Monday, October 9

ADF yashambulia majeshi ya UN

Walinzi wa amani wa UN nchini DRC
Waasi wa Uganda ADF wamefanya mashambulizi katika kambi ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na mwanajeshi wa Tanzania ameuawa.
Kambi hiyo ni kituo cha Kijeshi cha UN ambako ni makazi ya askari wa kulinda amani wa Tanzania, ambayo ni sehemu ya brigedia inayofanya ulinzi na inaruhusa ya kufanya mashambulizi dhidi ya waasi.
Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti tukio hilo na Mtanzania huyo ni kati ya watu waliouwawa katika shambulizi hilo.
Shambulizi hilo limemuuwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) na kujeruhi dazeni ya watu, kwa mujibu wa tamko la majeshi ya UN, MONUSCO, na jeshi la Congo.
Msemaji wa Jeshi la Congo Mak Hazukay amesema kuwa anaamini waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces au ADF kikundi cha wapiganaji wa Kiislam wa Uganda, kilihusika na shambulizi hilo, na pia mapambano mengine katika eneo hilo katika siku za karibuni. 

Kituo cha kijeshi kilichoko karibu na mashariki ya mji wa Beni pia kilishambuliwa mapema Jumatatu.

No comments:

Post a Comment