Monday, October 9

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI WAPYA IKULU DAR ES SALAAM LEO


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Angela Kairuki kuwa Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Hamisi Kigwangwalla  kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Mhe. Suleiman Saidi Jafo  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa) Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Kangi Lugola kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Stella Alex Ikupa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Juliana Shonza  kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai Ikulu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya kumbukumbu na Mawaziri na Naibu Mawaziri baada ya hafla ya kuapishwa  jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na aliyekuwa  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila huku Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu wa Bunge Mpya Mhe. Stephen Magaigai wakianfalia Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri mara tu baada ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya  Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba baada ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya  kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi) Mhe. George Mkuchika huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu  Waziri wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Kangi Lugola huku  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wizara ya Nishati Mhe. Subira Hamisi Mgalu huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Kilimo Dklt. Mary Mwanjelwa huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri  Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega  huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mhe. Juliana Shonza huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde   huku Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassima Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiangalia baada ya hafla ya kuapishwa  Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2017. Picha na IKULU

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA UADILIFI


 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (Kushoto) wakati alipokaribishwa katika ofisi za Wizara leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na Wa pili kushoto Katibu Mkuu Dkt. Maria Sasabo (Sekta ya Mawasiliano).
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri Eng. Atashasta Nditiye (Kulia), wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akisalimiana na Naibu Waziri hiyo Mhe. Elias Kwandikwa wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo. 
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akiwakabidhi manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa wakati (Katikati) vitabu vya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara hiyo kama mwongozo wa utendaji kazi mara baada ya kuapishwa jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

“Mimi nafurahi sana kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano. Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.

 Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
 “Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu. Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema .

Waziri amesema Wizara hiyo imefanya kazi nzuri na hili limewezekana kwa sababu sisi kama wizara tumezingatia maadili ya msingi katika utendaji wa kazi zetu, kuna timu nzuri ya watalaam ambao ni wachapa kazi, wana moyo wa kujituma na kazi zote walizozifanya zina matokeo mazuri. 

Kazi nzuri imefanyika, nawaomba  waheshimiwa manaibu mawaziri tufanye kazi kama timu moja na watalaam wetu ili tuweze kufikia malengo ambayo tumejiwekea katika wizara yetu, amesisitiza Waziri Mbarawa.Kwa upande wake Naibu Waziri anayeshughulikia Eng. Atashasta Nditiye anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano amesema kuwa amejipanga kufanya kazi na kulete matokea chanya na kwa maendeleo ya nchi.

“Nipo tayari kufanya kazi itakayoleta mabadiliko, tutaboresha miundombinu ili kuchochea kasi ya ukuaji wa viwanda na kila nitakachofanya ni utekelezaji wa yale amabayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayatarajia,” amesema mhandisi Nditiye.



Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri tangu serikali yake iingie madarakani Novemba 2015.

Tanzania Kushiriki Tamasha la 19 la Vijana na Wanafunzi nchini Urusi


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi akizungumza na baadhi ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi kabla ya kuwakabidhi bendera mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (katikati) akimkabidhi bendera mmoja wa vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Venerose Mtenga toka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Bw. Erick Shitindi juu ya vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la Vijana na Wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Erick Shitindi (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na vijana watakaoshiriki tamasha la 19 la Dunia la vijana na wanafunzi jijini Sochi nchini Urusi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

Na. Eliphace Marwa 
JUMLA ya Vijana 31 wanatarajia kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la dunia la vijana linalotarajia kufanyika Jijini Sochi nchini Urusi  kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 22 Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na ujumbe wa Vijana hao leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa bendera ya Taifa,  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Erick Shitindi alisema tamasha hilo litakuwa na zaidi ya washiriki ishirini elfu kutoka nchi 150 Duniani kote.
 Shitindi aliwapongeza vijana hao kwa fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo na kuwaomba kuitumia vyema fursa hiyo kwa ajili ya kuiwakilisha vema na kutangaza uzuri wa nchi viongozi kwa mataifa mbalimbali.
“Tamasha hili litatoa fursa kwenu vijana wa Tanzania na mtakapokuwa huko kuzungumzia mambo mazuri ya Tanzania na hasa kutangaza uzuri wa nchi yetu kwa vijana wa mataifa mengine” alisema Shitindi.
Aidha Shitindi aliwaasa vijana hao kwa kutambua kuwa wanakwenda nchi ya ugenini na hivyo kuwa makini kwa kuwa  watakutana na watu mbalimbali wenye tabia, maadili na itikadi za mlengo tofauti tofauti za kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.
“ Kama mnavyofahamu Tanzania inasifika Duniani kote kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu na ni nchi yenye maadili safi, hivyo tunategemea nanyi mtaenda kuonyesha nidhamu ya hali ya juu huko ugenini” aliongeza Katibu Mkuu Shitindi.
Shitindi aliwataka vijana hao kueleza uzuri na mandhari ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Mbuga za Serengeti na bonde la Ngorongoro ambalo ni moja kati ya maajabu saba ya dunia kuwa vipo na ni mali ya Tanzania na si vinginevyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Vijana Bi. Venerose Mtenga kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - ambaye ndiye mkuu wa msafara huo, alimuahidi Shitindi kuwa vijana hao watakuwa mabalozi wazuri kwa Tanzania.
Lengo la tamasha hilo ni kuwakutanisha vijana kutoka nchi mbalimbali duniani ili kujenga mshikamano, kubadilishana uzoefu kidiplomasia, na uzoefu katika mbinu mbali mbali za maendeleo katika utandawazi”, alisema Venerose Mtenga .

WAZIRI WA NISHATI, WAZIRI WA MADINI NA MANAIBU WAZIRI WAO WARIPOTI RASMI OFISI ZA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki, pamoja na Manaibu Waziri wa Wizara hizo wameripoti rasmi katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Ofisi hizo, Mawaziri hao  walifanya kikao cha pamoja ili kufahamishana masuala mbalimbali. Kikao hicho kiliwahusisha pia  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe na Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi, Juliana Pallangyo.

Aidha,  Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walifanya  kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

Viongozi hao wanaosimamia Sekta ya Madini, wanatarajia kufanya kikao na watumishi wa Wizara husika tarehe 10 Oktoba, 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu walikutana na Wafanyakazi wa Wizara husika na kutoa maagizo mbalimbali yatakayoboresha Sekta ya Nishati na hasa upatikanaji wa Umeme wa uhakika, unaotabirika na wa bei nafuu.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia), Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa pili kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa kwa kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) wakiwa katika kikao na Watumishi wa Wizara husika (hawapo pichani )katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki (wa kwanza kulia),  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. James Mdoe (wa kwanza kushoto) wakiwa katika Ofisi  za Wizara jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Kamishna Msaidizi wa Madini, Latifa Mtoro.

WATU 12 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI YA GARI NDOGO (HIACE) KUTUMBUKIA ZIWA VICTORIA, RAIS DKT MAHUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI


 Juhudi za kuopoa miili ya watu waliokuwemo kwenye gari hiyo ikiendelea.
 Baadhi ya Wananchi mbalimbali wakilishuhudia tukio hilo la kuzama kwa gari ndogo ya abiria (HIACE),ambalo  namba zake za usajili hazikuweza kutambulika mara moja,mara baada ya kuopolewa ziwani.
 Wananchi kutoka maeneo mbali mbali wakilifuatilia tukio hilo mapema leo Kigongo Feri jijini Mwanza
Globu ya Jamii imepokea picha na maelezo kadhaa kutoka kwa mdau aliyeko jijini Mwanza zikionesha na kueleza kutokea kwa ajali  jijini humo mapema leo,amesema kuwa ajali hiyo ni ya gari ndogo ya abiria Hiace ikiwa na ibiria imepitiliza na kutumbukia ziwa Victoria katika kivuko cha kigongo  feri -Busisi,Wilayani Misungwi na kusababisha vifo vya watu 12  na majeruhi wawili.

WAZIRI JAFO ATETA NA WATUMISHI WA TAMISEMI

Kadinali Pengo, Vatican watoa msimamo wa Kanisa juu ya Katiba mpya Tanzania

Askofu Marek Solczynski
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Marek Solczynski wametoa msimamo rasmi wa kanisa Katoliki kuhusu suala la Katiba mpya nchini Tanzania.
Kauli hizo zimekuja siku chache baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge, Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi kueleza umuhimu wa Katiba mpya kuwa ndiyo kipaumbele cha kwanza cha Watanzania.
Askofu Niwemugiza alisema yeye kama kiongozi wa dini anaongozwa na maadili, haki na ukweli hivyo hajali namna wengine watakavyomchukulia.
Akifungua mkutano wa asasi za kiraia uliolenga kujadili kuhusu Katiba Mpya wiki iliyopita, Askofu Niwemugizi alisema imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri.
Amesema hakuna mtetezi wa haki za binadamu anayetaka nchi iingie kwenye machafuko kwani wote lengo lao ni kuchochea maendeleo, amani na utulivu.

Askofu Niwemugizi alisema kuanza kutokea kwa matukio ya kuteka watoto, vifo katika mazingira ya kutatanisha na ongezeko la watu wasiojulikana ni ishara mbaya.

"Hizi sio dalili nzuri kwa Taifa lenye afya njema. Ni vielelezo vyenye dira mbaya. Imefika wakati tukae kama Taifa tukubaliane kuwa tunataka dira njema ambayo ni Katiba."
Akizungumza Dar es Salaam Jumamosi Kadinali Pengo amesema kauli ya Askofu Niwemugizi ni maoni binafsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Suala la Katiba Mpya ambalo baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wanajaribu kuligeuza kuwa ajenda kuu kwa sasa, Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inavyofanya.
“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni Katiba Mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya Katiba Mpya.
Kwangu mimi Katiba ni kitu ambacho kije baadaye, si cha haraka. “Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya Katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya Katiba,” alisisitiza Kadinali Pengo.
“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo si msimamo wa Kanisa na hauwezi kuwa msimamo wa kanisa kwa sababu sisi tuna taratibu zetu za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.
Alisema kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndiyo msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli hiyo imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa Kanisa au jimbo anakotoka.
Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Solczynski hakutofautiana na kauli ya Kadinali Pengo kwa kusema kuwa pamoja na kwamba Askofu Niwemugizi ana haki ya kutoa maoni yake lakini tatizo linakuja pale watu wakaposhindwa kung’amua kuwa ni maoni binafsi au ni ya Kanisa.
Alisisitiza kuwa Kanisa lina taratibu zake za kutoa maoni kwa masuala ya kijamii na kwa Serikali.

ADF yashambulia majeshi ya UN

Walinzi wa amani wa UN nchini DRC
Waasi wa Uganda ADF wamefanya mashambulizi katika kambi ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na mwanajeshi wa Tanzania ameuawa.
Kambi hiyo ni kituo cha Kijeshi cha UN ambako ni makazi ya askari wa kulinda amani wa Tanzania, ambayo ni sehemu ya brigedia inayofanya ulinzi na inaruhusa ya kufanya mashambulizi dhidi ya waasi.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti tukio hilo na Mtanzania huyo ni kati ya watu waliouwawa katika shambulizi hilo.
Shambulizi hilo limemuuwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) na kujeruhi dazeni ya watu, kwa mujibu wa tamko la majeshi ya UN, MONUSCO, na jeshi la Congo.
Msemaji wa Jeshi la Congo Mak Hazukay amesema kuwa anaamini waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces au ADF kikundi cha wapiganaji wa Kiislam wa Uganda, kilihusika na shambulizi hilo, na pia mapambano mengine katika eneo hilo katika siku za karibuni. 

Kituo cha kijeshi kilichoko karibu na mashariki ya mji wa Beni pia kilishambuliwa mapema Jumatatu.