basi  uwahimize   viongozi wa asasi zisizo za kiserikali hususani zile zinazojihusisha na  watanzania wenye  albinism kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na  Ofisi yangu  na Taasisi nyingine za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la  kuwasaidia  watanzania wenzetu”..
Akasema  Serikali  inachukulia kwa uzito wa hali ya juu  makosa  ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na  sheria kuchukua mkondo wake.
Akasisitiza kwamba  Katiba ya  Jamhuri ya Muungano  imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua   wakiwamo  watu wenye  albinism au ulemavu wa aina yoyote.
“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki hiyo  haimbagui mtu mwenye albinisim au  mtanzania yoyote ile na ndio maana  makosa ya jinai  dhidi ya  haki ya mtu kuishi  awaye yeyote yule  yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.
Kuhusu takwimu  zinazohusu matukio ya jinadi dhidi ya  watanzania wenye albinism,Mwanasheria Mkuu  wa Serikali  amesema kwamba tangu  mwaka  2006  hadi  mwaka huu kumekuwa na matukizo 66 dhidi ya watu wenye albinisma na   huki  miaka mingine ikiwa na haina tukio  lolote lile na kwamba kutokana na  juhudi zinazofanywa na serikali   matukio hayo yameendelea kupungua kwa kiasi kikubwa sana mwaka  hadi mwaka.
Kuhusu    hukumu dhidi ya  watuhumiwa,  Mwanasheria mkuu amesema utekelezaji wa hukumu dhidi ya  watuhumiwa wa makoja hayo ya jinai umekuwa wa mafanikio makubwa kwa zaidi ya asilimi 90 na kwamba  hukumu   zilizotolewa ni pamoja na vifungo,   huku  ya kifo kwa baadhi ya watuhumiwa. Ingawa pia kuna walioachiwa huru kutoka na  kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza.
Mwanasheria  Mkuu wa Serikali ametaja baadhi ya mafanikio mengine ni pamoja na Ofisi yake  kuandaa na kutekeleza  uratibu wa uhuishaji wa takwimu  za matukio  ya kijinai dhidi ya  watu wenye albinism.  Uratibu  ambao ulifanyika mwaka 2014 kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Sheria na Katiba na  Asasi za Kiraia.
Aidha  ametaja mafanikio mengine  ni  kuanzishwa kwa dawati maalum katika Divisheni ya  Mwendesha Mashtaka  kuhusu watu wenye albinism, kusimamia  upepelezi na kuendesha kesi.
Kwa upande wake Bi. Ikponwosa Ero akielezea madhmuni  ya  ziara yake hiyo hapa nchini  kuwa , pamoja na mambo mengine,  kutathimini hali ya haki za bindamu za watu wenye   albinisma,,  kutathimini hatua na jitihanda zinazofanywa na Serikali  katika kukabiliana na  changamoto zinazowakabili watu wenye albinism,  kubainisa mapungufu  na kuona uwezekano  wa kuziba mapengo ya mapungufu hayo.
Pamoja na kuuliza maswali  mbalimbali kwa Mwanasheria  Mkuu wa Serikali , maswali na hoja  zilizojibiwa na  Mwanasheria  Mwenyewe, pamoja na Mkurugenzi wa Divisheni ya  Katiba na  Haki za Binadamu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Divisheni ya Mashtaka, Mtaalamu huyo amemshukuru Mwanasheria Mkuu   kwa kutenga muda wa kukutana naye na kwa  maelezo na taarifa zikiwamo za kitakwimu ambazo  zimewasilishwa kwake. Pamoja na kutambua juhudi za serikali katika  eneo hilo.
Bi. Ikponosa Ero aliteuliwa na  Baraza la Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa June 15, 2015 kuwa Mtaalamu  Huru wa haki za bindamu kwa watu wenye albinism. 

Imetolewa na Kitengo cha Mwasiliano
Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa  Serikali

NAIBU WAZIRI MANYANYA :AWATA WAZAZI KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO SHULENI.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka kulia akitembelea shule ya Msingi Bagamoyo wakati wa ziara yake wilayani Korogwe kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel na anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akiwasili katika shule ya Msingi Matondoo wakati ewa ziara yake ya kukagua maendeleo ya sekta hiyo wilayani Korogwe
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akisalimiana na walimu wa shule ya msingi Matondoo wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka klushoto akimsikiliza Afisa Tarafa ya Korogwe mjini,Michael John kuhusu ujenzi wa baadhi ya madarasa kwenye shule hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji,Jumanne Shauri anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ziara yake wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akiwa ameshika mtoto wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bagamoyo iliyopo wilayani Korogwe ambapo aliwataka kusoma kwa bidii ili waweze kupata mafanikio

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Matondoo wakati wa ziara hiyo ambapo aliwataka kutilia mkazo masomo ya sayansi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akisalimia na wananchi wa Jimbo lake wakati wa ziara hiyo ya
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe ,Jumanne Shauri akizungumza katika ziara ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanyawa tatu kutoka kulia
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika halfa hiyo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akimuonyesha kitu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati waliojiwekea kuhakikisha wanapiga hatu kubwa kielimu
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya ambaye hayupo pichani

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya katika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kushoto wakati wa ziara yake alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa maktaba ya wilaya hiyo ambao umeshindwa kuendea kwa muda mrefu ambapo aliagiza uendelezwe kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri na
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda,Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia,
Mhandisi Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi matondoo

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154


 Rais Dkt John pombe Magufuli mapema leo amefungua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda
 Rais Dkt John pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya akina Mama waliofika kushuhudia hafla fupi ya ufunguzi wa barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipungia vikundi vya kwaya,ngoma na Burudani alipowasili kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo tayari kwa kuzindua Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Baadhi ya waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,wakimsikiliza kwa makini Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wakati akiwahutubia 19 Julai 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mustafa kijuu akisoma taarifa ya mkoa wake mbela ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akihutubia wananchi wa Biharamulo wakati wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Umati Waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, wakimsikiliza kwa makini Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, wakati akiwahutubia 19 Julai 2017.
Umati Waananchi waliohudhuria uzinduzi wa Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,wakimshangilia,Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa barabara kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa barabara kwenye viwanja vya stendi ya Biharamulo 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiondoa kitambaa kwenye jiwe kuashiria ufunguzi wa ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo, Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Viongozi wengine akiwemo Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wakikata utepe kuashiria ufunguzi Barabara ya Biharamulo,Kagoma, Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,.Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Makame Mbarawa mara baada ya kufungua Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154,Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na akiwa ameambatana na mkewe mama Janeth Magufuli Viongozi wengine akiwemo Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wakisaimiana na wananchi waliohudhuria ufunguzi Barabara ya Biharamulo,Kagoma ,Lusaunga yenye urefu wa kilometa 154, Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Mhandisi wa maji wa wilaya ya Biharamujlo mh Patrice Jarome na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Bukoba Ndugu Allen Marwa wakijibu hoja ya maji mbele ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mara baaada ya kuelezwa kero ya maji katika mji huo na wao kuahidi ndani ya siku kumi kufunga mitambo ya maji na kuwasambazia wananchi maji 19 julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wa wananchi kijiji cha Nyakahura waliokuwa njiani kumpokea akiwa njiani akielekea Ngara Mkoani Kagera, 19 Julai 2017. Picha na Ikulu.