Monday, August 21

Jua litapatwa lini tena nchini mwako?

Solar eclipse calculator

Jumatatu 21 Agosti 2017 mamilioni ya Wamarekani watashuhudia moja ya tukio kubwa zaidi ya jua kupatwa na mwezi katika kipindi cha karibu miaka 100.
Kwa kawaida, jua hupatwa mara mbili hivi kila mwaka, na hilo hutokea njia inayofuatwa na Jua, Dunia na Mwezi huendana sambamba.
Hili hapa ni jedwali la kuonesha ni lini mataifa mbalimbali Afrika yatashuhudia jua likipatwa hivi akribuni.
Takwimu zimetoka kwa Shirika la Anga za Juu la Marekani.
Kupatwa kwa jua kikamilifu 21 Agosti
Jua litapatwa kikamilifu leo kuanzia maeneo ya kaskazini mashariki mwa Bahari ya Pasifiki kabla ya kuanza kuonekana ardhini katika Lincoln Beach, Oregon mwendo wa saa 10:16 saa za huko (18:16 BST/Saa mbili jioni Afrika Mashariki).
Ukanda ambapo kutakuwa na giza totoro utapitia Amerika Kaskazini kwa dakika 90 hivi na kupitia maeneo ya Oregon, Idaho, Wyoming, Nebraska, Missouri, Illinois, Kentucky, Tennessee, North Carolina, South Carolina na Georgia.
Majimbo mengine nchini Canada na mataifa mengine ya Amerika Kusini na Kati pia yatashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu.
Aidha, baadhi ya nchi za Afrika Magharibi na Ulaya magharibi pia zitashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu. Lakini nchini Uingereza, katika maeneo mengi, jua litazibwa asilimia 4 pekee mwendo wa saa 20:00 BST.
Kupatwa kwa jua

Jua hupatwa vipi?

Kupatwa kwa jua kunatokea wakati dunia, mwezi na jua vinapokaa kwenye mstari mmoja mnyoofu wakati mwezi unakuwa kati ya dunia na jua. Hali hiyo inapotokea huwa kunajengeka kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia.
Kivuli hicho hufunika sehemu tu ya uso wa dunia.
Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa jua kwa maeneo yaliyo mengi huwa kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.
Hili hutokea takriban mara moja kila mwezi, lakini kutokana na mwinambo wa njia inayofuatwa na mwezi huwa hili linatokea juu sana au chini sana kwenye mbingu kiasi kwamba huwa haliwezi kuziba mwanga wa jua.
Kupatwa kwa jua
Sehemu yenye giza zaidi hufahamika kama kivuli cha kati na hapa ndipo jua hupatwa kikamilifu.
Sehemu ya nje hufahamika kama kivuli cha kando, ambapo jua huwa mwanga wake umezibwa kiasi tu. Hili husababisha kupatwa kwa jua kisehemu.
Kupatwa kwa jua kipete ni hali inayotokea ambapo mwezi huzuia mwanga wa jua kufika kwenye dunia kwa vile huweka duara la kivuli cha mwezi kwenye dunia na hivyo mwanga wa jua huonekana kama pete.
Aina hii ndiyo iliyoshuhudiwa nchini Tanzania tarehe 1 Septemba 2016 na katika baadhi ya maeneo ya bara la Afrika.
TaifaTareheAina ya kupatwa kwa jua
Algeria6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Angola6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Benin6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Botswana6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Burkina Faso6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Burundi6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Capo Verde10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Cameroon6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Jamhuri ya Afrika ya Kati6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Chad6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Comoros6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Congo (DR)12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Congo6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Cote d'Ivoire12/14/2020Kupatwa kwa jua kikamilifu
Djibouti12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Egypt12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Equatorial Guinea6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Eritrea12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Ethiopia12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Gabon6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Gambia, The10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Ghana6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Guinea10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Guinea-Bissau10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Kenya12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Liberia2026-12-08T00:00:00.000Kupatwa kwa jua kikamilifu
Libya6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Madagascar6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Malawi6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Mali6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Mauritania6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Mauritius2/17/2026Kupatwa kwa jua kipete
Morocco6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Msumbiji6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Namibia6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Niger6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Nigeria6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Rwanda6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Senegal10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Seychelles6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Sierra Leone10/14/2023Kupatwa kwa jua kipete
Somalia12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Afrika Kusini6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Sudan Kusini12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Sudan12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Swaziland6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Tanzania12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Tunisia6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete
Uganda12/26/2019Kupatwa kwa jua kipete
Zimbabwe6/21/2020Kupatwa kwa jua kipete

No comments:

Post a Comment