Tuesday, November 7

Watu wenye Silaha wavamia kituo cha Runinga, Afghanistan

Operesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionOperesheni ya kiusalama inaendelea kwa sasa katika eneo la mashambulio hayo
Watu wenye silaha wamevamia kituo kimoja cha Runinga mjini Kabul Afghanistan na kumuuwa mtu mmoja.
Washambuliaji watatu, waliingia kwa nguvu ndani ya jumba ambalo mna kituo cha Runinga cha Shamshad, baada ya kulipua vilipuzi.
Mlinzi na mmoja wa washambuliaji wanasemekana kuuwawa, huku operesheni ya kiusalama ingali ikiendelea.
Idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana.
Inaaminika kuwa kundi linalojiita Islamic State, ndilo lililohusika na uvamizi huo, hayo ni kwa mjibu wa shirika moja la habari Nchini Afghanistan, Amaq.
Mwaandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa hadi sasa anasikia milio ya risasi, kwani mshambuliaji mmoja aliyesalia anaendelea kukabiliana na walinda usalama.
'Nilifaulu kuhepa'
Shamshad TV ilizima mara tu baada ya shambulio hilo kuanza.
"Badhi ya wafanyikazi wenzangu wameuwawa na wengine kujeruhiwa. Nilifaulu kuhepa," Hashmat Istankzai, ripota wan kituo kimoja kinacjhotangaza kwa lugha ya Pashto, ameiambia BBC.
Shamshad TV, ina vipindi vingi vinavyotangazwa kwa lugha nyingi nchini Afghanistan, ikiwemo taarifa ya Habari kwa lugha ya Pashto.
Ni mojawepo ya vituo vinavyoshirikiana na BBC.
Mji mkuu, Kabul umekuwa ukilengwa mara kwa mara hasa katika miezi ya hivi karibuni, mashambulio ambayo yanateklezwa na wanamgambo wa Taliban na wapiganaji wanaojiita Islamic State.
Afghanistan ni mojawepo ya mataifa hatari zaidi kwa waandishi habari na wafanyikazi wengine wa vyombo vya habari.
Mwezi Mei mwaka huu, Dereva mmoja wa BBC alikuwa miongoni mwa zaidi ya watu 150 waliouwawa, katika shambulio baya na kubwa zaidi la kujitoa mhanga, lililofanyika katika mji mkuu Kabul.
Mwaka jana, wafanyikazi 7 wakituo kimoja cha kibinafsi cha runinga, cha Tolo TV waliuwawa na mhanga wa kujitoa kufa wa kundi la Taliban Mjini Kabul.

No comments:

Post a Comment