Monday, October 30

Lowassa afurahia Nyalandu kuomba kujiunga Chadema


Dar es Salaam: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM.
Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.
Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.
Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani.
“Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne.
“Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kuwania urais kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa).
Lowassa alimsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
“Nyalandu ana contacts (anafaham watu wengi) nyingi na jumuiya ya kimataifa, ni bidhaa nzuri kuwanayo,” alisema Lowassa, ambaye katika uchaguzi wa urais alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 (asilimia 39.97) ikiwa ni rekodi ya kura nyingi kwa upinzani tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992.

Meya Jiji la Mwanza ashikiliwa polisi


Mwanza. Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi ikidaiwa ni kutokana na agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella.
Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza.
Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na meya Bwire amesema kuwekwa kwake ndani kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa.
“Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017.
Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo.
Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.”
Tangu Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro kila upande ukiutuhumu mwingine kuhujumu shughuli za maendeleo.  (Imeandikwa na Jonathan Musa, Ngollo John na Saadam Sadick)

VIDEO-Nyalandu alivyoeleza kwa nini ameachia ngazi

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amefunguka mwanzo mwisho kwa nini ameamua kujiuzulu ubunge wake na kuihama CCM.
Nyalandu ameeleza hayo leo Jumatatu kuwa ameamua  kujiuzulu nafasi yake ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia leo Jumatatu, Oktoba 30.
Amesema mbali na hilo asubuhi ya leo Jumatatu amemwandikia Spika wa Bunge,Job Ndugai barua ya kujiuzulu nafasi yake ya ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo ameitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi sasa.
“Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania wenzetu na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya mihimili ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa kibunge wa kutunga sheria na wa kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana kikatiba,”
“Vilevile, naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya sasa, hakuna namna yoyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo ndio chimbuko la uongozi bora wa nchi na kuonyesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe na kwamba Serikali ni ya watu kwa ajili ya watu.”
Amesema yeye anaondoka anaondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa amekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, ujumbe wa kamati ya wabunge wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwani amejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali.
“Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna moja au nyigine, CCM nayo imekuwa chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,”
“Hivyo basi kwa dhamira yangu na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya kikatiba natangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii na nitaomba ikiwapendeza wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) basi waniruhusu kuingia malangoni mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na Chadema na Watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa kidemokrasia na uhuru wa mawazo.”
Amesema ameamua kujiuzulu kiti cha ubunge, jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania.
“Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, sote kama Taifa tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za kisiasa na makabila yote nchini uimarike. Tushindane kisera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu na Taifa lililo imara na nchi yenye adili.”

Askofu Cornelius Korir aliyechangia sana amani Kenya afariki dunia

Cornelius KorirHaki miliki ya pichaJIMBO LA KITUI/FACEBOOK
Askofu wa kanisa Katoliki nchini Kenya ambaye alifahamika sana kwa kuhimiza maridhiano na amani katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita amefariki dunia.
Askofu Cornelius Kipng'eno arap Korir wa jimbo la kanisa hilo la Eldoret, magharibi mwa Kenya alifariki dunia mapema leo akitibiwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi mjini Eldoret baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Mji wa Eldoret uliathiriwa sana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na waathiriwa wengi walitafuta hifadhi katika kanisa kuu la jimbo hilo mjini Eldoret.
Askofu Koris alizaliwa 1950 katika eneo l Segutiet Bomet katika eneo la Kericho katika uliokuwa mkoa wa Bonde la Ufa.
Alitawazwa kuwa askofu wa Eldoret mnamo Juni 1990 jimbo hilo lilipokuwa na parokia 50.
Rais Kenyatta ni miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi akimsifu kwa mchango wake kwa jamii.

Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria

Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili NigeriaHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionWatu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria
Watu 60 wametengwa katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, baada ya kukaribiana na watu wanakosiwa kuugua homa ya tumbili au monkeypox.
Kamishia wa afya katika jimbo la Kano, Kabul Gesto, alisema kwau moja ya dalili za ugonjwa huo iligunduliwa kwenye mgongwa lakini akasema kuwa ugonjwa huo huenda ukawa homa ya ndege.
"Hadi pale matokeo ya sampuni za damu yaliyotumwa kwenda mji mkuu Abuja yatakaporudishwa, hiki kitakuwa kisa cha kushukiwa," alisema wakati wa mahajIano na BBC.
Dr Getso anasema kuwa wagonjwa 11 katika majimbo 36 nchini Nigeria wameathirika na homa ya tumbuli.
Mamlaka za afya nchini Nigeria zimekuwa zikionya dhdi ya ulaji wa tumbili na nyama ya msituni wiki chache zilizopita.
Waziri wa afya Isaac Adewole anasema katika taarifa ya hivi punde kuwa licha ya tiba ya ugonjw ahuo kutujulikana hakuma wasi wasi kwa sababu homa hiyo siyo hatari.
Hata hivyo amewashauri watu kuchukua tahadhari ikiwemo kujiepusha na maeneo yenye misongamano.

VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU WAMPONGEZA MAVUNDE

Viongozi mbalimbali na waamini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa utendaji kazi na kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe.

Viongozi hao wamempongeza Mbunge Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika misikiti mbalimbali hapa Dodoma Mjini na kwa kusimamia mabadiliko makubwa katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Michezo na Uwezeshaji wananchi.

Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.

Kwa upande wake, Mavunde akizungumza katika Dua hiyo, amewashukuru Viongozi na waamini wa dini ya kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake vyema.

Mavunde ameipa Misikiti 16 Spika moja kila mmoja zenye thamani ya Tsh 4,000,000 na pia ameahidi kukabidhi Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa kwenye picha na viongozi wa dini.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisikiliza mawaidha katika Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.

Barclays Bank Tanzania launches its ultra-modern branch in Moshi

 Kilimanjaro Regional Commissioner, Ms. Anna Mghwira (centre), cuts a ribbon to officially open a new branch of Barclays Bank Tanzania in Moshi last weekend. Looking on the right is  Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed; on the left,  BBT Moshi Branch Manager, Ibrahim Omari  and Moshi District Commissioner, Kipi Warioba.
 Kilimanjaro Regional Commissioner, Ms. Anna Mghwira (centre), listens to Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left) during the opening ceremony on BBT Moshi branch. Looking on are Moshi District Commissioner, Kipi Warioba (right), BBT Moshi Branch Manager, Ibrahim Omari (second right),  and Barclays Tanzania Head of Customers Network, John Beja (second left).
 limanjaro RC. Anna Mghwira (left), being welcomed by Barclays Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations, Arona Luhanga.
Barclays Bank Tanzania Managing Director, (third left), poses for a memento photograph with some Moshi branch officials after the ceremony. 
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed giving his welcoming remarks during the opening ceremony of BBT Moshi branch in Moshi, Kilimanjaro last weekend.

Moshi District Commissioner, Kipi Warioba (second left), talking to Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (right), during the official opening ceremony of BBT Moshi branch last weekend. Looking on are, Barclays Tanzania Head of Customers Network, John Beja (left), and Moshi Municipal Mayor, Raymond Mboya.

DESTINATION TANZANIA EXCITES AMERICAN INFLUENCERS


Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke enjoying the scenery at Serengeti National Park recently during their visit organized by Tanzania Tourist Board.
By Geofrey Tengeneza.

Ms Stephenie Buelna and Carly Brooke the two famous American influencers have successfully concluded their visit in Tanzania following an invitation extended to them by Tanzania Tourist Board to visit and feature Destination Tanzania in their social media networks .

While in the country the two young ladies who are popular fashion models and bloggers with thousands of followers in their social media networks in the USA had a chance to visit Serengeti National Park, a site of great animal migration in the World and the Spice Island of Zanzibar where they took and posted different photos in their accounts of Facebook, Instagram, You tube, tweet as well as writing in their blogs and tweet.

“We had a wonderful experience in Serengeti and here in Zanzibar and most of our readers and followers have so far shown a great interest on destination Tanzania, once we are back in the USA we are going to write a lot” says Stephenie The two influencers were in the country as part of the Tanzania Tourist Board (TTB) strategies to engage celebrities and influencers in the massive campaign to promoting Tanzania as a preferred tourist destination by using social media and influencers so that to increase the number of tourists visiting the country and revenues.

USHAHIDI KESI YA MALKIA WAPIGWA KALENDA


Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Octoba 30, imeahirisha kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi wa meno ya tembo ya bilioni 13 a raia wa China, Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' na wenzake wawili sababu, shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake leo anaumwa.

Mwendesha Mashtaka wa serikali, Wankyo Simon amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini shahidi anaumwa, akaomba ipangiwe tarehe nyingine.

Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alisema hana pingamizi na kesi hiyo imeahirishwa hadi November 7 mwaka huu.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Washtakiwa hao, wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.

Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Ni Wakenya Rock City Marathon 2017

 Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19

Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ambae mbali na kuzindua mbio hizo pia alishiriki katika mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mkenya George Onyacha aliyetumia muda wa saa 02:23:27, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.

Katika mbio hizo zilizoanzia na kuhitimishwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo ilishuhudiwa nafasi ya kwanza hadi ya saba zikishikwa na wakimbiaji kutoka nchini Kenya huku nafasi ya nane ikienda kwa Mtanzania Paschal Mombo alietumia muda wa saa 02:30:43.

Akizungumzia siri ya ushindi wake, mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliomuwezesha kukimbia bila changamoto yoyote Too alisema ni kujituma kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.

“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi na ninashukuru Mungu nimefanikiwa,” alisema.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Alice Gradys Otero aliyetumia muda wa saa 02:48:18 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Tecla Chebet  aliyetumia saa 02:54:28 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Flavious Kwamboka alietumia muda wa saa 02:57:32.
Mtanzania Brabuelia Bryton kutoka mkoani Moshi alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 03:14:41

Washindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini humo  waliibuka na kitita cha Sh 4 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh 2 mil na washindi watatu Sh Mil 1.

Kwa upande wa mbio za km 21 Peter Limo kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa 01:05:24, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo George Wayaki aliyetumia muda wa saa 01:05:50

Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mtanzania Chacha Boy aliyetumia muda wa saa 01:05:59, ikiwa sekunde tisa tu nyuma ya mpinzani wake.

Upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Mkenya Dorifin Omare aliyetumia muda wa saa 01:17:12 akifuatiwa na Mkenya mwenzie Alice Mogiare aliyetumia saa 01:18:30 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mkenya Maiselina Issa alietumia muda wa saa 01:19:55.

Mtanzania Siatha Romanus kutoka mkoani Arusha alishika nafasi ya sita kwa upande wa wanawake katika mbio hizo akitumia saa 01:25:58
Katika mashindano hayo ilishuhudiwa washiriki ambao pia ni wadhamini wa mbio hizo kutoka  makampuni ya PUMA, Tiper, NSSF, RedBull,  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS wakishiriki kikamilifu katika mbio za KM 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri Shonza alisema aliwapongeza washiriki na waandaaji wa mbio hizo na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kurejesha hadhi ya mchezo wa riadha nchini.

“Tanzania inaweza kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia ngazi ya shule za msingi.” Alisema.

Naye Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka mbali  mbali na kuwapongeza waandaaji wa mbio hizo alisema licha ya wingi wa washiriki kutoka ndani ya nchi bado taifa linakabiliwa na uhaba wa wanaridha wa mbio ndefu yaani km 42 na wachache wanaofanya vizuri kwenye mbio hizo wamekuwa wakishindwa kushiriki mbio kama hizo zinazofanyika ndani ya nchini.

Abrahamu Too kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19.

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana  ambapo alikimbia mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.
 Baada ya uzinduzi kazi ikaanza!
 Mbali na kuzindua mbio hizo pia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (wa pili kulia)alishiriki kikamilifu katika mbio mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.

 Mbali na washiriki kutoka ndani ya nchin pia pia washiriki kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China na Marekani nao hawakuwa nyuma.

Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kwenye warsha ya kukabidhi zawadi kwa washindi ambapo pamoja na mambo mengine aliwapongeza waandaaji wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI).


Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mbio za Km 42 (waliosimama nyuma) mara baada ya kuwakabidhi zawadi pamoja na medali. Wengine ni pamoja na Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka(wa tatu kushoto), waandaaji pamoja na viongozi wa mchezo huo.

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 42 kwa upande wa wanawake ambapo washindi wa kwanza hadi watano wote walitoka nchini Kenya.
 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 5 ambazo zilikuwa mahususi kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi pamoja na washiriki kutoka kwenye mashirika mbalimbali (corporate race)
Meneja Mahusiano Mkuu wa Kampuni ya kuhifadhi mafuta nchini Tiper, Bw Emanuel Kondi (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi wa mbio hizo. Kampuni ya Tiper ni moja ya wadhamini wakubwa wa mbio hizo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuisaidia Serikali kutangaza utalii kupitia michezo pamoja na kuinua ya michezo kupitia riadha.

 Baadhi ya washindi wa mbio hizo, waandaaji na viongozi wa mchezo wa Riadha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Huduma kwa wateja Kanda ya Ziwa kutoka  kampuni ya ndege ya Precision Air, Bi Isabella Mwalwiba mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kampuni ya Precision ni miongoni mwa wadhamini wakubwa wa mbio hizo.
 Baadhi ya washindi wa mbio hizo wakipokea zawadi zao kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya CF Hospital ya jijini Mwanza.zawadi zao. CF Hospital ni miongoni mwa wadhamini  wa mbio hizo.
 Baadhi ya washindi wa mbio hizo, waandaaji na viongozi wa mchezo wa Riadha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Kanda  wa  kampuni ya Ulinzi ya KK Security, Bi Levina Vedasto  mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Kampuni ya KK Security ni miongoni mwa wadhamini wakubwa wa mbio hizo ambapo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi waliwahakikishia washiriki uwepo wa ulinzi na Usalama.
 Baadhi ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi wakifurahia medali zao!

Baada ya ushindi ilikuwa ni furaha tupu!