Thursday, August 31

KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION DONATES AN AMBULANCE TO IDODI HEALTH CENTRE, IRINGA


In fulfilment of its Corporate Social Responsibility, the Karimjee Jivanjee Foundation has donated a brand new ambulance to Idodi health centre through the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Hon William Lukuvi worth US$47,519.

The vehicle is meant to ease the challenges faced by Idodi health centres that hinder them to offer health services to the citizen effectively. Present during the presentation was Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee and Toyota Tanzania Executive Director, Yusuf A. Karimjee.

Speaking at the event Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee said that the Foundation is committed to support communities in Tanzania primarily through education and applauds the efforts of Idodi health centre to support the patients.

The Hon William Lukuvi thanked the Karimjee Jivanjee Foundation and Toyota Tanzania Ltd for their generosity, said that Toyota is the world’s most successful vehicle manufacturer. For seven generation, the Karimjee Jivanjee Group has established a strong record for its philanthropic activities by contributing to the development and growth of Tanzania and East Africa.

The Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) is an amalgamation of various Karimjee Jivanjee charitable institutions since the 1940’s. It was founded as a trust in 2006 and officially registered in 2010. Today, KJF’s core charitable and CSR focus centres on Education in Tanzania, most notably by providing annual scholarships to young Tanzanians to study at graduate level. 

Other past projects and partnerships have included: providing scholarships to Doctors to graduate for Masters Degree in Pediatric Oncology at Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS) through Tumaini la Maisha (NGO), supporting Read International in supplying text books to secondary schools, supporting Rotary International with various projects including the Muhimbili National Hospital (Cancer ward), promoting science and technology in Tanzania through the Young Scientists Tanzania (YST) programme and educational support to TESA, a Tanzanian NGO established by the Canadian alumni of the Karimjee Secondary School in Tanga. 
MINISTER for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr William Lukuvi receives an ignitions keys from Karimjee Rivanjee Foundation Chairman, Mr Hatim Karimjee in Dar es Salaam August 30, 2017 for Idodi Health Centre based in Iringa region. The brand new ambulance worth 106/-m to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. 
Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, William Lukuvi tests the brand new ambulance worth 106/-m in Dar es Salaam yesterday, after receiving it from Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim Karimjee (left) for Idodi Health Centre based in Iringa region. The vehicle is meant to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. (Photos by Robert Okanda)

Makataa ya wakimbizi wa Burundi kuondoka Tanzania yakamilika

Serikali za Tanzania na Burundi pamoja na shirika la umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR leo watafanya mkutano wa pamoja kuhusiana na kurudishwa kwa wakimbizi wa Burundi waliojiandikisha kurudi kwao kwa hiari.
Pia leo ndio siku ya mwisho ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba aliitoa juu ya utekelezwaji wa zoezi hilo la kuwarudisha wakimbizi hao wa Burundi nyumbani kwao.

TMA YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI UANDISHI WA HABARI ZA HALI YA HEWA



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi. 

Alisema wanahabari inabidi wazielewe vizuri, kuzichambua na kuwafikishia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kiusahihi wananchi jambo ambalo litasaidia wananchi na sekta mbalimbali kujipanga kukabiliana na ama athari zitokanazo na utabiri wa hali ya hewa. 

"...Semina kama hizi kwanza zinasaidia wanahabari kuelewa masuala mbalimbali yatokanayo na taarifa zetu za utabiri, kisha wao kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na taarifa zetu kupitia vyombo vyao mbalimbali vya habari. Kundi hili likielewa vizuri nao watakuwa mabalozi wazuri kufikisha ujumbe kupitia kalamu zao," alisema Dk Agnes Kijazi. 

Aidha pamoja na mafunzo hayo, TMA pia ilipokea mrejesho na ushauri kutoka kwa wanahabari ili kuboresha zaidi namna ya utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa umma. 


Picha ya pamoja ya washiriki wa semina kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa.

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YAPUNGUA NCHINI, DR. ZEKENG


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (UNAIDS), Bw. Dr. Leo Zekeng ofisini kwake jijini Dar Es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Zekeng alisifu jitihada zinazofanywa na Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ambazo zimesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 25 na pia idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya ukimwi imepungua kwa kiasi kikubwa. Dkt. Zekeng alisema kuwa kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bi Michel Sidibe anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini mwezi Oktoba 2017 .



Dkt. Zekeng akionesha takwimu zilizopo katika ripoti ya UNAIDS zinazoonesha namna maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yalivyopungua nchini Tanzania. 



Mazungumzo yanaendelea 



Mhe. Naibu Waziri akiagana na Dkt. Zekeng baada ya kukamilisha mazungumzo yao 



Picha ya pamoja 

WASANII NGULI NCHINI KUPIMANA MABAVU DIMBA CONCERT TRAVELNTINE MAGOMENI


 Meneja Tukio wa Tamasha la Dimba Concert , Mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamasha litakalo wakutanisha Wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini na bendi ya Msondo Ngoma katika ukumbi wa Traventine September 2 mwaka huu kwa kiingilio cha shilingi 10,000 na 20,000 kwa VIP.
 Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Tamasha la Dimba Concert , Jimmy Chika akifafnua namna bendi hizo zitkavyotoa burudani kwa mashabiki na wadau wa Muziki wa dansi watakaofika katika ukumbi wa traventine siku ya Jumamosi
 Msanii wa Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Husein Jumbe akiwatoa hofu Mashabiki wake kuwa muziki wao bado upo juu
 Mwanamuziki wa Mkongwe wa Double M Sound ,  Mwinyjuma Muumini akijigamba kwa tambo kuwa siku hiyo patachimbika kwa hiyo mashabiki wote wasikose kuhudhuria Tamasha hilo
 Mpiga gitaa la solo wa siku nyingi , Adolf Mbinga akionesha namna atakavyocharaza nyuzi siku ya Tamasha la Dimba Concert siku ya jumamosi
 Mwanamuziki Juma Kakere akieleza namna watakavyoweza kukonga nyoyo za Mashabiki kupitia nyimbo zake kadhaa ambazo ziliweza kutamba
 Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akieleza namna atakavyoweza kutoa burudani kwa wadau wa muziki wa Dansi na Mashabiki watakaofika siku hiyo
 Wanamuziki wakongwe wakiwa katika mazoezi yao wakionyesha namna watakavyoimba siku ya Dimba Concert  siku ya Jumamosi
 Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akiimba mbele ya waandishi wa habari namna atakavyofanya siku ya Dimba Concert itakayofanyika Sept 2 mwka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni

Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

Wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini wametambiana kuoneshana uwezo wa kuimba siku ya Tamasha la Dimba Concert litakalofanyika katika ukumbi wa Traventine Magomeni Septemba 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja tukio tamasha la  Dimba Concert,Mwani Nyangasa amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa  Taifa muziki bendi kupambana na wanamuziki nguli wa Bendi ya Msondo ngoma.

“ Dhumuni la tamasha hili ni  kuendeleza muziki wa dansi hapa  nchini  kwa kutumia wasanii hawa wakongwe ili waweze kuonesha vijana,wapenzi na wadau kuwa muziki huu bado upo hai.” Amesema  Nyangasa.

 Nae msanii nguli nchini Hussen Jumbe ametanabaisha kuwa wadau na mashabiki wa muziki huo wafike kwa wingi siku hiyo pale Traveltine  septemba 2 mwaka huu ili kupata radha halisi ya muziki wa dansi.

Kwa upande wake  raisi wa vijana  sauti ya simba Nyoshi El Saadat, amewaomba mashabiki wa muziki huo kufika  kwenye tamasha hilo  na kuwaahidi kutowaangusha na kuwapa burudani ya kukata na shoka.

MTUHUMIWA WA IPTL SETHI ADAI ANA PUTO TUMBONI LISIPOPATIWA MATIBABU STAHIKI LINAWEZA KUPASUKA.


Bilionea wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Indeprndent Power Tanzania Limited(IPTL), Harbinder Sethi.
 
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
WAKILI wa utetezi, Joseph Makandege  ameiomba Mahakama itoe amri mshtakiwa Habinder Sethi akatibiwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa sababu amewekewa puto ('Balloon') tumboni ambapo asipopata Huduma stahiki linaweza kupasuka na kumpelekea kifo.

Makandege amedai  hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai kuwa mapema, mahakama ilitoa amri mshtakiwa huyo apelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili lakini ba baada ya kuwasiliana na mteja wao walibaini Magereza walimpeleka Amana badala ya Muhimbili kinyume na amri ya mahakama.

Makandege aliiomba mahakama  mshtakiwa apelekwe Muhimbili kuhakikisha afya yake inatengamaa na hatimaye aweze kuhudhuria mashtaka yake,

Amedai mahakama ya iliamuru  mshtakiwa huyo apelekwe  Muhimbili baada ya kuzingatia kuwa anaupasuaji ambao ulipelekea  kuwekewa puto(balloon) tumbo lake.

Ameongeza taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa hali  hiyo ya mshtakiwa isipohudiumiwa ipasavyo inaweza kupelekea kifo na kudai,  Muhimbili ndiyo hospitali ya  juu ya serikali nchini ambayo inategemewa kwa kuwa na wataalam na vifaa stahiki  vinavyoweza kumtibu Sethi.

Alidai awali mahakama ilitoa amri bila  kumung'unya maneno kuwa Sethi apelekwe Muhimbili lakini magereza wakampeleka Amana huvyo in wazi amri ya mahakama  haijatekelezwa hadi leo.

"Naiomba Mahakama itoe amri rasmi mshtakiwa Sethi apelekwe hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu" ameomba Mwakandege

Wakili Wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alipinga vikali hoja ya kuwa amri ya mahakama imekiukwa na kudai magereza ndiyo wanakaa na watuhumiwa na kwa mara ya kwanza wao ndiyo wanamuangalia mgonjwa, na kwa tatizo la Sethi
Licha ya kumpeleka Amana, walimpelekea pia mtaalam Dk Wilson kutoka hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Baaada ya kusikiliza hoja zote hizo, Hakimu Shaidi amesisitiza na  kuamuru mshtakiwa Sethi apelekwe Muhimbili kwa ajili ya matibabu

Naye mshtakiwa James Rugemalira ameiomba mahakama apatiwe nafasi ya kuonana na mawakili wake ambao wako zaidi ya 10 kwani kati ya wote hao, mawakili wawili tu ndio wanakibali cha kumuona.

 kesi imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu.

Katika kesi hiyo, washtakiwa Sethi na RugemLila wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la utakatishaji Wa fedha USD 22,198,545 na bilioni 309,461,300,158.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI NCHINI KUFANYIKA MKOANI DODOMA

 Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akionesha kwa waandishi wa habari picha yenye mashine ya kushindilia barabara ambayo imegunduliwa na wahandisi wa hapa nchini na kupewa jina la Magufuli One, kulia ni Msajili Msaidizi wa bodi hiyo, Mhandisi Benedict Mukama .
Msajili Msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Benedict Mukama  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba, kushoto ni Kaimu Msajili wa bodi hiyo, Mhandisi Patrick Barozi.
Picha na Eliphace Marwa - MAELEZO

WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA UFANISI

Na Mwandishi Maalum

31/08/2017 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma, kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili epukana na malalamiko yanayoweza kujitokeza.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Prof. Janabi pia aliwahimiza wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuendelea kutunza vizuri kumbukumbu mbalimbali zikiwemo za wagonjwa na utendaji wa kazi zao za kila siku ili pale zitakapohitajika zipatikane kwa haraka.

“Mjitahidi kujaza fomu ya wazi ya mapitio na upimaji utendaji kazi (OPRAS) kwa wakati ili kusiwe na malalamiko ya upandaji wa vyeo kwani ujazaji wa fomu hizo ndiyo unaowezesha mfanyakazi kupimwa utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mzima”, alihimiza Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Godfrey Tamba aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zao katika mazingira bora.

Tamba alisisitiza, “Wafanyakazi wenzangu tunaodai haki zetu tukumbuke kutimiza wajibu wetu wa kazi kwa wakati, kwani uongozi wa TUGHE hautawatetea watu ambao hawatimizi wajibu wao ipasavyo”.

Hiki ni kikao cha pili cha wafanyakazi wote kufanyika tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

MAHAKAMA YAKATAA KUPOKEA KIELELEZO CHA USHAHIDI KESI YA WEMA.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo imekataa  kupokea msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka kama vielelezo vya ushahidi dhidi ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya imayomkabili Wema Sepetu na wenzake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro.

Akitoa uamuzi wake amesema anakubaliana na hoja zilizotolewa  na upande wa mashtaka kwamba msokoto wa bangi na vipisi hivyo vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na wafuasi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati wakisubiri kusomewa Mashtaka yanayomkabili ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na Wakili wake Peter Kibatara  wakiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza mashtaka yanayo mkabili ya kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Wakili Peter Kibatara na Kushoto ni Mama wa Wema Sepetu.

 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa nche ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayo Mkabiri.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu  akiwa na wakili wake Peter Kibatara wakiwa nje ya Mahakama ja Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MWIGULU AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI UREJESHAJI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI WALIO TAYARI KUREJEA NCHINI KWAO


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi, ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akipitia nyaraka mbalimbali wakatiKikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,Harrison mseke.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(watano kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, (wasita kulia), na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.