Baada ya kuwasili katika maadhimisho hayo yanayofanyika leo Alhamisi Novemba 9,2017, Makamu wa Rais amekagua gwaride maalumu na kupokea maandamano yakiongozwa na farasi na pikipiki.
Maadhimisho yamepambwa na vikundi mbalimbali vya wanawake, vikiwemo vikosi maalumu vya kupambana na uhalifu na cha komandoo wanawake.
Samia pia atatembelea mabanda na kukagua shughuli zinazofanywa na polisi wanawake.
Miongoni mwa mabanda yaliyopo, lipo kwa ajili ya uchangiaji damu.
No comments:
Post a Comment