Thursday, September 14

Aliyetaka unywele wa Hillary Clinton kutumikia kifungo jela

Aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kulia
Jaji mmoja nchini Marekani amemuhukumu kifungo jela aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli akisubiri hukumu ya kusababisha hofu ya kiusalama.
Jaji Kiyo Matsumoto alisema kuwa chapisho la mtandao wa facebok ambalo Shkreli aliahidi kumzawadi mtu yeyote atakayempatia unywele wa Hillary Clinton lilionyesha kuwa ni hatari kwa umma.
Shkreli aliyewahi kuwa afisa mtendaji wa zamani amekuwa huru baada ya kutoa dhamana ya dola milioni tano tangu alipokamatwa 2015.
Shkreli alitajwa kuwa mtu anayechukiwa zaidi nchini Marekani baada ya kampuni yake ya kuuza dawa kuongeza bei ya dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa Ukimwi.
Mnamo mwezi Agosti 2017 alipatikana na hatia ya makosa matatu kuhusiana na usalama na jopo la majaji ambalo pia lilifutilia mbali makosa mengine matano dhidi yake.
Shkreli alikuwa ameshtakiwa kuhusiana na kampuni ya dawa aliyomiliki Retropin mbali na hazina aliyokuwa akisimamia.
Siku ya Jumatano, Jaji Matsumoto aliamua kwamba chapisho hilo la Shkreli mnamo tarehe nne mwezi Septemba lililowekwa muda mfupi kabla ya bi Clinton kuanza ziara yake ya vitabu, lilionyesha kuwa ni hatari akikana hoja ya Shkreli kwamba maneno yake yalilindwa na uhuru wa kujieleza.
Bi Hillary ClintonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBi Hillary Clinton
Shkreli ambaye amekuwa akisuguana na wakosoaji wake katika mitandao ya kijamii alidai kwamba chapisho hilo lilikuwa la kejeli na la mpangilio wa DNA.
''Hili ni ombi lililochapishwa kwa lengo la kuwazawadi watakaokuletea unywele huo'', alisema jaji huyo.
Wakili wa Shkreli Benjamin Brafmin alisema: Tumekatishwa tamaa.Tunaamini kwamba mahakama ilifanya uamuzi wa makosa .
''Lakini yeye ni jaji na sasa tutalazimika kukubali uamuzi huo''.
Shkreli alipandisha bei ya dawa za ukimwi za Daraprim kwa asilimia 5000 ,2015 na kujipatia jina Pharma Bro.
Bei ya dawa hiyo ilipanda hadi $ 750 kutoka $ 13.50.

No comments:

Post a Comment