Saturday, July 8

Nahodha wa zamani wa Everton atua Dar

Dar es Salaam. Mchezaji wa zamani wa Everton, Leon Osman ametua nchini leo na ataendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi na wachambuzi wa soka Julai 12 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ujio wa Osman ni kufungua mlango kwa Everton itakayotua nchini wiki ijayo tayari kwa mechi dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Alhamis ijayo katika fainali ya Sportpesa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni ya Sportpesa, Abbas Tarimba  alisema msafara wa wachezaji wa Everton utatua nchini  Julai 12  na mchezaji huyo wa zamani ametangulia ili kufanya ziara ya kitalii hapa nchini.
"Mchezaji huyu wa zamani wa Everton ametangulia kwa  mambo makuu mawili, ambayo ni kufanya ziara ya kitalii nchini  atatembela mbuga za wanyama ya Ngorongoro siku ya Jumatatu ili kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini pia ataendesha semina kwa waandishi na wachambuzi wa soka 
Osman alisema hii ni mara ya pili kuja Tanzania na amefurahi  kuwa atapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii.

No comments:

Post a Comment