Monday, October 30

Askofu Cornelius Korir aliyechangia sana amani Kenya afariki dunia

Cornelius KorirHaki miliki ya pichaJIMBO LA KITUI/FACEBOOK
Askofu wa kanisa Katoliki nchini Kenya ambaye alifahamika sana kwa kuhimiza maridhiano na amani katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita amefariki dunia.
Askofu Cornelius Kipng'eno arap Korir wa jimbo la kanisa hilo la Eldoret, magharibi mwa Kenya alifariki dunia mapema leo akitibiwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi mjini Eldoret baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Mji wa Eldoret uliathiriwa sana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na waathiriwa wengi walitafuta hifadhi katika kanisa kuu la jimbo hilo mjini Eldoret.
Askofu Koris alizaliwa 1950 katika eneo l Segutiet Bomet katika eneo la Kericho katika uliokuwa mkoa wa Bonde la Ufa.
Alitawazwa kuwa askofu wa Eldoret mnamo Juni 1990 jimbo hilo lilipokuwa na parokia 50.
Rais Kenyatta ni miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi akimsifu kwa mchango wake kwa jamii.

No comments:

Post a Comment