MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete alikabidhiwa tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike iliyotolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.
Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo Mkurugenzi wa Room To Read Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.
Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa wa Pwani mama Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili ya wanafunzi wakike sanjari na kujenga maabara na vyumba vya madarasa ili kuweza kuwarahisishia wanafunzi hususani wasichana ili waweze kujifunza bila kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.
Mama Salma Kikwete amesema kuwa Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi kitaifa kwa mimba huku sababu mojawapo ni ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.
Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana katika mkoa wa Pwani na kuzihusisha Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha
Siku ya kumuenzi mtoto wa kike huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia maazimio ya malengo endelevu ya Umoja wa mataifa , viongozi wa nchi mbalimbali duniani walikubaliana na kuyapitisha huku miongoni mwa malengo matano mojawapo kuhakikisha tunafikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wasichana na wanawake wote duniani ifikapo mwaka 2030.
Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha
No comments:
Post a Comment