Thursday, August 10

NISHATI

WADAU WA NISHATI KUTOKA UMOJA WA ULAYA NA TANZANIA WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA NISHATI KATIKA MAJENGO MAKUBWA NCHINI


Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya,Margareta Zidar akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.



Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya, Lena Lampropoulou, akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.



Wadau mbalimbali wa Masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa wakiwa wanafuatilia mada katika Semina hiyo ya Nishati katika Majengo Makubwa



Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa



Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa



Wadau wa Masuala ya Nishati ya Majengo Makubwa kutoka nchini Tanzania na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Semina yao ya masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa iliyofanyika Serena Hotel Dar es Salaam.

JESHI LA POLISI


MASAUNI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA POLISI, AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema, Wilayani Kigamboni   kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict   Kitalika.



 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es  Salaam.


 
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa.



 Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.



 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni   ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali.



 Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. 



Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI YAMALIZA SINTOFAHAMU YA TANI 3,700 ZA TUMBAKU.


 SERIKALI imefanikiwa kumaliza sintofahamu ilikuwepo baina ya wakulima na wanunuzi wa tumbaku mkoani Tabora juu ya uwepo wa tani 3,700 zilizokosa soko.

Tani 3,700 zilikuwa zimekosa wanunuzi kwa sababu hazikuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi na hivyo kuhitaji utatuzi wa haraka wa Serikali ili kuinusuru tumbaku hiyo.

“Tumefanikiwa kuongea nao na tutauza zile tani 3,700 kwa wanunuzi,” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuamsha shangwe ukumbi mzima.

Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Aliwashukuru wanunuzi kwa kukubali kumaliza tatizo hilo kwani litaleta ari mpya kwa wakulima na kuwafanya wajipange vizuri kwa msimu ujao. “Makampuni ya ununuzi yatapita kwenye maeneo yenu, WETCU watafuatilia na tumekubaliana nao kuwa tutafanya kazi pamoja,” alisema Waziri Mkuu.

Kufuatia sintofahamu hiyo, wiki iliyopita, wakazi wa mkoa huo waliomuomba Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aingile kati ili kuwanusuru na adha ya zao hilo kukosa soko. Naye akawaahidi wananchi hao kwamba suala hilo atalikamilisha Waziri Mkuu.

Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Aggrey Mwanri wakati akiwasilisha muhtasari wa taarifa ya mkoa huo alisema katika masoko ya tumbaku yanayoendelea, kuna tatizo la tumbaku kukosa  wanunuzi kwani hapakuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi.

“Tumbaku inayofikia kilo milioni 3.7 kwa sehemu kubwa ililimwa kwa ufadhili waWETCU Ltd, kwa fedha ambazo zilikuwa ziende APEX. WETCU walinunua pembejeo na kuwapa wakulima waliokuwa chini ya vyama sinzia, na sasa haina wanunuzi. Tunaomba ulisemee hilo ili tupate ufumbuzi wa suala hili,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni mbunge wa Urambo, Mheshimiwa Margareth Sitta aliiomba Serikali ikubali kuliangalia suala hilo la tani za ziada 3,700 kwani wakulima wamejaza tumbaku majumbani mwao na kwenye maghala.

“Wakulima wetu wanahitaji kuuza hii tumbaku ili wapate fedha za kuanzia msimu ujao wa kilimo. Lakini pia tunaomba liangaliwe suala la upangaji madaraja ya tumbaku, wasaidiwe kukabili bei isiyotabirika na kutatua ukosefu wa soko la uhakika,” alisema Mama Sitta.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

SEVEN OPPORTUNITIES IN THE UGANDA-TANZANIA PIPELINE PROJECT AND HOW TO PARTICIPATE.


7 Opportunities in the Uganda-Tanzania Pipeline Project and How to Participate.
THE EAST African oil pipeline (or the Uganda-Tanzania pipeline is the talk of the town now. Not only in East Africa but all over the globe.
The construction of this pipeline is officially on. Social and resettlement planning services have been undertaking it in Tanzania.

The sad reality is that people don’t know about the business opportunities available in the project.
More and more people keep wondering what the opportunities emerging in this project are and how they can be part of it.
“Do they offer equipment or provide services?” they ask themselves.
If you are among these people seeking to do business in this projects but have no idea how to get started, then no need to worry.
This article shows you some opportunities available in the project and how you can participate so that you can reap a substantial profit.
The Tanzania-Uganda Pipeline Opportunities
  1. Pipes and connection supplies: One of the opportunities in this project is to supply and manufacture seamless tubes and pipes (LSAW) and also supplying steel pipes.
  2. Chemical Supplies: For the construction of the pipelines, there are a lot of specialty chemicals needed, from corrosion inhibitors additives to scale remover to chemicals that reduce paraffin build up. You cannot run a pipeline without these things, and you can get them from China really cheap. Which means your profit margin may increase by 30-50 percent.
  3. Pipeline equipment supplies: These cover all materials that are required in the pipeline transportation system. It includes fittings, valves, scraper traps, insulating flanges, flow tee, pumping station, etc.
  4. Civil engineering works: These include building construction work, construction and maintenance of roads, construction and maintenance of drainage system, etc.
  5. Pipeline inspection services.
  6. Food supply.
  7. Security services.
Are you ready to utilize opportunities in this project? Here is how to grab the opportunities:
1. Identify the decision makers and influencers in this Uganda-Tanzania pipeline project.
The first step in pursuing opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline is determining who the decision makers are.
Decision makers are the people who can approve or disapprove your proposal.
No matter how big a company is, there are decision makers who can approve or disapprove documents.
This can be easily achieved by making a list of key players in the project and starting to build long term relationship with them.
2. Demonstrate your experience.
You should demonstrate that you are the right person to execute the project you’re proposing.
You should demonstrate your capability and your experiences in executing similar project.
“What if my business is small and new n the industry?” you may ask.
Well, the answer is pretty simple. You still have a chance to tap opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline project.
If your business is small and new, and you don’t have any experience or working history to be taken as references to the service you want to render, you should consider going into a joint venture with an experienced contractor in the oil and gas industry in such bidding venture. However inexperienced, you still have a chance to participate in this work.
You have learned the opportunities in the East Africa pipeline project and you now know how to access them.
If you want to learn more about the opportunities in the Tanzanian oil and gas sector and how you can grab them, 

SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI



Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.


Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Kanuni za taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Crossborder Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ambapo wasafirishaji wa fedha taslimu na wasafiri wote wanaotoka au kuingia nchini, watatakiwa kutoa taarifa za fedha taslimu wanazosafirisha ikiwa fedha hizo zinalingana au zinazidi kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi (USD 10,000).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni hizo, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema utekelezaji wa kanuni hizi, pamoja na mambo mengine utaiwezesha nchi kuwa na takwimu za usafirishaji fedha taslimu.

“Takwimu hizo zitakazosaidia pamoja na mambo mengine kubaini vitendo vya kihalifu, kupunguza utoroshaji wa mitaji na kuhakikisha kuwa tunapunguza kama siyo kumaliza kabisa usafirishaji wa fedha zitokanazo na uhalifu au/na fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi” alisema Bw. Makombe

Aidha kanuni hizo zimeweka adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakabainika kutaka kupita na fedha zinazolingana au zinazozidi kiwango kilichowekwa bila kutoa taarifa au watakaotoa taarifa za uongo. Alizitaja adhabu hizo kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa fedha taslimu walizonazo na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kama vile kufunguliwa mashtaka.

“Wahalifu pamoja na mambo mengine, wanapenda kusafiri na fedha taslimu kwani wanaogopa kutumia benki kutuma fedha kutokana na umakini unaoongezeka katika benki na udhaifu unaoweza kuwepo mipakani” Alisisitiza Bw. Makombe.Kamishna huyo amewaasa washiriki wa warsha hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kuziba mianya yote ambayo wahalifu wanaweza kuitumia kutimiza kusudi lao ovu na kuhatarisha usalama wa nchi.

Kutokana na umuhimu wa ushiriki wa wadau mbalimbali katika utekelezaji wa kanuni hizo warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka taasisi mbalimbali wengi wao wakiwa ni maafisa forodha.

Washiriki hao wametoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kikanda, Mamlaka ya Mapato Tanzania na vikosi vya ulinzi na usalama

Wengine ni Bodi ya Mapato Zanzibar, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo-Zanzibar, Shirika la Posta, Benki kuu ya Tanzania, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Zanzibar, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Tanzania Bara Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bara na Zanzibar, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Idara ya uhamiaji na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.

MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA TEHAMA KUANDA MIPANGO YA BAJETI ZA MAMLAKA ZA SERIKALI WAFUNGULIWA MOROGORO



Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, akifungua mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma nchini, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).


Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA, Ofisi ya Rais Tamisemi, Baltazar Kibola, akiwasilisha mada juu ya mfumo mpya wa Tehama ulioboreshwa ujulikanao kama ‘PlanRep’ utakaoanza kutumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).



Meneja Mifumo ya TEHAMA kutoka Mradi wa PS3, Revocatus Mtesigwa, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama (hawapo pichani) utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa, mkoani Morogoro jana 





Washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa na wataalam kutoka Tamisemi na Mradi wa PS3, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI







 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. 



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. ill Gates aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dk Charles Tizeba (wa tatu Kushoto), Msaidizi wa rais Masuala ya diplomasia Bi. Zuhura Bundala (kushoto)  pamoja na maafisa alioongozana nao Bw. Bill Gates



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa katika mazungumzo na   Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.PICHA NA IKULU