Friday, July 7

G20: Trump na Putin wakutana ana kwa ana mara ya kwanza kabisa

Trump meets PutinHaki miliki ya pichaREUTERS
Donald Trump na Vladimir Putin wamekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza kabisa, na wakasalimiana kwa mikono huku mkutano wa G20 mjini Hamburg ukuanza.
Viongozi hao wa Marekani na Urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.
Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano huo mkuu wa siku mbili.
Kumeshuhudiwa maandamano katika barabara nje ya eneo ambapo mkutano huo unafanyika.
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano.
Alikuwa amepangiwa kufanya matembezi mafupi pamoja na wake wengine wa marais wanaohudhuria mkutano huo.
Lakini msemaji wake Stephanie Grisham amesema: "Polisi wa Hamburg walikataa kuturuhusu tuondoke."
Polisi 76 wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.
Mkutano wa G20 (Kundi la mataifa Ishirini) huwa ni mkutano wa nchi 19, zilizostawi na zinazostawi, pamoja na Umoja wa Ulaya (EU).
Katika hotuba yake ya kufungua mkutano huo, Kansela Angela Merkel alisema : "Sote tunafahamu changamoto zinazoikumba dunia kwa sasa.
"Tunafahamu kwamba muda unayoyoma na kwa hivyo suluhu lazima itafutwe. Na suluhu inaweza tu kupatikana iwapo baadhi yetu tutalegeza baadhi ya misimamo yetu na kufanya kazi kwa pamoja ingawa si lazima tulegeze misimamo sana, bila shaka, kwa sababu tunaweza kuwa na misimamo tofauti kuhusu baadhi ya masuala."
Merkel na TrumpHaki miliki ya pichaSERIKALI YA UJERUMANI
Image captionBi Merkel na Trump walizungumza kwa saa moja hivi Alhamisi
Kutarajiwe nini kutoka kwa mkutano wa Trump na Putin?
Video fupi ambayo imepakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa serikali ya Ujerumani imeonesha wawili hao wakisalimiana kwa mikono.
Bw Trump anaonekana baadaye akiupigapiga mkono wa Putin kama anaupapasa hivi huku wawili hao wakitabasamu wakiwa na viongozi wengine.
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana tena baadaye Ijumaa alasiri.
Haijabainika iwapo wawili hao watahutubia wanahabari baadaye au ni kwa kiasi gani wanahabari wataruhusiwa kufuatilia mkutano wa wawili hao.
Mwanamke akiwarushia polisi chupaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke akiwarushia polisi chupa
Magari yaliteketezwa wakati wa maandamano mjini Hamburg IjumaaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMagari yaliteketezwa wakati wa maandamano mjini Hamburg Ijumaa

Meli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong

Meli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong
Image captionMeli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong
Meli ya kwanza ya Uchina ya kubeba ndege za kivita Liaoning imewasili mjini Hong Kong.
Ziara hiyo ya kwanza nje ya China bara ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 20 tangu Uingereza ilipoikabidhi Hong Kong kwa China.
Inajiri baada ya ziara ya Xi Jinping katika mji huo wiki iliopita ikiwa ni ya kwanza kama rais wa China.
Wakati wa ziara yake ,ambayo ilikabiliwa na maandamano, alionya kwamba changomoto yoyote kwa serikali ya beijing haitakubalika.
Haki ya kisiasa ya Hong Kong imezua wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni huku kukiwa na wito wa kujitawala pamoja na kupigania uhuru.
Mwaka 2014 beijing ilisema kuwa itaruhusu Uchaguzi wa moja kwa moja wa kiongozi wa mji huo, Lakini miongoni mwa orodha ya wagombea waliokubalika na China.
Hatua hiyo ilisababisha maandamano yaliojulikana kuwa mwavuli yakitaka uhuru katika uchaguzi huo.
Ziara hiyo ya Bwana Xi ilijiri huku kukiwa na usalama mkali.
Baada ya Xi kuondoka siku ya Jumamosi ,maelfu waliandamana wakitaka haki yao ya kidemokrasia.

Ghana yatuma satelaiti yake ya kwanza anga za juu

Kundi la wataalamu waliofanikisha mradi huo
Image captionKundi la wataalamu waliofanikisha mradi huo
Ghana imefanikiwa kutuma satelaiti yake ya kwanza kabisa katika anga za juu.
GhanaSat-1, ambayo iliundwa na wanafunzi katika Chuo Kikuu cha All Nations cha Koforidua, ilitumwa hadi kwenye mzingo wa dunia kutoka kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
Shangwe, vifijo na nderemo vilitanda hewani baada ya ufanisi huo miongoni mwa watu 400, wakiwemo wahandisi, waliokuwa wamekusanyika katika mji huo wa kusini mwa Ghana kutazama moja kwa moja picha za uzinduzi huo wa satelaiti hiyo.
Mawasiliano ya kwanza kutoka kwenye satelaiti hiyo yalipokelewa muda mfupi baadaye.
Kurushwa angani kwa satelaiti hiyo ni kilele cha mpango wa miaka miwili, uliogharimu jumla ya $50,000 (£40,000).
Chuo kikuu hicho kilipokea usaidizi kutoka kwa Shirika la Upelelezi wa Anga za Juu la Japan (JAXA).
Satelaiti hiyo itatumiwa kufuatilia pwani ya Ghana kwa ajili ya kuunda ramani ya kina ya pwani ya taifa hilo pamoja na kufuatilia yanayojiri.
Kadhalika, itatumiwa kuongeza uwezo wa taifa hilo katika sayansi na teknolojia ya anga za juu.
Mratibu wa mradi huo Dkt Richard Damoah anasema kufanikiwa kwa mradi huo ni kama mwanzo mpya kwa taifa hilo.
"Hilo limetufungulia mlango kwetu kufanya mambo mengi zaidi kutoka anga za juu," ameambia BBC.
Amesema mradi huo "utatusaidia kutoa mafunzo kwa vizazi vijavyo jinsi ya kutumia satelaiti katika shughuli mbalimbali katika kanda yetu.
"Kwa mfano, [kufuatilia] uchimbaji madini haramu ni moja ya mambo ambayo tunakusudia tutafanikiwa kufanya (kwa kutumia satelaiti hiyo)".

Mke, mtoto watuhumiwa kushiriki kumuua baba

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa

Tabora. Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Mahona Pondamali (50) mkazi wa Wilaya ya Sikonge yanayosadikiwa kufanyika Aprili mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ijumaa, Julai 7, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa amesema Aprili 4 mwaka huu, mke wa marehemu Pondamali alitoa taarifa Polisi za kupotea kwa mume wake katika mazingira ya kutatanisha na ndipo Jeshi la Polisi lilipoamua kuanza uchunguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kubaini kuwa mtu huyo hakupotea bali aliuawa.
RPC Mtafungwa amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alikuwa na tabia ya ulevi na baada ya kulewa alikuwa akimpiga mke wake na watoto.
“Inadaiwa wanafamilia hiyo waliandaa mpango wa kumkodi  mtu wa kumpiga kwa ajili ya kumrekebisha tabia hali iliyosababisha mauti yake,” amesema.
Amesema kuwa baada ya wahusika kubaini kuwa amekufa ndipo walipoamua kwenda kumtupa katika shimo la wachanaji mbao.
“Polisi kwa kushirikiana na wananchi waligundua kuwa  kuna mwili katika shimo la wachana mbao  na kuamua kulifukua ndipo ndugu wa marehemu waliposema kuwa  ni ndugu yao aliyedaiwa kupotea,” amesema.
Amewataja wanaotuhumiwa kufanya mauaji hayo kuwa ni  mke wa marehemu Tatu Said (30), mtoto wa marehemu Katambi Mahona (13) na mlinzi jamii wa kukodi, Mwanza Mburuka (31).
Kamanda Mtafungwa amesema Polisi walifanikiwa kukamata ng’ombe mmoja kwa Mburuka ambaye inadaiwa kuwa alikuwa ni ujira kwa muuaji, (Mburuka.)
Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

MAMA JANETH MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bi. Winfrida Lawrent(65) kutoka Kata ya Kasenga kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Kilo 4000 Maharage, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bw. AnatoryBisate (64) kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Maharage kilo 4000, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya Kasenga AnatoryBisate (64) kulia pamoja na Bi. Winfrida Lawrent(65) kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli akiwasili katika eneo la mkutano mara baada ya kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga Chato mkoani Geita.
Mama Janeth Magufuli akiwa na viongozi wengine wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakwanza kushoto wakati wa dua kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
Mama Janeth Magufuli akifurahi pamoja Naibu Waziri wa nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati Kwaya ya Mwakazege ya kutoka Chato ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa, Wilaya na Chama waliojumuika na Waakilishi wa wazee wasiojiweza zaidi ya 400 Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Wazee wakishangilia wakati wa hotuba ya mgeni rasmi. PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakiwa katika Msiba wa Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo. Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza machache. Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akisoma taarifa fupi. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakiwa katika Msiba wa Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza machache.
Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akisoma taarifa fupi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakiwa katika Msiba wa Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza machache.
Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akisoma taarifa fupi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.