Friday, July 7

Meli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong

Meli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong
Image captionMeli ya China inayobeba ndege za kijeshi yawasili Hong Kong
Meli ya kwanza ya Uchina ya kubeba ndege za kivita Liaoning imewasili mjini Hong Kong.
Ziara hiyo ya kwanza nje ya China bara ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 20 tangu Uingereza ilipoikabidhi Hong Kong kwa China.
Inajiri baada ya ziara ya Xi Jinping katika mji huo wiki iliopita ikiwa ni ya kwanza kama rais wa China.
Wakati wa ziara yake ,ambayo ilikabiliwa na maandamano, alionya kwamba changomoto yoyote kwa serikali ya beijing haitakubalika.
Haki ya kisiasa ya Hong Kong imezua wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni huku kukiwa na wito wa kujitawala pamoja na kupigania uhuru.
Mwaka 2014 beijing ilisema kuwa itaruhusu Uchaguzi wa moja kwa moja wa kiongozi wa mji huo, Lakini miongoni mwa orodha ya wagombea waliokubalika na China.
Hatua hiyo ilisababisha maandamano yaliojulikana kuwa mwavuli yakitaka uhuru katika uchaguzi huo.
Ziara hiyo ya Bwana Xi ilijiri huku kukiwa na usalama mkali.
Baada ya Xi kuondoka siku ya Jumamosi ,maelfu waliandamana wakitaka haki yao ya kidemokrasia.

No comments:

Post a Comment