Saturday, September 2

TANZIA: ADVOCATE JUMA REGINALD WILFRED SAWAYA MAWALLA


WAKILI WA KWANZA KUAPISHWA BAADA YA UHURU WA TANGANYIKA
THE FIRST ADVOCATE TO BE INAUGURATED AFTER AFTER TANGANYIKA'S INDEPENDENCE




BWANA AMETOA NA BWANA AMETOA JINA LAKE LIHIMIDIWE
THE LORD HAS GIVEN AND THE LORD HAS TAKEN MAY HIS NAME BE PRAISED

ROHO YAKE ILALE MAHALI PEMA PEPONI. AMINA.
MAY HIS SOUL REST IN  PEACE. AMEN.


KUMBUKUMBU YA MAMA JOYCE MKAMSURI MAREALLE



Mama. unafikisha miaka saba tangu ulipotutoka Septemba 2, 2010.
Mama tunakukumbuka. 
Pumzika kwa amani mama yetu mpenzi. 
 - Emmy marealle

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI JIJINI TANGA LEO


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi (kulia). 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakisikiliza maelezo kuhusu mapango hayo kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora.
Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea mapango ya Aboni Jijini Tanga leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kuingia ndani ya mapango ya Amboni. Mhandisi Makani alisema mipango ya Serikali ni kutambua vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo vya mambo ya kale kama yalivyo mapango ya Amboni kuviboresha na kuvitangza ili vichangie zaidi katika pato ta taifa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipata maelezo ya vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Mapango ya Amboni kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni. Wajumbe hao waliishauri Serikali kuongeza thamani ya mapango hayo kwa kuboresha miundombinu na vivutio vilivyopo pamoja na kuvitangaza ili yachangie zaidi kwenye mapato ya Serikali.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia vivutio mbalimbali vya maumbo asilia ikiwemo ya wanyama na alama za kuabudia vilivyomo ndani ya mapango hayo.
Muoneshaji wa Kujitolea katika Mapango ya Amboni, Othman Mangula (kulia) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii moja umbo la asili lenye taswira ya Chui ndani ya Mapango ya Amboni ambapo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii ndani ya mapango hayo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Dkt. Iddi Mfunda (kulia) na Muwakilishi wa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Canisius Karamaga (wa pili kulia) wakiangalia baadhi ya vivutio katika mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akipenya kwenye njia nyembamba iliyopo ndani ya mapango ya Amboni.
Moja ya umbile la asili lililojitengeneza ndani ya mapango ya Amboni likiwa na taswira ya kwato za ngo'mbe.
Maumbo mbalimbali ya asili yenye taswira ya viumbe ni moja ya kivutio kikubwa ndani ya mapango ya Amboni, Pichani ni umbo la asili lenye taswira ya matiti ambalo lipo ndani ya mapango hayo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akimsaidia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungu Ardhi, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya kushuka katika moja ya mteremko uliopo ndani ya mapango hayo.
Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Canisius Karamaga akifurahia jambo ndani maporomoko hayo.
Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango Mtahiko ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Alan Kijazi akiwa ndani ya mapango hayo.
Picha na; Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii

White House yaomba msaada Congress kukabili kimbunga Harvey

Baadhi ya njia muhimu hazipitiki kutokana na kufurika maji
Image captionBaadhi ya njia muhimu hazipitiki kutokana na kufurika maji
Ikulu ya Marekani White House imesema italiomba bunge la Congress msaada wa dharura kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na kimbunga Hurricane Harvey.
Rais Donald Trump anatarajia kuomba kiasi cha dola bilioni 5.9.
Itachukua miezi kadhaa kwa nyumba hizi kurejea katika hali ya awali
Image captionItachukua miezi kadhaa kwa nyumba hizi kurejea katika hali ya awali
Mamlaka mjini Texas imesema kuna uhitaji wa zaidi ya dola bilioni 125.
Zaidi ya watu 39 wamefariki kutokana na kimbunga hicho,huku kikiacha madhara lukuki.
Baadhi ya nyumba hazifikiki baada ya kuzingirwa na maji
Image captionBaadhi ya nyumba hazifikiki baada ya kuzingirwa na maji
Katika ziara yake mjini Texas, makamu Rais Mike Pence ameahidi kujenga upya na kwa ubora zaidi sehemu zilizoharibika.
Mwandishi wa BBC mjini Texas Barbara Plett Usher amesema bunge la Congress linatarajiwa kuidhinisha mapema ombi hilo litakapokutana katika kikao chake wiki ijayo.

Mchango wa Trump

Rais Trump ameahidi kuchangia dola milioni 1
Image captionRais Trump ameahidi kuchangia dola milioni 1
Mike Pence amesema watu 311,000 wamejisajili kwa ajili ya kupata msaada baada ya kimbunga Hurricane Harvey.
Bado haijawekwa wazi ni kwa namna gani misaada hiyo inawez kuwafikia waathiriwa haraka iwezekanavyo.
Alipotembelea miongoni mwa miji iliyoathirika Rockport, Pence ametoa salam za pole kwa watu wote wa Texas.
White House pia imesema Rais Trump atachangia dola milioni moja kutoka kwenye fedha zake mwenyewe.
Vikosi vya waokoaji vimekuwa vikizunguka nyumba kwa nyumba kutafuta manusura na miili ya watu waliofariki ambapo itachukua takriban wiki mbili kwa zoezi hilo kukamilika.
Vikosi hivyo vya uokoaji vinaelekea upande wa Mashariki ambapo bado kimbunga Hurricane Harvey kinaendelea kupiga.
Mike Pence akisaidia kusafisha sehemu zilizoathirika Texas
Image captionMike Pence akisaidia kusafisha sehemu zilizoathirika Texas
Mamia kwa maelfu ya watu waliookolewa awali na ambao walihama mapema wametakiwa kutorudi katika makazi yao mpaka pale taarifa ya kuwaruhusu itakapotolewa tena.
Msaidizi wa ikulu ya White House amesema takriban nyumba 100,000 zimeathirika vibaya na kimbunga hicho.
Taarifa kutoka kamati ya dharura imesema imefanikiwa kuokoa watu 3,800 na zaidi ya 90,000 wamepata misaada ya haraka.

Usambazaji wa Nishati

Sehemu kubwa ya mitambo ya mafuta imeathirika vibaya
Image captionSehemu kubwa ya mitambo ya mafuta imeathirika vibaya
Wasambazaji wa nishati Kusini mwa Texas walilazimika kuzima mitambo yote ya umeme, gesi na hata mafuta ili kuondoa hatari zaidi majumbani na hata viwandani.
Inaweza kuchukua majuma kadhaa kwa huduma hizi kurejea kama awali.
Baadhi ya wakaazi waliorejea majumbani mwao bado wanakumbana na changamoto kadhaa.
Wakala wa kuhifadhi mazingira imewaonya wakaazi wa maeneo hayo kuhusu maji ambayo yametuama kwa kuweza kusababisha baadhi ya magonjwa kwa kuhofiwa kuwa na bakteria.
Mpaka sasa tatizo kubwa kiafya ni upatikajani wa maji safi na salama ya kunywa.
Maelfu ya majumba yanasalia bila ya huduma muhimu ya umeme.
Watu wakichagua nguo za misaada mjini Louisiana
Image captionWatu wakichagua nguo za misaada mjini Louisiana
Kimbunga Harvey kinatajwa bado kuwa na nguvu na kinatarajiwa kupiga Ohio siku ya Jumamosi jioni.
Mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha sehemu za Tennessee na Kentucky kwa siku mbili zijazo, huku mafuriko yakiendelea katika maeneo ya Arkansas, Mississippi, Tennessee, Kentucky, Texas, na Louisiana.

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) LAADHIMISHA MIAKA 53 TOKA KUANZISHWA KWAKE


 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia  maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia  maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya (kushoto}   pamoja na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kulia) mara baada ya kuzungumza kuhusu kuhusu miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya  Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi  wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wanne kutoka kushoto Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wanne kutoka kulia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa watatu kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wakuu wa Kamandi na machifu wa Makao makuu ya Jeshi hilo. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Mwanawe Rais Jacob Zuma, Duduzane amekanusha madai ya ufisadi

Duduzane Zuma ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais Jacob Zuma wa Afrika KusiniHaki miliki ya pichaAFP
Image captionDuduzane Zuma ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Mwanawe Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amekanusha madai kuwa amehusika katika kashfa ya ufisadi.
na kuwa na uhusiano na mfanyibiashara mmoja mwenye utata.
Duduzane Zuma ameiambia BBC kuwa, hakuna "ambacho hakijasemwa" kuhusiana na mshirika wake wa kibiashara na familia ya Gupta.
Barua pepe ambayo inahusiana na familia ya Bwana Zuma na ile ya magupta na kuanzisha uchunguzi ambayo itaonyesha uwezekano wa kuingiliwa kisiasa.
Rais Zuma na familia ya Magupta, mara kwa mara yamekanusha kuhusika na jambo lolote baya.
Katika mahojiano ya kipekee yaliyofanywa na mwaandishi wa BBC Milton Nkosi, Duduzane Zuma amesema kuwa, uhusiano wake na familia tajiri ya Magupta, hauna mambo mengine zaidi kwani yeye ni "mtu mzuri anayependwa na wengi".
"Siamini kuna kitu wanachohitaji kutoka kwangu," alisema huku akiongeza kuwa: "Wananipenda. Na mimi pia nawapenda."
Duduzane Zuma, ambaye ni mmojawepo wa watoto 21 wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, anasisiiza kuwa "si mfisadi".
"Binafsi sijawahi husika na biashara yoyote ya ufisadi," amesema.

Vikwazo vya Marekani vyaathiri utalii wa Korea Kaskazini

Sekta ya utalii inakua kwa kasi Korea Kaskazini
Image captionSekta ya utalii inakua kwa kasi Korea Kaskazini
Zuio la Marekani juu ya raia wake kuingia nchini Korea Kaskazini limeongeza madhara,wakati huu ambapo kumeibuka hali ya kusuguana baina ya mataifa hayo mawili.
Zuio hilo lilitolewa baada ya mwanafunzi kutoka Marekani Otto Warmbier kufariki punde tu alipoachiliwa kutoka gerezani Korea Kaskazini.
Marekani imesema ni muhimu kufanya hivyo kwa lengo la kuwaweka salama wananchi wake.
Kwa raia yeyote wa Marekani atakayekiuka sheria hiyo, atakumbana na adhabu ikiwemo kunyanganywa hati ya kusafiria.
Marekani imesema itaruhusu tu wananchi wake kusafiri kwenda Korea Kaskazini kwa sababu muhimu ikiwemo uandishi wa habari ama utoaji wa misaada ya kibinaadam.
Waandaaji wa ziara za kitalii wanasema kuwa takribani wamarekani 1,000 hutembelea Korea Kaskazini kila mwaka.
Wageni wengine ambao huingia Korea Kaskazini kwa wingi kama watalii ni raia wa China.
Siku ya Alhamis, waendeshaji wa biashara ya utalii waliwaondoa raia wa Marekani wa mwisho waliokuwa Pyongyang.
Takriban watalii 5,000 kutoka nchi za Magharibi kuitembelea Korea Kaskazini kila mwaka
Image captionTakriban watalii 5,000 kutoka nchi za Magharibi kuitembelea Korea Kaskazini kila mwaka
Simon Cockerell, mkuu wa shirika la kitalii la Koryo Tours, ameiambia BBC kwamba anatarajia kupungua zaidi kwa watalii katika ukanda huo kupita awali.
''Licha ya kwamba katazo hili litawaathiri raia wa Marekani, lakini linatuma ujumbe fulani ambao unaashiria kuwazuia watu wa nchi nyingine kutotembelea Korea Kaskazini'' alisema.
Otto Warmbier alikamatwa na kufungwa gerezani mwaka 2016 kwa kudaiwa kufanya njama za kufanya upelelezi akiwa kwenye hoteli moja wakati akiwa likizo.
Aliachiliwa na kupelekwa kwa familia yake mwezi June lakini alikua dhaifu sana na kufariki baadae, huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijulikani.
Marekani inasema kwamba takriban raia 16 wa nchi yake wameshikiliwa Korea Kaskazini kwa muongo mmoja sasa, huku watatu kati yao wakiwa bado kizuizini.
Otto Warmbier alizungumza na waandishi wa habari 2016 na kukana kuhusika na tuhuma za kipelelezi
Image captionOtto Warmbier alizungumza na waandishi wa habari 2016 na kukana kuhusika na tuhuma za kipelelezi
Wengi wao ni wamisionari,waandishi wa habari na Maprofesa.
Marekani imeilaumu Korea Kaskazini kwa kuwashikilia raia wake mara kwa mara na kuwatumia kama chambo ya kusuluhisha migogoro ya kumiliki silaha za nyuklia.
Wiki hii Korea Kaskazini ilitishia tena kurusha makombora yake ya nyuklia kwenye kisiwa cha Marekani cha Guam, huku ikianza kwa jaribio la kurusha kombora kwenye bahari ya Pacific kwa upande unaopakana na Japan.

Uchaguzi Kenya 2017: Mahakama yafutilia mbali ushindi wa Kenyatta

Wafuasi wa Bw Odinga wakisherehekea uamuzi wa mahakama mtaa wa Mathare, nairobiHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWafuasi wa Bw Odinga wakisherehekea uamuzi wa mahakama mtaa wa Mathare, Nairobi
Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku 60.
Majaji wa mahakama hiyo walisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi ambazo ziliathiri matokeo hayo.
Uamuzi huo wa umeifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika ambapo upinzani umewasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais na wakafanikiwa.
Mgombea urais wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa), waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, aliyekuwa amewasilisha kesi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ameutaja uamuzi huo wa mahakama kuwa wa kihistoria.
"Leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika. Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais," amesema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Rais Kenyatta, akihutubia taaifa baadaye, amesema hakubaliani na uamuzi uliotolewa na mahakama, lakini anaukubali na amewahimiza Wakenya kudumisha amani.
"Jirani yako atasalia kuwa jirani, bila kujali mrengo wao wa kisiasa, dini, rangi," amesema.
"Watu wachache, watu sita (majaji wa Mahakama ya Juu), hawawezi kubadilisha nia ya Wakenya milioni 40. Wakenya ndio wataamua, na hivyo ndivyo demokrasia ilivyo."
"Tuko tayari kurudi kwa debe, kuongea na Wakenya, kuwaambia yale tunataka na yale tunataka kutenda."
Tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza Rais Kenyatta mshindi akiwa na kura 8,203,290 (54.27%) naye Bw Odinga akiwa wa pili akiwa na kura 6,762,224 (44.74%)
Image captionBw Odinga (kati) akiwa na aliyekuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka (kushoto) na Musalia Mudavadi walipokuwa wanaingia mahakamani
Upinzani hata hivyo ulisema mitanbo ya tume ya uchaguzi ilidukuliwa na kuvurugwa kumfaa Bw Kenyatta.
Jaji Mkuu David Maraga akisoma uamuzi wa majaji wengi wa Mahakama ya Juu alisema uchaguzi huo "haukuandaliwa kwa kufuata katiba na sheria za uchaguzi...na ni batili."
Majaji wanne kati ya sita waliunga mkono msimamo huo.
Majaji wawili hata hivyo - Jaji Njoki Ndung'u na Jaji Jakctone Ojwang'- walikuwa na msimamo tofauti, wakisema makosa yaliyotokea hayakuwa makusudi na hayawezi kusababisha kufutiliwa mbali kwa shughuli yote ya uchaguzi.
Uamuzi wa mahakama ulipokelewa kwa shange na wafuasi wa upinzani ndani na nje ya ukumbi wa mahakama.
Image captionUhuru Kenyatta aliingia mdarakani mara ya kwanza 2013,
Makosa yalikuwa wapi?
Jaji Maraga alisema tume ilikosa "kuandaa uchaguzi huo wa urais kwa njia inayotakikana kikatiba na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi".
Hakufafanua ni makosa gani hasa yalitokea, lakini mahakama imeahidi kutoa hukumu yenye maelezo ya kina katika kipindi cha siku 21.
Amesema nyaraka zilizowasilishwa mahakamani ni nyingi na itachukua muda kuzidurusu vyema na kuandika hukumu kamili.
Majaji waliopinga walisema muungano wa upinzani Nasa haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kuthibitisha kura ziliibiwa.
Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Afrika (AU), Marekani na Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Afrika walikuwa wamesema shughuli ya upigaji kura iliendeshwa kwa njia huru na haki na kwa njia ya amani.
Ghasia zilizotokea katika maeneo kadha, wafuasi wa Odinga wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 28.
Ushindani mkali katika uchaguzi huo ulikuwa umezua wasiwasi kwamba huenda kungetokea ghasia - sawa na zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1000 waliuawa na maelfu wengine kufurushwa makwao.
Tume ya uchaguzi imesemaje?
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati amesema watu waliohusika katika kuvuruga uchaguzi wanafaa kuwajibishwa.
Amesema makamishna waliteuliwa mieszi saba tu kabla ya uchaguzi kufanyika lakini maafisa wengine wakuu wa tume hiyo hawakufanyiwa mabadiliko.
Amedokeza kwamba "tume inanuia kufanya mabadiliko ya ndani" na kuangalia upya mifumo yake kabla ya kuandaa uchaguzi mpya.
Amemwalika Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kufanya uchunguzi na kufungulia mashtaka watu wowote ambao walihusika kuvuruga uchaguzi.
Ameitaka Mahakama ya Juu kuharakisha kutoa uamuzi wa kina kusaidia tume hiyo ya uchaguzi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.