Tuesday, November 7

Watu wenye Silaha wavamia kituo cha Runinga, Afghanistan

Operesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionOperesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayo
Watu wenye silaha wamevamia kituo kimoja cha Runinga mjini Kabul Afghanistan na kumuuwa mtu mmoja.
Washambuliaji watatu, waliingia kwa nguvu ndani ya jumba ambalo mna kituo cha Runinga cha Shamshad, baada ya kulipua vilipuzi.
Mlinzi na mmoja wa washambuliaji wanasemekana kuuwawa, huku operesheni ya kiusalama ingali ikiendelea.
Idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana.
Inaaminika kuwa kundi linalojiita Islamic State, ndilo lililohusika na uvamizi huo, hayo ni kwa mjibu wa shirika moja la habari Nchini Afghanistan, Amaq.
Mwaandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa hadi sasa anasikia milio ya risasi, kwani mshambuliaji mmoja aliyesalia anaendelea kukabiliana na walinda usalama.
'Nilifaulu kuhepa'
Shamshad TV ilizima mara tu baada ya shambulio hilo kuanza.
"Badhi ya wafanyikazi wenzangu wameuwawa na wengine kujeruhiwa. Nilifaulu kuhepa," Hashmat Istankzai, ripota wan kituo kimoja kinacjhotangaza kwa lugha ya Pashto, ameiambia BBC.
Shamshad TV, ina vipindi vingi vinavyotangazwa kwa lugha nyingi nchini Afghanistan, ikiwemo taarifa ya Habari kwa lugha ya Pashto.
Ni mojawepo ya vituo vinavyoshirikiana na BBC.
Mji mkuu, Kabul umekuwa ukilengwa mara kwa mara hasa katika miezi ya hivi karibuni, mashambulio ambayo yanateklezwa na wanamgambo wa Taliban na wapiganaji wanaojiita Islamic State.
Afghanistan ni mojawepo ya mataifa hatari zaidi kwa waandishi habari na wafanyikazi wengine wa vyombo vya habari.
Mwezi Mei mwaka huu, Dereva mmoja wa BBC alikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 150 waliouwawa, katika shambulio baya na kubwa zaidi la kujitoa mhanga, lililofanyika katika mji mkuu Kabul.
Mwaka jana, wafanyikazi 7 wakituo kimoja cha kibinafsi cha runinga, cha Tolo TV waliuwawa na mhanga wa kujitoa kufa wa kundi la Taliban Mjini Kabul.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiria ufunguzi wa wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua chumba cha abiria uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya ufunguzi wa uwanja huo wa Ndege.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na kumshukuru Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya shughuli za ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.
Wananchi wakishangilia wakati wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi huo wa uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

MOI:WAGONJWA KULALA CHINI IMEBAKI HISTORIA


Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imekuwa na uwezo wa vitanda 340 ya kulaza wagonjwa na kuachana na kulaza wagonjwa chini ya sakafu iliyokuwa inatokana na ukosefu wa vitanda katika taasisi hiyo.

Uwezo wa MOI kuwa na vitanda hivyo imetokana na jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli kutoa maelekezo ya kutaka watanzania wasipate huduma katika taasisi hiyo wakiwa wamelazwa chini ya sakafu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa MOI, Jumaa Almas, amesema kuwa suala la wagonjwa wanaofika katika taasisi ya MOI kulazwa chini ya sakafu limebaki kuwa historia.

Jumaa amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli alichukua jitihada na kununua vitanda ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika hospitali hiyo.

Meneja huyo amesema taasisi ya MOI mazingira ya kutolea huduma katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Dk. Pombe Magufuli, yameboreshwa na kuanza kutumika kwa mradi wa awamu ya tatu ya kupeleka mazingira ya kazi ya kuwa rafiki kwa watoa huduma na wagonjwa.

Jumaa amesema mazingira katika kipindi cha nyuma yalikuwa hatarishi kwa watumishi na wagonjwa kupata maambukizi kutokana na kuwa nafasi finyu ya kuwa na idadi kuliko uwezo wa nafasi.

Amesema awali wodi yenye vitanda 33 ilikuwa inalaza wagonjwa 90 hadi 100 hali ambayo ilikuwa ni wakati mgumu kwa utoaji huduma kwa watumishi kwa nafasi kuwa finyu ambapo idadi ya wagonjwa wa upasuaji imeongezeka hadi kufikia waonjwa 600 hadi 700 kwa mwezi.
Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Jumaa Almas akizungumza na waandishi habari juu ya mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha Rais Dk. John Pombe Magufuli kutoa maelekezo ya kboresha huduma kwa kununua vitanda leo, jijini Dar es Salaam.

DK. KIGWANGALLA, "SIWEZI KUJARIBIWA NA SIWEZI KUCHEZEWA, SIKO HAPA KWA BAHATI MBAYA"


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hamdun Mansur (katikati) na Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Ndugu Bajuta wakisoma ramani ya Pori Tengefu Loliondo na mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro muda mfupi kabla ya kuaza ziara ya kukagua maeneo hayo jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana, pamoja na mambo mengine alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Wizara hiyo, Prof. Alexander Songorwa kwa tuhuma za rushwa na kuhujumu jitihada halali za Serikali za kumaliza mgogoro huo. Aliagiza Mkurugenzi huyo afikishwe TAKUKURU kwa uchunguzi wa tuhuma hizo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo lenye mgogoro la Pori Tengefu Loliondo jana mkoani Arusha jana.
Dk. Kigwangalla (kulia) akimuhoji mmoja ya wananchi jamii ya wafugaji alipotembelea Pori Tengefu Loliondo jana.
Waziri Kigwangalla (kushoto) akioneshwa  mpaka wa Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori Tegefu Loliondo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Hamdun Mansuri wakati wa ziara yake ya kukagua iwapo mifugo inaingizwa katika hifadhi ya Serengeti kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari. 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SHUGHULI ZA MKUTANO WA TISA WA BUNGE



AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

Imeandikwa na Rais wa Taifa la Palestina, Mheshimiwa Mahmuud Abbas
Waingereza wengi hawamjui “Sir.Arthur James Balfour”ambae aliwahi kuwa Waziri Mkuu mwanzoni mwa karne ya ishirini, lakini jina lake ni maarufu sana kwa Wapalestina wapatao milioni kumi na mbili. Katika kumbukumbu ya azimio la Balfour,serikali ya Uingereza inalazimika kutumia fursa hiyo ili kurekebisha makosa ya kihistoria iliyoyafanya dhidi ya wananchi wetu wa Palestina.

Mnamo Novemba 2,1917 akiwa ofisini kwake mjini London,“Sir.Arthur James Balfour”alisaini barua akiliahidi shirika la kizayuni, kuanzisha taifa lao ndani ya ardhi ya Palestina. Ameahidi kutoa ardhi hiyo wakati sio yake, huku akifumbia macho haki za kisiasa za Wapalestina walioishi katika ardhi hiyo kwa miaka mingi. Kwa Wapalestina ambao ni raia wangu, matukio yaliyosababishwa na barua hii yamekuwa na uharibifu mkubwa, huku pia yakiacha madhara ya muda mrefu kwa wananchi wetu.

Sera ya Uingereza iliyounga mkono uhamaji wa Wayahudi kwenda Palestina, ikiwa ni mbadala wa kukataa kwao haki ya Kiarabu ya Palestina ya kujipangia mustakabali wao, sera hiyo imeleta mvutano mkali kati ya wahamiaji wa Kiyahudi wa Ulaya na wakazi wa asili wa Kipalestina. Palestina iliyokuwa ajenda ya mwisho ya kumaliza ukoloni, inasumbuka kama tunavyosumbuka wananchi wake kutafuta haki yetu isiyo badilika katika kujipangia mustakabali, jambo ambalo ni janga kubwa mno kushuhudiwa na historia ya sasa.

Mnamo mwaka 1948, wanajeshi wa kizayuni waliwafukuza kwa mabavu kutoka katika miji yao, watu wanaofikia milioni moja wakiwemo wanawake na watoto, huku wakifanya mauaji ya kutisha na kubomoa kabisa vijiji kadhaa. Wakati tulipofukuzwa kwa mabavu kutoka mji wa Safad, umri wangu ulikuwa miaka kumi na tatu, wakati Israel ikisherehekea kuasisi taifa lake, sisi Wapalestina tunakumbuka siku ya giza zaidi katika historia yetu. 

Azimio la “Balfour” kwa hakika sio tukio la kusahaulika, kwani wananchi wangu leo wanaofikia zaidi ya milioni kumi na mbili wamesambaa duniani kote, baadhi yao wakilazimishwa kwa nguvu kuacha miji yao mnamo mwaka 1948, huku zaidi ya Wapalestina milioni sita bado wanaishi uhamishoni hadi leo hii, waliosalia katika miji yao ni milioni (1.75) ila wao wanaishi chini ya mfumo wa kibaguzi uliopangika nchini Israel.

Aidha, Wapalestina zaidi ya milioni (2.9) wanaishi Ukingo wa Magharibi wakiwa chini ya uvamizi wa kijeshi na wa kinyama uliogeuka kuwa ni ukoloni. Miongoni mwao wapo wakazi wa Jerusalem ambao ni wa asili kabisa wapatao laki tatu (300,000), bado wanapambana na sera za kivamizi za Israel zinazowahamisha kwa nguvu kutoka katika mji wao. Huku wapalestina wengine wapatao milioni mbili wapo katika Ukanda wa Gaza, ambayo ni gereza la wazi linaloharibiwa mara kwa mara na vifaa vya jeshi la Israel.

Azimio la “Balfour” kwa hakika sio mnasaba wa kusherehekea, hasa katika wakati ambao bado upande mmoja unadhulumiwa na unapata dhiki kwa sababu ya azimio hilo, kuasisiwa kwa taifa la watu fulani, kumepelekea kufukuzwa kwa watu wengine na kuendelea kukandamizwa, haiwezekani kulinganisha kati ya mvamizi na taifa linalokaliwa kimabavu. Ni lazima kulisawazisha kosa hili ambalo Uingereza inabeba jukumu kubwa na inalazimu sherehe hizo zifanywe katika siku ambayo, wakazi wote wa ardhi hii wakiwa katika uhuru, heshima na usawa. 

Tukio la kusaini azimio la “Balfour”, limeshatokea na halibadiliki lakini ni jambo ambalo yapasa kurekebishwa, jambo hili linahitaji unyenyekevu, ushujaa, kukubali yaliyopita, kukiri makosa na kuchukuwa hatua stahiki za kurekebisha makosa hayo. Nami katika mtiririko huu, ninapongeza ushujaa wa wananchi wa Uingereza wanaoitaka serikali yao kuchukua hatua kama hizi zifuatazo: Wabunge 274 wamepiga kura ya kulitambua taifa la Palestina, wakati maelfu ya wananchi wakiitaka serikali yao kuomba radhi kwa azimio la Balfour, huku makundi kadhaa na asasi za kiraia zikiandamana kuunga mkono haki za taifa letu bila usumbufu wowote.

Pamoja na mateso tuliyokumbana nayo karne iliyopita, bado wananchi wa Palestina wamesimama kidete, kwani sisi ni wananchi tunaojifaharisha kwa urithi wake mwingi, ustaarabu wake mkongwe na kwa kutambua ya kwamba Palestina ndio chimbuko la dini tatu za mbinguni. Ukweli wa mambo, tumezoea kwa miaka mingi kuishi na matukio yaliyotuzunguka, ambayo yamesababishwa na mtiririko wa matukio yaliyoanza mwaka 1917, tukafikia makubaliano machungu kwa ajili ya kufikia amani, kuanzia kukubali kuasisiwa taifa la Palestina kwa asilimia 22% tu ya ardhi ya kihistoria, kulitambua taifa la Israel bila ya sisi kutambuliwa hadi leo hii.

Tukawa na msimamo wa ufumbuzi wa dola mbili kwa muda wa miaka thelathini iliyopita, msimamo ambao utekelezaji wake umekuwa hauwezekani pamoja na muda kupita. Hivyo basi, muda wa kuwa Israel inaendelea kupata kinga na misaada kutoka jamii za kimataifa, badala ya kuichukulia hatua kwa ukiukaji wake unaoendelea dhidi ya misingi ya sheria za kimataifa, jambo hilo halitaihamasisha kuacha uvamizi wake na lazima huu utakuwa ni mtazamo dhaifu.

Inapasa kwa Israel na marafiki zake kutambua vizuri kuwa, ufumbuzi wa kuwepo dola mbili unaweza kwisha kabisa, isipokuwa taifa la Palestina litabaki hapa na kuendelea na juhudi zake ili kurudisha uhuru wake, iwe kupitia ufumbuzi wa dola mbili au mapambano kwa ajili ya kujipatia haki sawa kwa kila mkazi wa Palestina ya kihistoria.

Muda umefika sasa kwa serikali ya Uingereza kuchukua nafasi yake, kwani kuchukua hatua stahiki kunalenga kumaliza uvamizi kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio yake, likiwemo azimio la hivi karibuni la Baraza la Usalama namba 2334 na kulitambua taifa la Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967, lenye mji mkuu wake Jerusalem ya Mashariki. Kufanya hivyo, kutapeleka mbele upatikanaji wa haki za kisiasa za wananchi wa Palestina, kuondoa dhulma kwa wananchi hao na usawa wa haki zake za kisheria, bila shaka utachangia kupatikana amani iliyo sawa ya uadilifu na ya kudumu katika Mashariki ya Kati kwa Wapalestina, waisrael na mataifa mengine ya eneo husika. 

ESRF YAWEZESHA WARSHA YA ANDIKO THABITI LA UTAFITI

Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3 kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la kuombea fedha kwa ajili ya tafiti. Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam. 

Akizungumza Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa. Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko bora ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Wanazuoni (Think Tank Initiatives-TTI) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda nchini. “Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi Alisisitiza umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifungua warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

 Aliongeza kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Alisisitiza kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini. Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti.  Picha juu na chini ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji Maendeleo Afrika, Prof. Olu Ajakaiye akielezea namna bora ya utengenezaji wa maandiko kwa ufupi na kwa usahihi wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kwa washiriki kutoka shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana iliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia program ya TTI , Julie LaFrance, amesema kwamba ni muhimu kwa watafiti kuendelea na utafiti endelevu na wa kina ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii ya watu baada ya kupata matokeo baada ya utafiti. 

Aliongeza kwamba baada ya semina hiyo watafiti wa ndani watakuwa wamepata uelewa mkubwa wa kuandika mapendeko thabiti na bora zaidi yenye kuvutia wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kuanza kuwapa fedha kwa ajili ya tafiti zenye tija nchini. Warsha hiyo pia iliwakutanisha watafiti kutoka Taasisi ya IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na chuo cha Jamii kutoka Ghana.   Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akiwasilisha mada umuhimu wa jinsia kama moja ya kipengele muhimu katika kuandaa maandiko mbalimbali ya kitafiti katika kushawishi wabia wa maendeleo kutoa ruzuku za uatfiti.  Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifurahi jambo wakati mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3095" align="aligncenter" width="1404"] Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akichangia jambo wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI. Prof. Peter Okidi-Lating (aliyesimama) kutoka Chuo Kikuu cha Makerere akipitia meza za vikundi kazi vya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI. Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa zoezi la vikundi kazi katika meza ya washirki kutoka ESRF katika warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Pichani juu mshiriki Aldegunda Ngowi kutoka ESRF na chini ni mshiriki kutoka Ghana wakichangia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo.  Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kutoka Shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana   Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akibadilishana mawazo na Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance wakati warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 7,2017