Thursday, September 14

Mtoto ‘atekwa’ na kuuawa kisha mwili wake kutupwa mtaroni Kibaha

Morogoro. Mtoto Rehema Juma(5) mkazi wa Mtaa wa Kingolwira Manispaa ya Morogoro ameuawa na mwili wake kutupwa kwenye mtaro Kibaha mkoani Pwani baada ya ‘kutekwa’ na mtu anayedaiwa kuvaa baibui.
Mtoto huyo inadaiwa ‘alitekwa’ wakati akiwa anacheza jirani ya nyumbani kwao.
Taarifa za tukio hilo limeibua taharuki kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro hususani wenye watoto wadogo hasa ukizingatia siku za hivi karibuni kulitokea matukio ya utekaji na mauaji ya watoto jijini Arusha ambapo tukio hili la Morogoro bado halijafahamika kama visasi ama ushirikina.
Bibi aliyekuwa akimlea toto huyo, Maua Muhongole (74) amesema mtoto huyo alitekwa Septemba 12 jioni alipokuwa akicheza na wenzake na kwamba jitihada za kumtafuta zilifanyika hadi kufikia leo ndipo alipokea taarifa za kupatikana kwa mwili wa mtoto huyo maeneo ya Kibaha mkoani Pwani.
"Majira ya saa mbili kasoro usiku wakati chakula kikiandaliwa nilimtuma mjukuu wangu mwingine akamuite mwenzake ambapo alirudi na kunimbia kuwa wenzake wamemwambia hayupo kaondoka na mwanamke aliyevaa baibui kwenda kuchukua pipi dukani muda mrefu uliopita," amesema Maua .
Mtoto Ndichai Idrisa (6) ambaye alimuona Rehema akiondoka alisema aliondoka na mama huyo wakati yeye akiwa kwenye baiskeli akirudi nyumbani na baba yake na alimuita ili arudi nyumbani lakini Rehema hakuongea lolote.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kumtafuta mtuhumiwa aliyehusika na wizi wa mtoto huyo kabla ya kuuawa.
Kamanda Rwegasira alikiri kupokea taarifa za kupotea kwa mtoto huyo hata hivyo alisema kuwa tayari ameshatuma askari wake kwenda eneo la tukio kunakohisiwa kuwa mwili wa mtoto ulikutwa kwenye mtaro ili wajiridhishe na kuweza kutoa taarifa.
Amesema tukio la wizi wa mtoto lilitokea Septemba 12 saa mbili usiku na kwamba inadaiwa mwizi wa mtoto huyo alimdanganya  amfuate ili akampatie pesa na kutokomea naye.
Amesema pia mwizi wa mtoto huyo alitumia gari ndogo aina ya taxi yenye rangi nyeupe iliyokuwa imeegeshwa mita 60 kutoka eneo la tukio ambalo lilionekana tangu majira ya mchana na baada ya tukio hilo gari hilo lilitoweka.

Majaliwa atoa tamko usimamizi wa madini

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani(katikati) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Mtaalamu wa Jiolojia, Timo Gawronski,walipotembelea maabara zilizopo kwenye kituo cha madini(AMGC). 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuandaa mikakati madhubuti ya kusimamia sekta hiyo kwa manufaa ya Taifa.
Amesema hayo alipofunga mkutano wa 37 wa ngazi ya mawaziri wa nishati na madini wa nchi wanachama wa Kituo cha Madini Afrika (AMGC) uliolenga kujadili mchango wa sekta ya madini katika maendeleo ya bara hilo.
Mkutano huo umefanyika leo Alhamisi katika kituo cha AMGC kilichopo jijini hapa, Tanzania ikiwa mwenyekiti.
Waziri mkuu amesema licha ya nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania kuwa na utajiri wa madini, sekta hiyo haina tija kwa maendeleo hivyo ameagiza kuandaliwa mikakati madhubuti.
"Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa madini, sehemu kubwa ya madini hayo hayajatumika. Tanzania ina madini mengi kama vile dhahabu, almasi na Tanzanite lakini mchango wake ni asilimia nne pekee," amesema.
Kutokana na hali hiyo, amezitaka nchi wanachama wa AMGC kuandaa mikakati ya pamoja ili madini yawanufaishe wananchi.
"Changamoto iliyopo ni jinsi gani tunaweza kusimamia sekta hizi na kuleta maendeleo kuliko kuacha mashimo na umasikini," amesema.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amesema wamepokea maagizo hayo na kuanzia mwakani watatumia kituo hicho kuchenjua mchanga wa madini na kufanya uyeyushaji.
"Nitoe wito kwa kampuni za madini na wachimbaji wadogo kuanza kuleta madini kwenye kituo hiki kwa ajili ya kuongeza thamani na kufanya uchambuzi," amesema

Mbunge wa CCM aeleza alivyohusika ndege iliyomsafirisha Lissu

Dodoma. Mbunge wa Mpendae (CCM) Salim Hassan Turky ameeleza alichokifanya katika suala la ndege iliyomsafirisha Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ni kuingia dhamana na si kulipa malipo taslimu ya dola 9,000 za Marekani.
Turky alimesema hayo leo Alhamisi mara baada ya kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa alilipia gharama za ndege hiyo.
Amesema kuwa nyaraka inayosambaa katika mitandao ya jamii inayosemekana kutumwa na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Peter Msigwa sio tiketi ni invoice.
Amesema anapenda kuiweka Tanzania katika hali ya usalama na ukweli na kwamba maneno mengine si vizuri.
“Tusifanye tukio la Tundu Lissu kuwa la siasa. Mimi binafsi tukio zima la mbunge mwenzangu limenisikitisha sana limenisononesha sana. Nikiwa kama kamishna wa Bunge lakini pia ni binadamu kuna kuzaliwa na kufa,”amesema.
“Kwa hiyo tukio hilo lilipotokea tuliitwa na makamishna wote na Spika wetu wakiwemo Mbowe (Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani) Msigwa na timu yake. Kwanza ndege ilikuwepo pale Airport ambayo ilikuwa imeshaagizwa na Bunge iko stand by kumpeleka moja kwa moja Muhimbili.”
Amesema walichoamua ni kuwa aende moja kwa moja Nairobi nchini Kenya lakini ndege hiyo haikuwa na kibali cha kwenda nchini humo na kwamba ili uweze kwenda nchini humo unalazimika kuwa na marubani wawili.
Hata hivyo, amesema Spika Ndugai alihangaika kupata kibali cha ndege iliyokuwepo uwanjani ili iweze kumpeleka mgonjwa Nairobi.
“Wakati mambo yote tayari rubani wa ndege akasema kuna kitu kinaitwa landing Instrument ambayo ile ndege haina kwa hiyo haitaweza kuruka,” amesema.
Amesema kutokana na majibu hayo waliingiwa na sitofahamu watafanya nini lakini yeye aliingia katika uzoefu wake aliopewa na Mungu kwa kutafuta ndege kwa ndugu zake ambao wanafanya nao biashara sana.
“Nikawaambia ndege ipo wakatoa nauli zao za ghali ghali kwa sababu tunajuana wakakubali kutusaidia kwa dola 9,200 pamoja na ambulance (gari la wagonjwa) mimi ndio niliyoita kwa kubaliana na Mbowe na Msigwa kwamba Turky haya mambo yasimamie baadaye…na ndicho
kilichofanyika,” amesema.
Amesema ilikuwa siku ya pili walipe fedha hizo lakini haikuwezekana na kwamba jambo hilo limezungumziwa bungeni na Spika kuwa yeye ametoa fedha hizo na kwamba Chadema watalipa.
Amesema kauli hiyo haina tatizo kwa sabababu kama Chadema isingelipa hadi jana ingebidi atoe fedha zake kulipa deni hiyo la ndege.
“Kwa sababu wale mabwana watakuwa wamepitiliza bahati leo mchana nimempigia mwenye ndege saa 6.30 ndio akaniambia kuwa wamelipa,”amesema.
Alipoulizwa kwa maana hiyo yeye aliingia udhamini wa malikauli, Turky
amesema malikauli hiyo kwake inakubalika si kwa mtu mwingine.
Amesema malikauli iliyokuwa inahitajika pale ni kwamba kama Chadema wasipolipa basi papatikane mtu wa kulipa.
“Hapana sikulipa cash(fedha taslimu) na bahati mbaya siku ile
isingeweza kuruka kama zisingepatikana dola 9000 kwa maana lazima ulipe ndio ndege iruke na hapa Dodoma hakuna mtu aliyekuwa na hata dola 1000 kwa hivyo ilikuwa kidogo hali ngumu lakini tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake,”amesema.
Alipoulizwa kama ana hisa katika kampuni hiyo, Turky amesema hana hisa na kwamba ndege hizo amekuwa akizutumia mara nyingi .

Mchungaji Msigwa amjia juu Spika Ndugai kuhusu gharama za Lissu

Dar es Salaam. Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amemjia juu Spika wa Bunge, Job Ndugai akimtaka kuacha kudanganya kuwa ndege iliyomsafirisha Tundu Lissu ilikodiwa na mbunge wa CCM.
Maelezo ya Mchungaji Msigwa yamekuja saa chache baada ya Spika Ndugai kueleza bungeni kuwa mbunge wa CCM ndiye aliyeagiza ndege kutoka Nairobi kwa gharama za dola za Marekani 9,200 kumsaidia Lissu halafu atakuja kurudishiwa.
Baada ya maelezo hayo Msigwa ambaye yuko na Lissu kwenye matibabu jijini Nairobi ameandika, “Spika Ndugai muogope Mungu, usilete utani katika maisha ya Mh Lissu, umeliongopea Bunge na umma, gharama zote za ndege zimelipwa na Chadema na Watanzania. The parliament deserve better than you!

Matukio ya uvamizi ofisi za mawakili, Lissu yaviibua vyama 11

Mwenyekiti wa Umoja wa Viongozi wa Vyama vya

Mwenyekiti wa Umoja wa Viongozi wa Vyama vya siasa visivyokuwa na uwakilishi Bungeni Renatus Muhabi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu wa umoja huo, Abdul Mluya. Picha na Salim Shao 
Dar es Salaam.  Umoja wa vyama 11 vya siasa umesikitishwa na vitendo vya kihalifu vinavyoendelea kujitokeza hapa nchini huku vikiitaka Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama wa raia kuhakikisha wahusika waliofanya tukio la kumshambulia risasi Tundu Lissu watafutwe na wachukuliwe hatua.
Vyama hivyo ni AFP, DP, Demokrasia Makini, UPDP, Chama Cha Kijamii (CCK),  ADC,  TLP, UMD, NRA, ADA Tadea, Sauti ya Umma (SAU) ambapo vimesema mbali na tukio la Lissu, pia wameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa uhalifu katika maeneo ya ofisi za mawakili.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam walipokutana kutoa tamko la kuishinikiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuongeza muda katika utoaji wa maoni kuhusu sheria mpya ya vyama vya siasa nchini.
“Hata Rais na Watanzania wengi hawakufurahishwa na tukio hilo, tunaungana pia na Bunge na Rais aliyezungumza hadharani, akaagiza watafutwe wachukuliwe hatua. Nadhani kuna mambo mengi kwa pamoja tunatakiwa kuwa na kauli moja kama Watanzania, tutatoa tamko la pamoja kuhusu hali hiyo kisiasa na hali ya usalama wa raia,” alisema mwenyekiti wa umoja huo, Renatus Muhabi.
Katika hatua nyingine, vyama hivyo vimekubaliana kufuta mapendekezo yake katika mchakato wa kuandaa sheria mpya ya Vyama vya Siasa baada ya mchakato huo kutumia muda mwingi bila kuendelezwa huku wakiachwa nyuma bila kushirikishwa katika hatua inayoendelea kwa sasa.
Muhabi aliwaambia waandishi wa habari tayari wameshawasilisha nakala ya barua hiyo kwa msajili na nyingine wakiwasilisha ofisi ya waziri mkuu na Baraza la Vyama vya Siasa. 
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alipoulizwa kuhusu hilo amesema ni kweli barua ya vyama hivyo wameipokea. Kuhusu hoja ya kupewa rasimu, Nyahoza amesema hakuna rasimu yoyote iliyoandaliwa hadi sasa na ndiyo maana ya kuwataka watoe maoni yao.
“Wao watupatie maoni yao, unatoa maoni ndiyo unatengenezewa rasimu, halafu unapewa uangalie kilichoandaliwa,” amesema Nyahoza.

Manji arudi mtaani, amuuliza hakimu kuhusu udiwani wake

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusufali Manji (41) na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na  mashtaka saba ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh 200 milioni na mihuri.
Mbali na Manji  wengine walioachiwa huru ni Deogratius Kisinda(28), Abdallah Sangey(46)  na Thobias Fwere (43).
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Alhamisi amewaachia huru washtakiwa hao  saa saba  mchana  mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe kwa  kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi ya washtakiwa hao  na Mahakama ikaridhia.
Akiwasilisha ombi hilo mahakamani hapo, Wakili Kishenyi amesema kuwa leo yaani siyo tarehe ya kesi hiyo, ila waliomba hati ya wito ya mshtakiwa (Remove order) na kuiarifu Mahakama kuwa DPP kwa niaba ya jamuhuri  hakusudii  kuendelea  kuwashtaki washtakiwa  hao katika kesi hiyo  na akaomba iondolewe chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20.
Baada ya kueleza hayo,  Wakili wa washtakiwa hao, Hajra Mungula aliusema sheria hiyo  inaruhusu DPP kuwaachia huru washtakiwa  na pia inaruhusu kuwakamata.
Hakimu Shaidi  kutokana na ombi hilo, aliwaambia washtakiwa hao kuwa mashtaka yamefutwa, wako huru  hivyo waondoke.
Mara baada ya kuachiwa huru, Manji aliulizia kuhusu malalamiko yake aliyoyawasilisha  mahakamani hapo kuhusu udiwani wake na Hakimu Shaidi alimueleza kwa kuwa yuko huru atalishughulikia hilo.
Manji alishaeleza kuhusiana na kutokubaliana na hatua ya kumvua udiwani iliyofikiwa na halmashauri ya manispaa.
Baada ya kuelezwa hayo Manji na wenzake waliondoka kwa kutumia gari moja   mahakamani hapo kuelekea  nyumbani kwao. Kesi  hiyo kabla ya kufutwa ilikuwa katika hatua  ambayo upelelezi wake ulikuwa bado haujakamilika na  ilipangwa kutajwa mahakamani hapo Septemba 18,2017.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo, ilisomwa Julai 15, 2017, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo Manji alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo.
Kesi hiyo ilisomwa siku hiyo na wakili wa serikali Tulumanywa Majigo ambaye  alidai kuwa Juni 30, 2017 katika eneo la Chang’ombe ‘A’wilaya ya Temeke Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa na askari polisi wakiwa na bunda 35 za vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye thamani ya Sh 192.5milioni na kwamba mali hiyoilipatikana kinyume cha sheria.

Bomoabomoa kuikumba Serengeti Moshi

Lango la kuingia katika kiwanda cha Kampuni ya 

Lango la kuingia katika kiwanda cha Kampuni ya  Bia  ya Serengeti  eneo la Bomambuzi, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro likiwa limewekwa alama ya X. 
Moshi. Kiwanda cha Bia cha Serengeti (SBL) ni miongoni mwa majengo yaliyowekwa alama ya X kuashiria kuwa yanapaswa kubomolewa kwa kuwa yapo eneo la reli.  
Timu ya Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco) imeweka alama maeneo mbalimbali likiwemo eneo hilo, wahusika wakipewa siku 30 kuondoka.
Kiwanda cha Serengeti kipo Kata ya Bomambuzi mjini Moshi.
Ofisa Uhusiano wa SBL, John Wanyancha amesema hana taarifa kamili kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, amesema amejipanga pamoja na uongozi wa kiwanda kulifanyia uchunguzi.
Amesema alipokea taarifa kutoka kwa watumishi wa kiwanda leo Alhamisi saa tano asubuhi kuhusu uwekaji wa alama hizo unaoendelea. Ameahidi kutoa tamko kesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi amesema halmashauri haimiliki reli kwa kuwa ipo chini ya shirika la reli.
Mwandezi amesema yapo maeneo mawili yanayosadikiwa kuwa na hati miliki na  ameshaandaa timu kwa ajili ya kwenda kufanya uchunguzi kubaini kama yapo eneo la reli.
“Wataalamu wapo kwenye uchunguzi kubaini hati hizo ni za ukweli au la,” amesema

Mbowe: Lissu anaweza kuongea na kula kidogo

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 
Nairobi. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hivi sasa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaweza kuongea na kula kidogo.
Akizungumza na waandishi leo Alhamisi jijini Nairobi, Mbowe amesema taarifa za kwamba Lissu amepata maambukizi katika kifua ambayo yanatishia maisha yake siyo za ukweli. 
Mbowe amesema hali ya Lissu inabadilika kila siku hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anaendelea kurejea katika hali yake.
Amesema Lissu ameweza kuonana na baadhi ya waliomtembelea kwa maelekezo ya madaktari ambao wanamtibu.
"Pamoja na kwamba kuna watu wengi wanataka kumuona lakini ni wachache wanaoruhusiwa kumuona kwa kuwa madaktari wanataka apumzike,"amesema Mbowe.

Kubenea augua ghafla, apumzishwa hospitali Dom

Dodoma. Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika zahanati ya Bunge.
Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Alhamisi jioni kuwa mbunge huyo alikwenda katika zahanati hiyo baada ya kujisikia vibaya.
“Alijisikia kukosa nguvu akaenda katika zahanati hiyo, amepumzishwa na sasa hivi ndio anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndio kwanza amekaribia kumalizia dripu,” amesema Silinde.
Hata hivyo waandishi wa habari walipofika katika zahanati hiyo hawakuruhusiwa kumuona na badala yake wauguzi walisema amepumzika.
Daktari wa zahanati ya Bunge, Dk Noel Solomoni amethibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo  tangu saa 10 jioni leo.
Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza zaidi kama alifikishwa ama alikwenda mwenyewe katika zahanati hiyo iliyopo ndani ya Bunge.

Ukosefu wa umeme wasababisha watu 5 wazee kufariki Florida

Florida nursing home evacuatedHaki miliki ya pichaWFOR-TV
Watu watano katika makao ya kuwatunza watu wazee ambayo yalibaki bila umeme kwa siku kadhaa baada ya kimbunga Iram wamefariki.
Polisi waliondoa karibu watu 120 kutoka makao hayo seo Jumatano baada ya makao hayo kubaki bila vifaa vya huduma za hewa.
Meya mmoja alisema kuwa watu watatu walipatikana wakiwa wamekufa katika makao ya Holltwood Hills na wawili walifariki walipofikishwa hospitalini.
Watu milioni 10 bado hawana umeme huko Florida, Georgia na Carolina baada ya kimbunga Irma.
Irma ambacho kimewaua watu kadha nchini Marekani, kilikumba kusini magharibi mwa Florida siku ya Jumapili asubuhi.
Si makao tu ya huko Florida yaliyobaki bila umeme baada ya kimbunga Irma.
Zaidi ya nusu ya makao ya watu wazee huko Pembroke Pine, Florida bado hawakuwa na umeme hadi leo Jumatano.

''Wanawake hupoteza hamu ya ngono ikilinganishwa na wanaume''

Wanawake hupoteza hamu ya tendo la ngono ikilinganishwa na wanaumeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake hupoteza hamu ya tendo la ngono ikilinganishwa na wanaume
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia za ngono uliofanywa nchini Uingereza.
Utafiti huo umebaini kwamba huku wanawake na wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu.
Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya kufanya tendo la ngono.
Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open.
Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.
Mtaalam wa maswala ya ngono Ammanda Major amesema kuwa kwa binadamu kukosa hamu ya tendo la ngono sio swala lilisilokuwa la kawaida na kuna sababu nyingi tofauti ambazo wanaume na wanawake wanahitaji mabadiliko.
''Kwa wengine ni kawaida lakini wengine husababisha machungu mengi'' ,alisema.
Kwa jumla asilimia 15 ya wanaume na asilimia 34 ya wanawake waliofanyiwa utafiti huo walisema kuwa walipoteza hamu ya tendo la ngono kwa muda wa miezi mitatu ama hata zaidi katika mwaka uliopita.
Kwa wanaume, ukosefu huo wa hamu ya ngono ulikuwa juu miongoni mwa wanaume wa kati ya umri wa miaka 35-44 huku kwa wanawake ukionekana kati ya umri wa miaka 55 na 64.

Mbunge awasilisha ombi la kuondolewa kwa jaji Maraga Kenya

Jaji mkuu David Maraga
Image captionJaji mkuu David Maraga
Mbunge wa chama tawala cha Jubilee nchini Kenya amewasilisha ombi la kutaka kufutwa kazi kwa jaji mkuu David Maraga.
Mbunge huyo wa Nyeri, Njiri Wambugu amewasilisha ombi lake mbele ya tume ya huduma za majaji akidai kwamba jaji Maraga alihusika katika kufanya makosa.
Akihutubia vyombo vya habari, mbunge huyo anadai kwamba Jaji huyo ''aliwashinikiza'' wenzake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais Uhuu Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria mnamo tarehe 1 Septemba.
Wambugu amefananisha ubatilishwaji wa matokeo hayo ya urais na mapinduzi ya majaji na sasa anataka nia ya jaji Maraga kuchunguzwa.
Wabunge wa chama cha Jubilee na rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiukosoa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo na wameendelea na kuwataja majaji hao kuwa ''wakora''.
Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa urais wa Oktoba 17, uamuzi huo wa majaji na sababu zao utaangaziwa upya.

Aliyetaka unywele wa Hillary Clinton kutumikia kifungo jela

Aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kulia
Jaji mmoja nchini Marekani amemuhukumu kifungo jela aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli akisubiri hukumu ya kusababisha hofu ya kiusalama.
Jaji Kiyo Matsumoto alisema kuwa chapisho la mtandao wa facebok ambalo Shkreli aliahidi kumzawadi mtu yeyote atakayempatia unywele wa Hillary Clinton lilionyesha kuwa ni hatari kwa umma.
Shkreli aliyewahi kuwa afisa mtendaji wa zamani amekuwa huru baada ya kutoa dhamana ya dola milioni tano tangu alipokamatwa 2015.
Shkreli alitajwa kuwa mtu anayechukiwa zaidi nchini Marekani baada ya kampuni yake ya kuuza dawa kuongeza bei ya dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa Ukimwi.
Mnamo mwezi Agosti 2017 alipatikana na hatia ya makosa matatu kuhusiana na usalama na jopo la majaji ambalo pia lilifutilia mbali makosa mengine matano dhidi yake.
Shkreli alikuwa ameshtakiwa kuhusiana na kampuni ya dawa aliyomiliki Retropin mbali na hazina aliyokuwa akisimamia.
Siku ya Jumatano, Jaji Matsumoto aliamua kwamba chapisho hilo la Shkreli mnamo tarehe nne mwezi Septemba lililowekwa muda mfupi kabla ya bi Clinton kuanza ziara yake ya vitabu, lilionyesha kuwa ni hatari akikana hoja ya Shkreli kwamba maneno yake yalilindwa na uhuru wa kujieleza.
Bi Hillary ClintonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBi Hillary Clinton
Shkreli ambaye amekuwa akisuguana na wakosoaji wake katika mitandao ya kijamii alidai kwamba chapisho hilo lilikuwa la kejeli na la mpangilio wa DNA.
''Hili ni ombi lililochapishwa kwa lengo la kuwazawadi watakaokuletea unywele huo'', alisema jaji huyo.
Wakili wa Shkreli Benjamin Brafmin alisema: Tumekatishwa tamaa.Tunaamini kwamba mahakama ilifanya uamuzi wa makosa .
''Lakini yeye ni jaji na sasa tutalazimika kukubali uamuzi huo''.
Shkreli alipandisha bei ya dawa za ukimwi za Daraprim kwa asilimia 5000 ,2015 na kujipatia jina Pharma Bro.
Bei ya dawa hiyo ilipanda hadi $ 750 kutoka $ 13.50.