Jumatatu 21 Agosti 2017 mamilioni ya Wamarekani watashuhudia moja ya tukio kubwa zaidi ya jua kupatwa na mwezi katika kipindi cha karibu miaka 100.
Kwa kawaida, jua hupatwa mara mbili hivi kila mwaka, na hilo hutokea njia inayofuatwa na Jua, Dunia na Mwezi huendana sambamba.
Hili hapa ni jedwali la kuonesha ni lini mataifa mbalimbali Afrika yatashuhudia jua likipatwa hivi akribuni.
Takwimu zimetoka kwa Shirika la Anga za Juu la Marekani.
Kupatwa kwa jua kikamilifu 21 Agosti
Jua litapatwa kikamilifu leo kuanzia maeneo ya kaskazini mashariki mwa Bahari ya Pasifiki kabla ya kuanza kuonekana ardhini katika Lincoln Beach, Oregon mwendo wa saa 10:16 saa za huko (18:16 BST/Saa mbili jioni Afrika Mashariki).
Ukanda ambapo kutakuwa na giza totoro utapitia Amerika Kaskazini kwa dakika 90 hivi na kupitia maeneo ya Oregon, Idaho, Wyoming, Nebraska, Missouri, Illinois, Kentucky, Tennessee, North Carolina, South Carolina na Georgia.
Majimbo mengine nchini Canada na mataifa mengine ya Amerika Kusini na Kati pia yatashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu.
Aidha, baadhi ya nchi za Afrika Magharibi na Ulaya magharibi pia zitashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu. Lakini nchini Uingereza, katika maeneo mengi, jua litazibwa asilimia 4 pekee mwendo wa saa 20:00 BST.
Jua hupatwa vipi?
Kupatwa kwa jua kunatokea wakati dunia, mwezi na jua vinapokaa kwenye mstari mmoja mnyoofu wakati mwezi unakuwa kati ya dunia na jua. Hali hiyo inapotokea huwa kunajengeka kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia.
Kivuli hicho hufunika sehemu tu ya uso wa dunia.
Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa jua kwa maeneo yaliyo mengi huwa kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.
Hili hutokea takriban mara moja kila mwezi, lakini kutokana na mwinambo wa njia inayofuatwa na mwezi huwa hili linatokea juu sana au chini sana kwenye mbingu kiasi kwamba huwa haliwezi kuziba mwanga wa jua.
Sehemu yenye giza zaidi hufahamika kama kivuli cha kati na hapa ndipo jua hupatwa kikamilifu.
Sehemu ya nje hufahamika kama kivuli cha kando, ambapo jua huwa mwanga wake umezibwa kiasi tu. Hili husababisha kupatwa kwa jua kisehemu.
Kupatwa kwa jua kipete ni hali inayotokea ambapo mwezi huzuia mwanga wa jua kufika kwenye dunia kwa vile huweka duara la kivuli cha mwezi kwenye dunia na hivyo mwanga wa jua huonekana kama pete.
Aina hii ndiyo iliyoshuhudiwa nchini Tanzania tarehe 1 Septemba 2016 na katika baadhi ya maeneo ya bara la Afrika.
Taifa | Tarehe | Aina ya kupatwa kwa jua |
Algeria | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Angola | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Benin | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Botswana | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Burkina Faso | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Burundi | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Capo Verde | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Cameroon | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Jamhuri ya Afrika ya Kati | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Chad | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Comoros | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Congo (DR) | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Congo | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Cote d'Ivoire | 12/14/2020 | Kupatwa kwa jua kikamilifu |
Djibouti | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Egypt | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Equatorial Guinea | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Eritrea | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Ethiopia | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Gabon | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Gambia, The | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Ghana | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Guinea | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Guinea-Bissau | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Kenya | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Liberia | 2026-12-08T00:00:00.000 | Kupatwa kwa jua kikamilifu |
Libya | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Madagascar | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Malawi | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Mali | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Mauritania | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Mauritius | 2/17/2026 | Kupatwa kwa jua kipete |
Morocco | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Msumbiji | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Namibia | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Niger | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Nigeria | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Rwanda | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Senegal | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Seychelles | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Sierra Leone | 10/14/2023 | Kupatwa kwa jua kipete |
Somalia | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Afrika Kusini | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Sudan Kusini | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Sudan | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Swaziland | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Tanzania | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Tunisia | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |
Uganda | 12/26/2019 | Kupatwa kwa jua kipete |
Zimbabwe | 6/21/2020 | Kupatwa kwa jua kipete |