Thursday, April 5

Maana ya matokeo Arumeru Mashariki by zittokabwe Matokeo ya Arumeru na kata za Mwanza, Songea na Mbeya ni mwanzo wa safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi. Mhe Mwenyekiti Freeman Mbowe na Mhe Joshua Nassari Mnamo tarehe 11 Machi mwaka huu 2012 nikiwa ndani ya ndege natokea Arumeru kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenda Kirumba Mwanza kuzindua kampeni za Udiwani katika kata ya Kirumba, niliandika makala kuhusu nini kitaamua mshindi katika uchaguzi ule. Nilianza makala yangu ile kwa kusema haya "Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu". Haya maneno ilikuwa ni nukuu ya sehemu ya hotuba niliyotoa wakati namkaribisha Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua rasmi kampeni zetu. Ardhi ilikuwa ajenda kubwa sana. Washindani wetu wa CCM wakaona hatari ya hoja ya Ardhi na kuanza kutoa ahadi mbalimbali za kumaliza kero ya Ardhi. Hawakuaminika. Wananchi walisema, hawa wamemaliza miaka 50 bila kutatua kero hii, watawezaje kupata suluhisho sasa. Wakakataa. Hawakuichagua CCM na badala yake wakamchagua kwa kura nyingi sana ndugu Joshua Nassari, kijana wa miaka 26 tu kuwa Mbunge wa Jimbo Lao. Katika makala ile nilieleza wazi kwamba "Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari. Sasa Nassari lazima aibebe ajenda Ardhi. Hana namna ni lazima awe sauti ya wananchi masikini waliofukarishwa na mfumo mbovu wa kugawa Ardhi ulioanzishwa wakati wa ukoloni na kuendelezwa chini ya Uongozi wa CCM. Ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi wa Arumeru ni ishara ya dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuongoza Taifa letu zinahesabika. Ukilinganisha nguvu ya rasilimali watu na fedha ambayo CCM waliiweka huko Meru kulinganisha na CHADEMA unaona dhahiri kabisa kuwa fedha sio kigezo cha kushinda uchaguzi. Wananchi sasa wanataka masuala Yao yashughulikiwe. Hii pia imejionyesha katika chaguzi za Madiwani. CCM imepoteza nusu ya viti vya Udiwani vilivyokuwa vinagombewa. Katanza Lizaboni Songea, Kiwira Mbeya na Kirumba Mwanza zote zimeenda CHADEMA. Kata ya Msambweni Tanga imeenda CUF. CCM walipata kata katika Wilaya ya Bagamoyo, Bariadi na Temeke. Pia walipata kata katika manispaa ya Dodoma. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa Madiwani ambao CCM imepoteza nusu ya viti vilivyokuwa vinagombewa toka mfumo wa vyama vingine uanze. Arumeru imekuwa jimbo la kwanza CCM kulipoteza kwa chama cha upinzani Tangu mwaka 1997 ambapo CCM walipoteza jimbo la Magu kwa chama cha UDP. Kwa CHADEMA hili ni jimbo la kwanza kulichukua kutoka CCM katika uchaguzi mdogo toka ianzishwe mwaka 1992. Itakumbukwa kwamba mwaka 2008 CHADEMA ilishinda jimbo la Tarime kwa kulirejesha maana kilikuwa linashikiliwa nacho. People's power Hivyo ni dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuwa madarakani zinahesabika. Ushindi wa Arumeru na Udiwani katika kata mbalimbali umeleta mageuzi makubwa ya kisaikolojia kwa wananchi kuliko hata ushindi wa Tarime. Ni wazi kabisa kuwa ushindi huu utafutiwa na mikutano wa kunadi chama katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Kusini na ile ya Magharibi ambapo CHADEMA haijafanya operesheni. Kushindwa kwa CCM Arumeru pia kutal eta mpasuko zaidi ndani ya CCM na kuunganisha nguvu za wanasiasa ndani ya CHADEMA. Wakati CCM itakuwa inanyoosheana vidole kutafuta mchawi na hata wengine kufurahia kushindwa kwao (wakiamini ni kushindwa mmoja wa mahasimu wao), CHADEMA itakuwa inashikana mikono na kuimarisha mshikamano ili hatimaye kuchukua Dola ifikapo mwaka 2015. Jambo moja la dhahiri unaliona Baada ya uchaguzi wa Arumeru. Sasa ukipanda Basi kutoka Moshi kwenda Arusha, utopita ngome ya Chadema tu. Moshi mjini, Hai, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini. Kwa waliomsoma Rais Museveni katika kitabu chake cha Sowing the Mustered seed, akitumia njia za Frelimo katika ukombozi, eneo hili sasa ni Liberated Zone. Ukanda uliokombolewa. Lengo langu ni kuonyesha kuwa hii ndio safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi.

Matokeo ya Arumeru na kata za Mwanza, Songea na Mbeya ni mwanzo wa safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi.

Mnamo tarehe 11 Machi mwaka huu 2012 nikiwa ndani ya ndege natokea Arumeru kuzindua kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenda Kirumba Mwanza kuzindua kampeni za Udiwani katika kata ya Kirumba, niliandika makala kuhusu nini kitaamua mshindi katika uchaguzi ule. Nilianza makala yangu ile kwa kusema haya
"Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu".

Haya maneno ilikuwa ni nukuu ya sehemu ya hotuba niliyotoa wakati namkaribisha Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua rasmi kampeni zetu.
Ardhi ilikuwa ajenda kubwa sana. Washindani wetu wa CCM wakaona hatari ya hoja ya Ardhi na kuanza kutoa ahadi mbalimbali za kumaliza kero ya Ardhi. Hawakuaminika. Wananchi walisema, hawa wamemaliza miaka 50 bila kutatua kero hii, watawezaje kupata suluhisho sasa. Wakakataa. Hawakuichagua CCM na badala yake wakamchagua kwa kura nyingi sana ndugu Joshua Nassari, kijana wa miaka 26 tu kuwa Mbunge wa Jimbo Lao. Katika makala ile nilieleza wazi kwamba
"Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari. Sasa Nassari lazima aibebe ajenda Ardhi. Hana namna ni lazima awe sauti ya wananchi masikini waliofukarishwa na mfumo mbovu wa kugawa Ardhi ulioanzishwa wakati wa ukoloni na kuendelezwa chini ya Uongozi wa CCM.
Ushindi wa CHADEMA katika uchaguzi wa Arumeru ni ishara ya dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuongoza Taifa letu zinahesabika. Ukilinganisha nguvu ya rasilimali watu na fedha ambayo CCM waliiweka huko Meru kulinganisha na CHADEMA unaona dhahiri kabisa kuwa fedha sio kigezo cha kushinda uchaguzi. Wananchi sasa wanataka masuala Yao yashughulikiwe. Hii pia imejionyesha katika chaguzi za Madiwani.

CCM imepoteza nusu ya viti vya Udiwani vilivyokuwa vinagombewa. Katanza Lizaboni Songea, Kiwira Mbeya na Kirumba Mwanza zote zimeenda CHADEMA. Kata ya Msambweni Tanga imeenda CUF. CCM walipata kata katika Wilaya ya Bagamoyo, Bariadi na Temeke. Pia walipata kata katika manispaa ya Dodoma.

Huu ni uchaguzi wa kwanza wa Madiwani ambao CCM imepoteza nusu ya viti vilivyokuwa vinagombewa toka mfumo wa vyama vingine uanze. Arumeru imekuwa jimbo la kwanza CCM kulipoteza kwa chama cha upinzani Tangu mwaka 1997 ambapo CCM walipoteza jimbo la Magu kwa chama cha UDP. Kwa CHADEMA hili ni jimbo la kwanza kulichukua kutoka CCM katika uchaguzi mdogo toka ianzishwe mwaka 1992. Itakumbukwa kwamba mwaka 2008 CHADEMA ilishinda jimbo la Tarime kwa kulirejesha maana kilikuwa linashikiliwa nacho.

People's power

Hivyo ni dhahiri kabisa kwamba siku za CCM kuwa madarakani zinahesabika. Ushindi wa Arumeru na Udiwani katika kata mbalimbali umeleta mageuzi makubwa ya kisaikolojia kwa wananchi kuliko hata ushindi wa Tarime. Ni wazi kabisa kuwa ushindi huu utafutiwa na mikutano wa kunadi chama katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Kusini na ile ya Magharibi ambapo CHADEMA haijafanya operesheni.

Kushindwa kwa CCM Arumeru pia kutal eta mpasuko zaidi ndani ya CCM na kuunganisha nguvu za wanasiasa ndani ya CHADEMA. Wakati CCM itakuwa inanyoosheana vidole kutafuta mchawi na hata wengine kufurahia kushindwa kwao (wakiamini ni kushindwa mmoja wa mahasimu wao), CHADEMA itakuwa inashikana mikono na kuimarisha mshikamano ili hatimaye kuchukua Dola ifikapo mwaka 2015.

Jambo moja la dhahiri unaliona Baada ya uchaguzi wa Arumeru. Sasa ukipanda Basi kutoka Moshi kwenda Arusha, utopita ngome ya Chadema tu. Moshi mjini, Hai, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini. Kwa waliomsoma Rais Museveni katika kitabu chake cha Sowing the Mustered seed, akitumia njia za Frelimo katika ukombozi, eneo hili sasa ni Liberated Zone. Ukanda uliokombolewa.

Lengo langu ni kuonyesha kuwa hii ndio safari ya mwisho ya CCM na kwamba wanaondolewa madarakani kwa sababu wananchi wamekasirishwa, hasira ambazo fedha haiwezi kununua. Hasira ambayo matusi hayawezi kuifuta. Hasira ambayo vitisho havifui dafu. Hasira ya kutaka huduma bora. Hasira ya kuchoka na umasikini na kufukarishwa. Hasira ya kuchoshwa na ufisadi.