Saturday, July 8

Nahodha wa zamani wa Everton atua Dar

Dar es Salaam. Mchezaji wa zamani wa Everton, Leon Osman ametua nchini leo na ataendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi na wachambuzi wa soka Julai 12 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ujio wa Osman ni kufungua mlango kwa Everton itakayotua nchini wiki ijayo tayari kwa mechi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Alhamis ijayo katika fainali ya Sportpesa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba  alisema msafara wa wachezaji wa Everton utatua nchini  Julai 12  na mchezaji huyo wa zamani ametangulia ili kufanya ziara ya kitalii hapa nchini.
"Mchezaji huyu wa zamani wa Everton ametangulia kwa  mambo makuu mawili, ambayo ni kufanya ziara ya kitalii nchini  atatembela mbuga za wanyama ya Ngorongoro siku ya Jumatatu ili kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini pia ataendesha semina kwa waandishi na wachambuzi wa soka 
Osman alisema hii ni mara ya pili kuja Tanzania na amefurahi  kuwa atapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii.

Abiria waomba kuruhusiwa kusafiri usiku


Morogoro. Abiria wa mabasi yanayotoka mikoa ya bara yanayopita mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam wameiomba serikali iruhusu mabasi ya abiria kusafiri baada ya saa sita usiku hasa katika maeneo ambayo sio hatarishi kwa usafiri wa wakati huo.
Abiria hao walitoa ombi hilo jana Ijumaa wakati wakizungumza na Mwananchi katika kituo cha mabasi Msamvu.
Wamelalamikia kitendo cha kuzuiwa kuendelea na safari hata kabla ya saa sita usiku na kubainisha kuwa kinasababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wengi.
Kwa muda mrefu sasa serikali imepiga marufuku mabasi ya abiria kuendelea na safari baada ya saa sita usiku hivyo baadhi ya mabasi yanayotoka mkoani Mwanza na Mbeya kuelekea Dar es Salaam yanalazimika kulala mkoani Morogoro.
Abiria Shiraji Nyanda alisema kulala njiani kunawaongezea wasafiri gharama na wale wenye watoto wanapata usumbufu zaidi.
"Nia ya serikali ni njema ya kuhakikisha usalama wa watu wake lakini kwa barabara ya Dar-Moro ni salama sana… wangeruhusu tu mabasi yaendelee na safari. Lakini kibaya zaidi tunazuiliwa hapa kabla hata ya hiyo saa sita," alisema Nyanda.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni zilizopo, mabasi ya abiria hayaruhusiwi kusafiri baada ya saa nne usiku.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jane Arnold, ambaye alikua anasafiri na watoto, alisema kulala kwenye basi na watoto kumemsababishia usumbufu na kumuongezea gharama za safari.
Akizungumzia malalamiko hayo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Morogoro, Victor Ayo, alisema mabasi hayo yanazuiliwa Morogoro sit u kwa kuogopa kutenkwa, bali pia kwa usalama wa abiria na vyombo hivyo vya usafiri.
Akifafanua, alibainisha kuwa mabasi yanazuiliwa kusafiri usiku ili pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uchovu wa dereva.
Alisema kwa wakati huo dereva anakuwa amechoka baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu na barabara hiyo inakuwa na msongamano wa malori.
"Niwashauri tu abiria wawe wavumilivu katika hili kwani linafanyika kulinda usalama wao," alisema.
Ofisa huyo pia aliwataka madereva kutii sheria za usalama barabarani ili kulinda usalama wao na usalama wa watumiaji wengine wa barabara.

MAONESHO YA SABASABA 2017;FINCA MICROFINANCE BANK WANG'ARA KATIKA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUHUDUMIA WATEJA




Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wakala wa Finca Express Grace Kimaro akiwa anamsajili mteja mpya wa Finca kwa kutumia Tablet katika banda lao mapema jana katika maonesho ya sabasaba.Jijini Dar es salaam. 
Mfanyakazi wa FINCA Microfinance Bank Beatrice kimaro akimpiga picha katika kumsajili mteja mpya wa FINCA kwa kutumia mfumo wa kisasa ambao hutumia Tablet mapema jana katika maonesho ya sabasaba ,Jijini Dar es salaam. 
Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 
Wafanyakazi wa Finca Microfinance Bank wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda la FINCA kufungua akaunti Mapema jana katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Wateja waliofika katika banda la Finca Microfinance Bank wakipata maelezo jinsi ya kufungua akaunti na huduma za mikop zinazotolewa na Benki,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Wana Chadema 51 mbaroni Chato


Chato. Viongozi na wanachama 51 wa Chadema waliokamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani wilayani Chato wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Miongoni mwa waliotiwa mbaroni wanaoendelea kusota mahabusu ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Fabian Mahenge na Katibu wake, Sudi Kanganyala.
Mwenyekiti wa Serikali kijiji cha Mkuyuni, Anaclet Twegosora, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Chato, amewataja viongozi wengine wanaoshikiliwa kuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoani Geita, Vitus Makange na Neema Chozaire ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa.
Wengine ni Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Chato, Uhuru Selemani, Katibu wake Mangesai Rudonya na diwani mstaafu kata ya Muganza, Marko Maduka.
Kama ilivyokuwa jana, hakuna kiongozi wa Jeshi la Polisi anayekuwa tayari kulizungumzia suala hili.
Wakati Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, Alex Mkama, ambaye tukio hilo linaendelea wilayani kwake akisema hawezi kulizungumzia, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, amesema yuko likizo na kuelekeza atafutwe kaimu wake Allan Bukumbi ambaye tangu jana hapokei simu yake ya kiganjani wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno anaotumiwa.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Ansbert Ngurumo, amesema kutawanywa kwa mabomu ya machozi na kukamatwa kwa viongozi na wanachama hao ambao walikuwa katika mkutano wa ndani ni kinyume cha sheria kwa sababu vikao vya ndani havihitaji kutoa taarifa wala kibali cha polisi kwa mujibu wa sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1995.

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAFURIKA KATIKA BANDA LA UBER NA KUJIUNGA NA HUDUMA


Wafanyakazi kampuni ya Uber Godfrey Mabula na Ibrahimu Kunguya wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika katika banda kujua jinsi Program ya Uber inayorahisisha usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu pia wateja wote waliopakua Program hiyo walipata punguzo la kiasi cha 8200Tsh kwa safari yao ya kwanza.Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 
Mfanyakazi wa Uber Ibrahim Kunguya akimsaidia mteja jinsi ya kutumia Program ya uber ambayo imekuwa msaada kwa wakazi wa jiji la Dar kusaidia kurahisisha usafiri kwa njia ya kiteknolojia ,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar Es Salaam. 
Balozi wa Uber akimsaidia mteja jinsi ya kupakua na kutumia program ya Uber katika banda lao katiika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar es salaam. 
Wateja waliofika katika banda la uber wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Uber Jinsi ya kupakua na kutumia Progamu ya Uber ambayo inarahisisha usafiri na kwa gharama nafuu,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakipata maelekezo jini ya kujiunga na programu ya Uber katika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar Es salaam. 
Bango linaloonyesha jinis ya kuipata program ya Uber katika APP store na Google play na kutumia kutumia usafiri kwa bei nafuu na kwa kisasa zaidi . 
Balozi wa Uber akitoa maelekezo kwa mteja aliyefika katika banda lao ambapo pia wateja walijipatia punguzo la kiasi cha 8200 Tsh mara baada ya kupakua na kutumia program ya uber katika kuagiza usafiri kwa bei nafuu na kwa teknolojia ya kisasa mapema jana katika maonesho ya saba saba. 

Huduma zikiendelea kutolewa katika banda la Uber mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 

UJENZI WA DARAJA LA KAVUU UMEKAMILIKA


Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.

“Serikali iliona kero kubwa wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari yatakayozidisha Tani 36.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua ujenzi wa Nyumba za Viongozi Mkoani humo na kuuagiza Wakala wa Majengo nchini (TBA), kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

“Serikali imeshatoa fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi, ujenzi huu ulisimama kwa takribani miezi minne kwa sasa hakuna sababu ya ujenzi kusuasua wakati fedha zipo, ninakuhakikishia Mkuu wa Wilaya nyumba hizi zitakamilika kwa wakati ili zianze kutumika,” alisisitiza Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Eng. Nyonyani amekagua ujenzi wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula. 

Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto), akikagua ujenzi wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini (TBA) Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel Kassanda.


Meneja Wa Wakala Wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati Naibu Waziri huyo alipokagua, Mkoani Katavi.


Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kukagua Daraja la Kavuu ambalo ujenzi wake umekamilika na linatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu..

 Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na wakazi wa kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kuongea nao.
 Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akiongea na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare (Kulia), Wakati Waziri Ngonyani alipotembelea Jimboni kwake mwishoni mwa wiki.
 Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Muonekano wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula. 

WAZIRI MAUDLINE WA ZANZIBAR AVUTIWA NA KAZI ZA JKT MAONESHO YA SABASABA


 Kaimu Afisa Habari wa Jeshi La Kujenga Taifa (JKT),Kanal Separatus Lubinga  akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
 SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba

 CPL.Maximilian Joseph wa SUMA JKT Guard  akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
  SSGT. Faustine Mabata kutoka Suma JKT Furniture akitoa maelezo kwa Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
 Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico  akiangalia namna ya ufugaji Samaki kwa kutumia mfumo Raisi alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba
Waziri wa kazi, Uwezeshaji, Wazee ,Vijana na Maendeleo kwa watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maudline Cyrus Castico alipotembelea Maonesho ya 41 ya Sabasaba

Taifa Stars waifunga Lesotho kushika nafasi ya tatu Cosafa

Himidi Mao

Shujaa wa Taifa Stars leo amekuwa golikipa Said Mohammed Mduda aliyepangua penalti ya Nahodha wa Lesotho
Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA Castle baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku huu Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Shujaa wa Taifa Stars leo amekuwa golikipa Said Mohammed Mduda aliyepangua penalti ya Nahodha wa Lesotho, Thapelo Mokhehle baada ya Sera Motebang kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wake na kurudi uwanjani.
Waliofunga penalti za Lesotho ni Hlompho Kalake na Tsoanelo Koetle wakati Shiza Kichuya aligongesha mwamba wa juu penalti ya kwanza ya Tanzania, kabla ya Nahodha Himid Mao,Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi kumtungua kipa wa Mamba Samuel Ketsekile kuipatia Taifa Stars ushindi mzuri wa 4-2.
Ushindi unakuja siku 25 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 Juni 10, mwaka huu katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Romeo Kasengele wa Zambia, aliyesaidiwa na washika vibendera Thomas Kusosa wa Zimbabwe na Helder de Carvalho wa Angola, ndani ya dakika 90 timu hizo zilishambuliana kwa zamu, Lesotho wakitawala zaidi kipindi cha kwanza na cha pili Taifa Stars wakazinduka.
Kutoka na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola 8,300.
Fainali ya COSAFA Castle 2017 itachezwa Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg baina ya majirani, Zambia na Zimbabwe na bingwa atapata dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000.