Friday, September 8

Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa Caribbean

Police patrol the area as Hurricane Irma slams across islands in the northern Caribbean on Wednesday, in San Juan, Puerto Rico, 6 SeptemberHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean
Kimbunga kikali kwa jina Irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo takriban watu saba wameuawa.
Kisiwa kidogo cha Barbuda kilisemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa maeneo ya kisiwa cha St Martin yanayomilikiwa na Uingereza yameharibiwa kabisa.
Jitihada za uokoaji zinatatizwa kutokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maeneo mengine.
Image captionKimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean
Wakati huo huo upepo umetajwa kupata nguvu na kuwa vimbunga viwili.
Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico.
Zaidi ya nusu ya wakaazi wote milioni tatu wa Puerto Rico hawana umeme baaada ya kimbunga Irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali. Maafiasa wanasema huenda umeme ukakosa kwa siku kadhaa.
Image captionKimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean
Kimbunga hicho chenye nguvu nyingi kuwai kushuhudiwa kwa miongo kadha kilikuwa na upepo wa kasi ya kilomita 295 kwa saa na kilitarajiwa kupita karibu na kwenye pwani cha Jamhuri wa Dominica leo Alhamisi
Kimbunga Irma kwanza kilikumba kisiwa cha Antigua na Barbuda. Takriban mtu mmoja aliripotiwa kuuliwa ambapo waziri mkuu Gaston Brown alisema kuwa karibu asilimia 95 ya majengo yaliharibiwa.
Image captionKimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean
Hata hivyo alisema kuwa watu wote 80,000 nchini Antigua na Barbuda walinusurika maafa.
Maafisa wamethibisha vifo vya takriban watu 6 na uharibifu kwenye himaya za Ufaransa za St Martin na Saint Barthélemy.
Umeme umekatwa katika visiwa vyote na makundi ya kutoa huduma za dharura yanajaribu kufika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Ndege za Israel zashambulia kiwanda cha silaha za kemikali nchini Syria

Ndege za Israel zashambulia kiwanda cha silaha nchini SyriaHaki miliki ya pichaIVAN SIDORENKO
Image captionNdege za Israel zashambulia kiwanda cha silaha nchini Syria
Syria inasema kuwa ndege za jeshi la Israeli zimeshambulia kituo cha kijeshi magharibi mwa nchi huku ripoti zikiseka kuwa kiwanda cha silaha za kemikali zilishambuliwa.
Taarifa za jeshi zilisema kuwa makombora yaliyofyatuliwa kutoka anga ya Lebanon yalilenga kiwanda hicho kilicho karibu na Masyaf na kuwaua wanajeshi wawili.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kiwanda ya kutengeneza silaha za kemikali kilishambuliwa
Israeli ambayo imefanya mashambulizi kadha kwenye viwanda vya silaha nchini Syria awalia haijasema lolote.
Kisa hicho kinatokea siku moja baada wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kusema kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulizi la silaha za kemikali katika mji unaoshilkiliwa na waasi mwezi Aprili.
Image captio
Takriban watu 83 waliuawa katika mji wa Khan Sheikhoun na Styria imekana kutumia silaha za kemikali.
Ujasusi wa nchi za magharibi unasema kuwa Syria inandelea kuunda silaha za kemikali.
Isarel inaripotiwa kuendesha mashambulizi ya ndega maeneo yanayotajwa kutumika kuunda silaha za kemikali miaka ya hivi karibuni.
Hivi karibuni Isreal iliishitumu Syria kwa kuruhusu hasimu wake Iran kujenga viwanda vya makombora nchini humo na inasema inalenga kuzuia kupelekwa kwa silaha kutoka Syria hadi kwa wanamgambo wa Lebanon, Hezbolllah.

Macron ataka kujadiliwa kwa mustakabali wa Ulaya

Macron anasema hii ndio njia pekee ya kulikomboa bara hilo
Image captionMacron anasema hii ndio njia pekee ya kulikomboa bara hilo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka kufanyika kwa mkutano wa haraka kujadili mustakabali wa bara la Ulaya.
Akizungumza mjini Athens, Macron ameonya kwamba Ulaya itakufa iwapo haitabadilika.
Amesema viongozi wa Ulaya wanapaswa kuwasilisha mapendekezo yao ifikapo mwishoni mwa mwaka, yatayofungua mjadala kwa wananchi kuamua ni aina gani ya muungano wanaouhitaji.
Mependekezo hayo yanatarajiwa kutoa picha mpya ya namna ya kuboresha umoja wa Ulaya
Image captionMependekezo hayo yanatarajiwa kutoa picha mpya ya namna ya kuboresha umoja wa Ulaya
Macron ameahidi kuwasilisha mapendelezo yake ndani ya wiki chache zijazo, huku akisema itahusisha njia za kidemokrasia zaidi ikiwemo bunge la nchi yake.

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana

Tundu Lissu,mwanasheria mkuu wa CHADEMAHaki miliki ya pichaBUNGE
Image captionTundu Lissu,mwanasheria mkuu wa CHADEMA
Mwanasiasa wa upinzani nchni Tanzania Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.
Mwanasiasa huyo amekimbizwa hospitali ya mkoa wa Dodoma na kupokea huduma ya kwanza na taarifa zinasema kuna mipango ya kumsafirisha hadi Nairobi kwa matibabu zaidi.
Rais wa Tanzania John Magufuli kupitia kwenye Twitter amesema amesikitishwa sana na kushambuliwa kwa mbunge huyo.
Ameandika: "Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria."
Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki akiwa nyumbani kwake.
Chama hicho kimelaani vikali tukio hilo.
Wakati huo huo, Chama tawala cha CCM, kupitia Katibu wao wa Itikadi na Uenezi,imesema kimepokea kwa mstuko mkubwa kushambuliwa kwa mbunge huyo wa upinzani.
"Chama cha Mapinduzi (CCM) kinalaani tukio hilo la kikatili na lisilo na utu tunalitaka Jeshi la Polisi kuwatafuta, kufanya uchunguzi wa tukio hili na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote waliohusika."
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi, Jires Mroto ameiambia BBC kuwa wameanza uchunguzi wa tukio hilo.
"Tunaomba wananchi wenye taarifa ya uhalifu huu, waweze kujitokeza" amesema Kamanda Mroto.
Hivi karibuni, mbunge huyo kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA, amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanya uchochezi.
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akithibitisha tukio la leo alisema, amesema "yupo hospitali, bado anajaribu kupambana kuokoa maisha yake"
Gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, limemnukuu Mganga mkuu wa hospitali ya Dodoma akisema wakili huyo ana majeraha ya risasi miguuni na tumboni.