Thursday, August 31

MTUHUMIWA WA IPTL SETHI ADAI ANA PUTO TUMBONI LISIPOPATIWA MATIBABU STAHIKI LINAWEZA KUPASUKA.


Bilionea wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Indeprndent Power Tanzania Limited(IPTL), Harbinder Sethi.
 
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
WAKILI wa utetezi, Joseph Makandege  ameiomba Mahakama itoe amri mshtakiwa Habinder Sethi akatibiwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa sababu amewekewa puto ('Balloon') tumboni ambapo asipopata Huduma stahiki linaweza kupasuka na kumpelekea kifo.

Makandege amedai  hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai kuwa mapema, mahakama ilitoa amri mshtakiwa huyo apelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili lakini ba baada ya kuwasiliana na mteja wao walibaini Magereza walimpeleka Amana badala ya Muhimbili kinyume na amri ya mahakama.

Makandege aliiomba mahakama  mshtakiwa apelekwe Muhimbili kuhakikisha afya yake inatengamaa na hatimaye aweze kuhudhuria mashtaka yake,

Amedai mahakama ya iliamuru  mshtakiwa huyo apelekwe  Muhimbili baada ya kuzingatia kuwa anaupasuaji ambao ulipelekea  kuwekewa puto(balloon) tumbo lake.

Ameongeza taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa hali  hiyo ya mshtakiwa isipohudiumiwa ipasavyo inaweza kupelekea kifo na kudai,  Muhimbili ndiyo hospitali ya  juu ya serikali nchini ambayo inategemewa kwa kuwa na wataalam na vifaa stahiki  vinavyoweza kumtibu Sethi.

Alidai awali mahakama ilitoa amri bila  kumung'unya maneno kuwa Sethi apelekwe Muhimbili lakini magereza wakampeleka Amana huvyo in wazi amri ya mahakama  haijatekelezwa hadi leo.

"Naiomba Mahakama itoe amri rasmi mshtakiwa Sethi apelekwe hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu" ameomba Mwakandege

Wakili Wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alipinga vikali hoja ya kuwa amri ya mahakama imekiukwa na kudai magereza ndiyo wanakaa na watuhumiwa na kwa mara ya kwanza wao ndiyo wanamuangalia mgonjwa, na kwa tatizo la Sethi
Licha ya kumpeleka Amana, walimpelekea pia mtaalam Dk Wilson kutoka hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Baaada ya kusikiliza hoja zote hizo, Hakimu Shaidi amesisitiza na  kuamuru mshtakiwa Sethi apelekwe Muhimbili kwa ajili ya matibabu

Naye mshtakiwa James Rugemalira ameiomba mahakama apatiwe nafasi ya kuonana na mawakili wake ambao wako zaidi ya 10 kwani kati ya wote hao, mawakili wawili tu ndio wanakibali cha kumuona.

 kesi imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu.

Katika kesi hiyo, washtakiwa Sethi na RugemLila wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la utakatishaji Wa fedha USD 22,198,545 na bilioni 309,461,300,158.

No comments:

Post a Comment