Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye
viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja
hivyo .
Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha,
Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu
kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani
kutaharibu upelelezi.
Kamanda Sabas amedai
kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza
wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye
viwanja hivyo.
Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu
juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai
ya kuomboleza ..
Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo
walikaidi agizo hilo na kuanza kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi
wa CHADEMA , hali iliyoleta mvutano kati
ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi
wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa
kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi
kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika
kadhaa mabumu yalianza kusikika.
Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo
uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu,
Halima Mdee...