Wednesday, December 21

Maafa Dar 5

Maafa Dar 4

Nyumba zachomwa moto kwa imani za kishirikina. Na Fredy Bakalemwa, Mbeya.

Wakazi wa mtaa wa Igoma A kata ya Isanga jijini Mbeya wamezizoma moto nyumba mbili, moja ikiwa ya mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Juma Kahawa.

Nyumba nyingine iliyoteketezwa kwa moto na watu walioamua kujichukuliwa sheria mkononi ni ya Bwana Herman Tonji naye ni mkazi wa mtaa huo.

Imedaiwa na baadhi ya wakazi wa mtaa huo kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na kuwatuhumu watu hao kuwa ni washirikiana kwa madai kuwa baadhi ya watoto katika mtaa huo wamepotea na kukutwa wakiwa wamekufa katika mazingira tatanishi.

Tukio la Jumatano jioni katika mtaa wa Igoma kata ya Isanga lilinaswa na kamera ya Star Tv ambapo umati wa watu walitoka mkutanoni baada ya kushindwa kupata mwafaka hasira zikawaelekeza kujichukulia sheria mkononi.

Wakati tukio likiendelea kikosi cha zima moto kilifika eneo la tukio ili kuokoamalizilizokuwa zimesalia lakini hata hivyo sehemu kubwa yamalizilikuwa zimeteketea.

Kwa kuwa watekelezaji wa hatua hiyo walitambua kuwa wanavunja sharia, baada ya kuona askari polisi wakiwa na silaha hakuna aliyesalia bali walihamia katika nyumba nyingine ya Bwana Herman Tonji.

Polisi walipofika wakachukua hatua za kuokoa baadhi yamalikabla ya kuteketea, lakini siyo kila kitu kiliguswa.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ACP Advocate Nyombi alitoa tamko, kuthibitisha tukiohilokwa kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

Mwisho.

Mafuriko yaleta maafa Dar • Watu kumi wahofiwa kufa, 2,000 wakosa makazi

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali na radi iliyonyesha usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam, imesababisha vifo vya watu zaidi ya kumi pamoja na kusababisha uharibifu wa miundombinu, huku zaidi ya watu 2,000 wakikosa makazi. Miongoni mwa maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo kwa kiasi kikubwa ni Kigogo Mburahati, Ubungo Msewe, Bonde la Mkwajuni, Bonde la Msimbazi na mengine ambako nyumba za watu zilizama na kusababisha baadhi ya wananchi kutojulikana waliko. Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, mmoja wa wahanga hao kutoka eneo la Kigogo Mburahati, Grace Anthony alisema watoto wadogo wawili wanasaidikiwa kufa katika eneo hilo baada ya kusombwa na maji wakati wakiwa katika harakati za kujiokoa. Mzee mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 anadaiwa kufa maji baada ya mwili wake kukutwa katika Mto Msewe eneo la Ubungo Msewe, wakati mtoto mwingine wa miaka minane anadaiwa kufariki dunia katika eneo la Kiwalani, baada ya kushika waya wa umeme ulioanguka kutokana na mvua hizo. Aliyataja maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo ni kutoka eneo la Festini hadi kituo cha Saluni, yote yakiwa Kigogo Mburahati ambako baadhi ya nyumba zilizamishwa chini huku watu wakihangaika kuokoa maisha yao. “Maji yametapakaa eneo lote kama unavyoona na baadhi ya nyumba zimeezuliwa, mali zetu zimesombwa pamoja na gari za watu, hapa hatuna jinsi, kilichopo kwa sasa ni kuiomba serikali itusaidie,” alisema Anthony. Alisema chanzo cha mafuriko hayo ni mkondo wa maji ya mvua yanayotoka maeneo ya Mabibo na Kigogo kushindwa kupita katika daraja la Kigogo, hali inayosababisha maji hayo kupwa na kusambaa ndani ya makazi ya watu. Aliyafananisha mafuriko hayo na gharika kwani awali liliwahi kutokea mwaka 1997 na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha yao. “Mafuriko ya leo ni ya pili kutokea, tukio kama hili tulikumbana nalo mwaka 1997 na chanzo kikubwa ni ufinyu wa daraja pamoja na msongamano wa kaya za watu hasa kwa wale wanaoishi mabondeni. “Awali mwaka huu mwezi Machi mafuriko yalitokea lakini yalisababisha kaya zilizokumbwa na mafuruko hayo kukosa mahali pa kuishi kutokana na maji kujaa ndani, huku baadhi ya kaya zikitakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi wa barabara sanjari na daraja,” alifafanua Anthony. Vyanzo vya uhakikika vililiambia Tanzania Daima Jumatano kwamba maeneo ya Bonde la Mkwajuni pia na Kigogo kuna nyumba zimezama, hivyo kusababisha baadhi ya watu kutoonekana. “Nyumba nyingi zimezama; watu wanahaha kwa kushindwa kujua la kufanya badala yake wengi wao wamelazimika kukaa juu ya mabati ya nyumba zao wakiwa na magodoro… suala hili limetokea katika eneo la Bonde la Mkwajuni na Kigogo,” kilisema chanzo hicho cha habari. Habari nyingine zinaeleza kwamba katika eneo la Magomeni Mwembechai nyumba zilijaa maji hadi eneo la dirishani, hivyo kuwalazimu wanaoishi kuzihama kwa muda. Kwa mujibu wa habari, hadi saa 7:19 mchana jana wananchi hao bado walikuwa hawajapatiwa msaada wowote zaidi ya kuhaha. Taarifa kutoka kwa mashuhuda zinapasha kwamba maafa mengine yametokea katika eneo la Kigogo kutokana na nyumba nyingi kujaa maji hivyo kuwakosesha wananchi wake mahala pa kuishi. Katika maeneo ya Mbagala, Wilaya ya Temeke iliripotiwa kwamba mvua hizo zilizoambatana na radi zimesababisha kupigwa shoti ya umeme hivyo kubomoka. Mvua hizo zilisababisha pia tafrani baada barabara nyingi kujaa maji na kusababisha misafara ya magari kukwama kwenye foleni kwa muda mrefu. Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kwa daladala kwa nyakati tofauti walisema kwamba mvua hizo zimewafanya washindwe kufika katika sehemu zao za kazi kwa wakati. Walisema kulikuwa na madimbwi ya maji katika barabara mbalimbali likiwamo eneo sugu la Akiba, hali iliyowafanya madereva kushindwa kupitisha magari yao katika hali ya kawaida. Mmoja wa abiria hao, Shaban Issa alisema ukiachilia mbali madimbwi ya maji, kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za barabarani uliofanywa na madereva walipofika kwenye makutano ya barabara kutokana na kutokuwepo askari wa kuongoza magari. Alisema kutokana na kutokuwepo askari wa kuongoza magari katika makutano hayo ya barabara kutokana na mvua hiyo, baadhi ya madereva walikuwa wakipitisha magari yao bila kutii taa za barabarani, hali iliyosababisha msongamano na kuzusha foleni zisizo za lazima. Naye Maggy Mdoe, alisema maeneo mengine yalioathirika na msongamano huo ni pamoja na Ubungo mataa, Usalama, Tazara, Morocco na Fire. “Tumechukua muda mrefu kwa sababu ya uzembe wa madereva kushindana kupita kwenye mataa kutokana na kujifanya wana haraka wakati hata hawajaruhusiwa na taa za upande wao,” alilalamika Mdoe. Alitoa wito kwa madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani, na si lazima kila mara wasimamiwe na mtu kwani huo si utaratibu mzuri. Mafuriko hayo pia yamewakosesha makazi baadhi ya wananchi wa eneo la Tabata Relini kutokana na nyumba pamoja na vyombo vyao kusombwa na maji. Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Alli Khatib aliliambia Tanzania Daima Jumatano kwamba mafuriko yanasababishwa na serikali kwa kutojenga miundombinu imara kwa ajili ya kuzuia majanaga ya mafuriko. Aliitaka serikali kuwatengenezea mkondo wa kupitisha maji ili kuweza kuzuia mafuriko hayo ambayo yanawafanya kukosa makazi ya kuishi. Alisema kuwa mvua iliyonyesha kwa siku moja imesababisha watu kukosa makazi, na kwamba kama ikinyesha kwa siku mbili serikali itegemee maafa makubwa kwa wananchi wanaoishi katika mikondo ya mifereji midogo. “Mvua hii imekosesha wananchi sehemu ya kukaa kutokana na nyumba kujaa maji ya mafuriko pia daraja la Ubungo Msewe kuzolewa na maji,” alisema Khatib. Mvua hizo zimesababisha pia mawasiliano kuharibika katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na watu waishio Kimara na Mbezi kushindwa kupita katika barabara yenye daraja hilo. Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan, amesema atachukua hatua za haraka kuimarisha miundombinu ya maeneo mbalimbali ili kukabiliana na hali ya mafuriko makubwa kama ilivyopata kutokea mwaka 1998 na jana kwenye maeneo ya Tandale kwa Mtogole, bonde la Kigogo na Magomeni. Azan ambaye alikuwa akitembelea maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hizo, alisema wakazi wa Tandale na maeneo yake, wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu kwani ndio chanzo cha mafuriko. “Suala hili la mafuriko kwa wakazi wa Jimbo la Kinondoni, lipatiwe ufumbuzi ikiwemo kujenga mitaro mikubwa maeneo korofi ya Tandale ili kuzuia ama kukabiliana na hali hiyo,” alisema Azan. Tanzania Daima lilikuwa kwenye eneo la tukio tangu alfajiri, ili shuhudia foleni kubwa kwa magari yaliyokuwa yakipita Barabara ya Shekilango, yakisubiri kupungua kwa maji. Katika eneo hilo gari aina ya Escudo lilisombwa na maji na kutumbukia mtoni huku baadhi ya fremu za muda za eneo la mto huo zikiwa zimejaa maji na zingine kuharibika kabisa. Kwa upande wa abiria waliokuwa wakitumia barabara ya Tandale, walikwama kupita baada ya maji kutanda barabarani. Aidha, katika hali ya kusikitisha, mtoto mchanga wa siku moja aliokotwa akielea kwenye maji na kuopolewa na askari wa Kikosi cha Zimamoto akiwa amekufa. Habari hii imeandaliwa na Hellen Ngoromera, Efracia Massawe, Shehe Semtawa, Chalila Kibuda na Andrew Chale.

Maafa Dar

Maafa Dar 2

Maafa Dar