Friday, October 13

UN yasema idadi ya wakimbizi Wakiislam wa Rohingya inaongezeka

Wakili wa wakimbizi wawili wa Rohingya asema hatma ya zuio dhidi ya Serikali ya India kuondolewa nchini limeahirishwa Ijumaa, Octoba 13, 2017.
Mashirika ya misaada yanaongeza operesheni za huduma mbalimbali ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya idadi ya wakimbizi wa Rohingya inayoongezeka katika kambi za wakimbizi huko Bangladesh.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa idadi mpya ya wakimbizi wanaowasili hapo inaongezeka kutokana na msukumo unaotokana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi jirani ya Myanmar tangu mwisho wa Agosti kufikia watu 536,000 kama ilivyoripotiwa na VOA.
Ripoti iliyotolewa Jumatano huko Geneva na ofisi ya haki za binadamu ya UN imewatuhumu wanajeshi wa Myanmar, wakisaidiwa na makundi ya wanajeshi wakibudha wenye silaha, kwamba siyo tu wameshambulia majumba ya Waislam wa Rohingya na vijiji vyao lakini pia wamekuwa wakijaribu “kuondoa kabisa alama na kumbukumbu zote za watu hao katika ardhi yao” huko eneo la Rohingya ili kufanya watu hao wasiweze kuwepo kabisa katika nchi hiyo.

Zaidi ya wakimbizi nusu milioni wamekimbia Myanmar kuelekea eneo la Bangladesh Cox Bazar tangu Agosti 25, wakati mashambulizi katika vituo vya usalama yalipofanywa na wapiganajiwa Rohingya na kusababisha majeshi ya Myanmar kutumia nguvu kupita kiasi kupambana nao.
Lakini ripoti ya UN iliyokuwa imejikita katika mahojiano 65 iliyofanya na mamia ya wakimbizi, imesema kuwa operesheni ya kuwaondosha Waislam wa Rohingya huko eneo la Rakhine ilianza mapema kwa mwezi moja takriban.
Wakimbizi wamewaambia wachunguzi wa UN kwamba hata kabla ya mashambulizi na baada yake, vyombo vya usalama vilitumia vipaza sauti kuwashinikiza Waislam kukimbia eneo hilo na kutafuta hifadhi huko Bangladesh, la sivyo “tutachoma nyumba zenu na kuwaua.”
Pia Waislam wa Rohingya wameeleza visa vilivyofanywa na vyombo vya usalama ikiwemo kuwapiga risasi wanavijiji na ubakaji wa makundi kwa wasichana wadogo chini ya miaka mitano yaliofanywa na askari wasio na magwanda.
Wimbi kubwa la wakimbizi wa Rohingya takriban 11,000 tayari wamewasili kupitia mpakani mwa nchi hiyo wakiingia Bangladesh Jumatatu. Msemaji wa UN katika masuala ya wakimbizi Andrej Mahecic amesema kuwa ilivyokuwa eneo la mpakani liko shuwari, lakini ameongeza kuwa bado watu wanahangaika nchini Myanmar wakijaribu kuondoka kuelekea Bangladesh.
"Bila shaka kuna idadi kubwa ya watu wameripotiwa au wanasubiri kuvuka mto Naf kwa kutumia maboti na kisha kuvuka Bangladesh.”
Operesheni kubwa ya misaada inaendelea kufanyika huko eneo la Cox Bazar, Bangladesh, ambapo mashirika ya misaada yamekuwa yakiwasaidia wakimbizi hao sehemu za kuishi, chakula, maji, usafi na mahitaji mengine muhimu. Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu na Shirika la Mwezi Mwekundu lina wasiwasi juu ya upatikanaji wa mahitaji mbalimbali muhimu ya afya katika jamii hizo za wakimbizi.
Mkurugenzi wa Afya wa Red Cross Julie Hall amesema kliniki zinazotumia magari tayari zimeweza kuwasaidia zaidi ya watu 4,000, lakini huduma hizo bado hazitoshelezi kabisa. Amesema kuwa shirika lake liko mbioni kutayarisha hospitali ya rufaa yenye vitanda 60.
“Hili litafanyika kati ya kambi mbili kubwa. Itaweza itapoanza kutoa huduma, kuwa na kitengo cha upasuaji, ukunga na wagonjwa wa nje pamoja na maabara, etc. Na hii itakuwa ni huduma inayotolewa siyo tu kwa wahamiaji lakini pia kwa wenyeji wa eneo hilo waliowapokea wakimbizi hao.
Mbali na hatua hizi, mashirika hayo yanafanya juhudi kupunguza na kuzuia maambukizi. Kampeni ya chanjo ya cholera inaendelea kwa masiku kadhaa. WHO imeripoti kuwa watu 235,000 kati ya walengwa 650,000 kati ya walengwa wa kampeni hiyo tayari wamepewa chanjo hiyo dhidi ya maradhi hayo hatarishi.

Polisi yatangaza kuviwajibisha vikundi vya Whats App Tanzania

Viongozi wa makundi ya What's App nchini Tanzania wanatakiwa kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.
Kufanya hivyo kutawasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa na naibu mkuu wa kitengo cha Makosa ya Mtandano, Joshua Mwangasa wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi makosa ya kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.

Viongozi wa makundi hayo wametakiwa kutowavumilia wahalifu hao na mara moja wametakiwa watoe taarifa polisi.

"Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika," Amesema Mwangasa.

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.

Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.

"Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo," amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.

Amesema simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha hivyo matumizi yake yanapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Mkuu wa Mkoa Akemea vikao kudorora

MKUU WA MKOA WA RUKWA, ZELOTE STEVEN.

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Steven ameagiza kuanza kufanyika vikao vya kamati za maendeleo za wilaya (DCC) kwa kuwa vimekuwa havifanyiki kwa muda mrefu hali inayonyima fursa ya kupata ushuru mzuri kutoka ngazi ya wilaya.

Akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Rukwa (RCC) alisema kwa muda mrefu vikao hivyo havijafanyika kwa kisingizio cha kutokuwa na posho, kitu ambacho si sahihi.

Zelothe alisema kwa ngazi ya mkoa, kikao hicho kimekuwa kikifanyika bila posho, lakini cha kushangaza kwa ngazi ya wilaya vikao kama hivyo havifanyiki.

"Naagiza kuanzia sasa ni lazima vikao hivyo vifanyike. Posho ya kikao isiwe kigezo mbona vikao vya RCC vinafanyika na kama hakuna posho, tunalipa pindi zinapopatikana. Sitaki kusikia kuwa hamfanyi vikao vya DCC kwa madai kakuna posho," alisema.

Aliwasihi watumishi wa umma kuongeza kasi katika kuwatumikia wananchi kwa sababu dunia hivi sasa imebadilika hivyo “lazima tukimbie kwa sababu mkoa wa Rukwa unahitaji maendeleo kwa kasi kubwa”.

Katika kikao hicho, mmoja wa wajumbe waalikwa, Zeno Nkoswe, alipendekeza kuwa umefika wakati sheria iliyoanzisha vikao hivyo itazamwe upya, ili uwakilishi uongezwe kwa kuwa wajumbe halali ni 28 ambao wanawakilisha zaidi ya wakazi milioni moja wa mkoa huo.

Nkoswe alisema kutokana na zama za sasa, ni vyema idadi ya wajumbe wa kikao hicho ikaongezeka kwa uwakilishi, tofauti na sasa kwa sababu walio wengi ni waalikwa na iko siku wanaweza wasihudhurie kwa vile hawabanwi na sheria.

Afariki dunia mgodini

KAMANDA WA POLISI MKOA WA GEITA, MPONJOLI LODSON.

MCHIMBAJI mmoja amefariki dunia na mwingine kunusurika baada ya kufukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa dhahabu usio rasmi wa Bingwa, katika kijiji cha Rwamgasa wilaya na mkoa wa Geita usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Lodson, alisema jana kuwa aliyefariki ni Fikiri Paulo (27), mkazi wa kijiji cha Mlanda wilayani Chato ambaye mwili wake ulitolewa shimoni akiwa ameshaaga dunia.

Mwili huo ulitolewa shimoni na wachimbaji wadogo, kwa mujibu wa mkurugenzi wa mgodi wa Bingwa, Hussein Nyanzala.

Nyazala alisema walikesha wakiendesha zoezi la kuufukua mwili wa marehemu kuanzia saa 5:00 usiku ajali ilipotokea hadi saa moja asubuhi ya jana.

Kamanda Mponjoli alimtaja manusura wa ajali hiyo kuwa ni Musa Evarist (19), mkazi wa kijiji cha Mpomvu.

Alisema Evarist aliokolewa muda mfupi baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mwamba.

Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni kukatika kwa gema la udogo wa mwamba wa mawe katika shimo walimokuwa wakichimba vijana hao.

Baada ya gema kukatika, imeelezwa, kifusi kulifukia wachimbaji hao.

IGP SIRRO AKAGUA MAABARA YA KISAYANSI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (CP) Alice Mapunda, alipokagua Kamisheni hiyo kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akiangalia moja kati ya sampuli zinazofanyiwa Uchunguzi wa Kisayansi katika Maabara ya Polisi Makao Makuu, alipofanya ukaguzi kwenye kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi kwa lengo la kuona namna wanavyofanyakazi pamoja na changamoto wanazokutananazo wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Picha na Jeshi la Polisi.

WAZIRI MBARAWA ASISITIZA JUU YA KUWATUMIA WAANDISI VIJANA KATIKA MILADI MIKUBWA NCHINI


 Waziri wa  Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa , akizungumza na Wahandisi majengo wakati wa ufunguzi wa semina yao ya siku mbili katika ukumbi  wa Mlimani City Jijini  Dar es Salaam
 Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa , akikabidhi zawadi kwa Mwalimu wa shule ya Sekondari Royola , Venancy Robert mara baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwa sekondari zote nchini
 Waziri wa  Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa ,  kwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Royola,Ashraf Raphael mara baada ya kuibuka bingwa wa kitaifa katika uandishi wa Insha
 Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Prof Makame Mbarawa.
Waziri wa  Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi , Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Insha za uandishi wa majengo
PICHA ZOTE NA HUMPHREY SHAO

HUONI HAFIFU HUCHANGIA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI DARASANI

 Mwalimu wa shule ya Msingi Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
 Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima


 Zoezi la Uandikishaji wa majina wanafunzi wa shule ya Msingi Nguvumali kwa ajili ya upimaji wa macho likiendelea
Zoezi la kuwapima wanafunzi likiendelea
SABABU kubwa za wanafunzi wa shule za msingi  kutokufanya vizuri darasani imeelezwa inatokana  na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana akili .

Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15 wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.

Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.

“Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.

Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.

Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia matitabu zaidi na kampuni hiyo.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Noor Optics, Raouf Nasser alisema lengo kubwa ni kutoa huduma hiyo katika shule zote za msingi ili kusaidia kubaini changamoto za macho zinazowakabili na namna ya kupatiwa ufumbuzi.

Alisema alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Tanga wameamua kuendesha zoezi hilo kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto ambao watabainika wanakabiliwa na matatizo hayo ili waweze kufikishwa kwa wataalamu kwa matibabu zaidi.

“Asilimia kubwa ya wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika hospitali kufanyiwa vipimo vya matatizo hayo hivyo sisi tumeamua kwa nia moja kusaidia jamii ikiwa ni kurudisha faida kwao kutokana na huduma tunazotoa “Alisema.

Aidha alisema msingi mzuri wa kuyatunza macho ni lazima kuwepo utaratibu wa kuyafanyia vipimo mara kwa mara hasa wanapokuwa kwenye hatua ya ukuaji kabla ya kufikia umri mkubwa ambapo tatizo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI


MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete  alikabidhiwa  tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike  iliyotolewa na  Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.

Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo  Mkurugenzi wa Room To Read  Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.

Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa  wa Pwani mama  Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili  ya wanafunzi wakike  sanjari  na kujenga  maabara  na vyumba  vya madarasa  ili kuweza  kuwarahisishia  wanafunzi  hususani wasichana  ili waweze kujifunza  bila  kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.
Mama Salma Kikwete amesema kuwa  Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi  kitaifa kwa mimba  huku sababu mojawapo ni  ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.
Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana  katika mkoa wa Pwani  na  kuzihusisha  Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha 
 Siku ya kumuenzi mtoto wa kike  huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia  maazimio  ya malengo endelevu  ya Umoja wa mataifa , viongozi  wa nchi mbalimbali  duniani  walikubaliana  na kuyapitisha   huku miongoni mwa malengo  matano   mojawapo  kuhakikisha  tunafikia usawa  wa kijinsia  na uwezeshaji  wa wasichana  na wanawake  wote  duniani ifikapo mwaka 2030.

Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha

WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MAFUNZO NA UTPC



Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Vijijini kutoka vilabu mbalimbali vya waandishi wa habari hapa Nchini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari hapa Nchini(UTPC),chini ya ufadhili wa SIDA yaliyofanyika leo Mkoani Morogoro.(Habari Picha na Pamela Mollel).
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Nikson Mkilanya ambae alikuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo,akisisitiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema fursa hiyo waliyoipata katika kuibua changamoto mbalimbali za vijijini.
Mkufunzi wa Mafunzo ya uwandishi wa habari za vijijini Joe Nakajumo akizungumza na baadhi ya wanahabari walioshiri mafunzo hayo leo Mjini Morogoro.
Mshiriki wa mafunzo Edith Karlo kutoka Kigoma PressClub kikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nekson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo oleo.
Mshiriki wa mafunzo Adam Juma kutoka Mtwara Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Pamela Mollel kutoka Arusha Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Agustino Kihombo kutoka Iringa Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Raya Kipingu kutoka Tanga Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Khadija Yussuph kutoka Pemba Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Eliza Faustine kutoka Mwanza Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Sunday Bavuga kutoka Njombe Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

Mshiriki wa mafunzo Ally Hamisi kutoka Zanzibar Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Anita Balingilaki kutoka Simiyu Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Amon Mtega kutoka Ruvuma Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Halima Katala kutoka Morogoro Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Norrah Damian kutoka Dar es saalam Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Alphonce Kabilondo kutoka Geita Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Laudence Semkondya kutoka Mbeya Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Happy Mtweve kutoka Dodoma Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.
Mshiriki wa mafunzo Shija Ferisha kutoka Shinyanga Press Club akikabidhiwa Cheti na Mgeni rasmi Nikson Mkilanya mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo leo.

MAISHA YANAVYOWEZA KUKUTENGENEZEA MSONGO WA MAWAZO


MAJUZI nilishuhudia watu wawili wakirushiana maneno makali kwenye foleni ya mashine ya kutolea fedha (ATM). Tukiwa tumesimama kusubiri zamu yetu ya kupata huduma, dada mmoja aliyeonekana kuwa na haraka ya kupata huduma kuliko sisi, alivuruga utaratibu wa kusimama kutaka kuwawahi waliokuwa mbele yake.
Labda kwa kukerwa na jitihada hizo za kuvuruga utaratibu, mama mmoja aliyekuwa amesimama nyuma alikosa uvumilivu. “Hivi watu wengine mkoje? Unatunaje sisi tuliosimama huku nyuma? Unafikiri hatuna haraka kama wewe? Acha dharau” alifoka mama huyo huku akitamka maneno makali yanayoweza kutafsiriwa kama matusi.
Pamoja na kosa la ukosefu wa ustaarabu lililokuwa limefanyika, watu wengi waliokuwa wamesimama kwenye foleni hiyo walifikiri mama yule alizidisha hasira. Kuona watu wanamgeuzia kibao mama alianza kumtukana kila mtu hali iliyokuza mzozo ule usio rasmi.
“Hebu muwe mnatafuta mahali sahihi pa kutolea hiyo misongo ya mawazo mliyonayo,” alipendekeza mzee mmoja kwa kejeli na kusababisha watu kuangua kicheko.
Matukio ya watu kutukanana na kurushiana maneno bila sababu ya msingi yamekuwa mengi. Unapofuatilia soga kwenye mitandao ya kijamii, vijiweni, katika usafiri wa umma na hata kupitia mazungumzo yanayofanyika kwenye vyombo vya habari, unaona namna watu wanavyojibizana pasipo kuwa staha.
Aidha, kuna tabia ya ukosoaji mkubwa unaoendelea kuota mizizi katika jamii yetu. Hivi sasa, kwa mfano, ni kawaida watu kumshambulia mtu hata yule wasiyemfahamu kwa sababu tu amejipambanua kuwa na mawazo tofauti na yale waliyonayo wao.
Hali hii ya ukosoaji na matusi ni kiashiria cha kukata tamaa kunakozidi kuota mizizi katika jamii yetu. Ni wazi watu wengi, ingawa wangependa kuwa furaha, hawana furaha. Kuna hali ya watu kuishi na uchungu mkubwa ndani yao na hawajui wafanye nini kung’oa mizizi hiyo.
Limeibuka wimbi la watu kutafuta majibu ya matatizo yao kupitia njia za mkato. Kuna wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ahadi ya kutatuliwa kwa shida walizonazo. Kuna wanaokimbilia biashara za kitapeli kwa ahadi ya kupata utajiri wa haraka. Wengine wanakimbia kutoka imani moja kwenye imani nyingine kutafuta majibu ya shida zinazowasumbua. Haya yote ni mifano ya kitu kinachoitwa msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo ni maumivu ya kihisia anayokuwa nayo mtu kama matokeo ya kukosa matumaini na kukata tamaa. Maumivu haya na kukosa matumaini, mara nyingi ni matokeo ya kutokufikiwa kwa matarajio. Mtu huyu anayeishia kukata tamaa, hufika mahali akakwama kifikra na hivyo kushindwa kuona njia ya haraka inayoweza kumfanya afikie matarajio aliyonayo.
Chukulia kijana aliyemaliza chuo kwa matumaini ya kupata kazi mara tu baada ya mahafali yake. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, kijana huyu anatembea na bahasha ya kaki bila mafanikio. Pamoja na jitihada kubwa anazofanya za kutafuta kazi, kijana huyu anashindwa kufikia ndoto na mipango aliyonayo ndani ya muda fulani. Ikiwa hivyo, taratibu hali ya kukataa tamaa huanza kuchukua nafasi yake na hatimaye hukabiliwa na msongo wa mawazo.
Mfano mwingine ni kuondokewa na mtu wa karibu katika maisha.  Anaweza kuwa mzazi, mwenzi wa maisha, mtoto, ndugu wa damu au hata rafiki wa karibu. Kwa kawaida, hawa ni watu ambao kwa kiasi kikubwa wanahusika na mipango tunayokuwa nayo. Hawa ndio wanaobeba thamani ya maisha yetu. Katika hali isiyotarajiwa, ghafla mtu huyu umpendaye anaondoka.
Kama hujawahi kufiwa na mtu wa karibu, ni vigumu kuelewa maumivu yanayosababishwa na kuondokewa na mtu uliyempenda. Maumivu haya humfanya mtu akapoteza ramani ya maisha na kila akitazama mbele haoni dalili za mwangaza. Moyo unajaa masononeko na uchungu na hali ya kujihurumia kupita kiasi. Bila kupata msaada wa haraka mtu anaweza kujikuta akipatwa na kichaa tunachoweza kukiita msongo wa mawazo.
Pia kuna matukio mengine kama kuugua au kuuguza mtu kwa muda mrefu; kukosa au kufukuzwa kazi; kukataliwa, kusalitiwa au kuachana na mpenzi au mwenzi wa maisha; kukosa mtoto baada ya kujaribu kwa muda mrefu; kugombana na watu wa karibu kama ndugu au wafanyakazi. Ipo mifano mingi zaidi ya hii inayochangia kukata tamaa. Hata hivyo, kwa ujumla msongo wa mawazo unachangiwa na ufahamu wa mtu kufika mahali akaona hakuna jibu rahisi tena la matatizo yanayomkabili.
Mtu kama huyu anaweza kujikuta akigombana na kila mtu kwa sababu tu, ndani yake anaishi na hasira ya kushindwa kufikia matarajio aliyokuwa nayo.

JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAZIWA



MAHITAJI
Maziwa ½ lita
Ngano 1 kilo
Mafuta
Chumvi kijiko kimoja cha chakula

JINSI YA KUPIKA
Bandika mafuta kiasi jikoni yaache yachemke halafu yamimine kwenye ngano, kisha koroga na mwiko au kijiko ili usiungue mikono.
Bandika maziwa jikoni na hakikisha yamechemka vizuri kisha yamimine kwenye ngano uanze kukanda unga wako taratibu.
Wakati ukikanda ongeza maziwa kama mchanganyiko wako bado mzito na endelea kufanya hivyo hadi uwe mwepesi.
Unga ukiwa tayari kata matonge halafu anza kusukuma chapatti kwa ajili ya kuchoma.
Wakati unachoma acha iive mpaka upate rangi ya kahawia, geuza upande wa pili na kuongeza mafuta kidogo huku ukiendelea kuigeuza geuza mpaka iive.
Baada ya kuiva ondoa na kuweka kwenye sahani safi na hadi hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Chakula hiki kinaweza kuliwa asubuhi kama kifungua kinywa au jioni sambamba na mchuzi wa nyama, maharagwe au supu ya samaki.