Saturday, August 26

Wake wa wanajeshi walalamika kuhusu hali ya waume zao Ufaransa

Wake wa wanajeshi walalamika kuhusu hali ya waume zao UfaransaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWake wa wanajeshi walalamika kuhusu hali ya waume zao Ufaransa
Mamia ya wake wa wanajeshi wa Ufaransa, wanafanya maandamano mjini Paris, kupinga hali ya maisha wanamoishi waume zao, wakaiwa katika zamu za kupambana na ugaidi.
Mercedes Crepin, ambaye alisaidia kuunda kundi la "wake wa jeshi wenye hamaki"; amesema , baadhi ya wanajeshi wamewekwa katika mabanda ya maji na yaliyojaa mende na kunguni.
Baada ya wapiganaji wa Kiislamu kushambulia ofisi ya gazeti la Charlie Hebdo, Januari mwaka wa 2015, serikali ya Ufaransa iliweka wanajeshi zaidi ya elfu saba kulinda mahala na matukio muhimu.

Mayweather na McGregor kuzipiga katika pigano la $600m

Myweather kushoro na Conor McGregor kulia
Image captionMyweather kushoro na Conor McGregor kulia
Mashabiki wengi wa ndondi wamelifutilia mbali pigano kati ya Floyd Mayweather na Muingereza Conor McGregor wakiitaja mechi hiyo kuwa 'kihoja' badala ya pigano.
Lakini maoni hayo ya kutoridhishwa na pigano hilo miongoni mwa mashabiki wa mchezo huo hayataathiri idadi ya watazamaji wake huku pigano hilo likitarajiwa kuonyesha katika runinga za zaidi ya mataifa 220 kuingana na naibu rais wa Showtime Stephen Espinoza.
Idadi hiyo ya watazamaji kutoke kote duniani inaweza kuipiku rekodi ya watazamaji ya watu milioni 4.6 iliowekwa wakati wa pigano kati ya Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao 2015.
Watazamaji wa pigano hilo nchini Uingereza watalipa pauni 20 kila mmoja lakini wale wa Marekani watalipa pauni 75 kila mmoja.
Fedha hizi zikijumlishwa na mauzo ya tiketi ya kutazama pigano hilo ,ufadhili na biashara inaweza kuleta kiwango kikubwa cha fedha.
Mayweather na McGregor kulia muda mfupi baada ya mkutano wao
Image captionMayweather na McGregor kulia muda mfupi baada ya mkutano wao
Tiketi pia zinauzwa kutazama pigano hilo katika vilabu katika mji wa Las Vegas, huku zaidi ya kumbi 400 za filamu pia zikilionyesha pigano hilo.
Hiyo inamaanisha kwamba takriban dola milion 600 zinaweza kupatikana, kiwango kinachokaribia kile cha pigano kati ya Mayweather na Pacquiao.
Mayweather anatarajiwa kujipatia dola milioni 300 huku McGregor akiweka kibindoni dola milioni 100.
Kumekuwa na ripoti kwamba Mayweather anaonekana kumpuuzilia mbali McGregor.
Wiki hii wachanganuzi watano wamesema kuwa hatua ya Mayweather kumpuuza mpinzani wake kunaweza kuwa hatari kubwa kwake.
Floyd Mayweather akibeba mataji alioshinda kabla ya kustaafu 2015
Image captionFloyd Mayweather akibeba mataji alioshinda kabla ya kustaafu 2015
Babake Mayweather Floyd jr, wiki hii alisema kuwa mwanawe amepoteza uwezo wake mkubwa tangu alipostaafu 2015.
Lakini iwapo atashinda pigano lake la hamsini katika maisha yake ataweza kuipita rekodi iliowekwa na Rocky Marciano ya kushinda mara 49 bila kushindwa.

Majaji wafanya mgomo nchini Uganda

Majaji wafanya mgomo nchini UgandaHaki miliki ya pichaUJOA
Image captionMajaji wafanya mgomo nchini Uganda
Majaji na mahakimu nchini Uganda wameanza mgomo kufuatia tangazo la siku ya Alhamisi jioni lililotolewa na muungano wao kulingana na gazeti la daily Monitor nchini humo.
Gazeti hilo limemnukuu rais wa muungano wa majaji nchini humo {Ujoa} Godfrey Kaweesa akisema kuwa majaji wamelazimika kufanya mgomo kwasababu serikali imefeli kutoa mpango mahususi kuangazia maswala yanayowakabili mwezi mmoja uliopita.
''Kwa sababu serikali imeshindwa kuangazia maswali yetu kama ilivyoahidi'', tumeamua kufanya mgomo hadi pale hatua zitakapochukuliwa.
Kulingana na The Monitor, takriban mwezi mmoja uliopita, majaji kutoka mahakama ya juu hadi katika mahakama za mahakimu walikutana mjini Kamapala na kuamua kufanya mgomo kuanzia Agosti 23 iwapo maslahi yao hayataangaziwa.
Maafisa hao wa mahakama wanataka jaji wa hadhi ya juu , Jaji Mkuu kulipwa mshahara wa $ 15,000 huku hakimu akilipwa $ 3,000
Pia wanataka magari ya usafiri, bima ya matibabu na nyumba kulingana na Gazeti hilo.

YANGA YAMWONGEZA MKATABA GEORGE LWANDAMINA


Klabu ya Yanga pamoja na kuimarisha kikosi kwa kusajili wachezaji wenye uwezo, imempa mkataba mpya kocha wao George Lwandamina
Kocha wa Yanga, George Lwandamina hana mpango wa kuondoka, maana tayari ameongezewa muda wa kuendelea kufanya kazi Jangwani.

Uongozi wa Yanga umeamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wao George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali kumalizika Julai 16, mwaka huu.

Katika mkataba wake uliopita, Lwandamina aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kuifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya kutolewa na Mbao FC ya Mwanza.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema  mchana kuwa, wameamua kumuongezea mkataba Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake.
“Tunaingia mkataba mwingine wa mwaka mmoja na Lwandamina kwani ule wa mwanzo umeisha na sasa kila kitu kipo tayari hivyo muda wowote tena kwa uwazi kabisa atasaini mkataba mpya.
“Tumejitahidi kwa uwezo wetu kuboresha mkataba wake mpya kwa kumuongezea maslahi kidogo ili apate motisha ya kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Mkwasa.

Lwandamina alitarajiwa kusaini mkataba huo muda wowote kuanzia jana mchana ili awe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi yake kwa uhuru na kujiamini.

BRIGEDIA JENERALI MBUNGU AWATAKA ASKARI WA SUMA JKT GUARD KUWA MABALOZI WAZURI WA MAPAMBANO YA RUSHWA MAKAZINI


 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakila kiapo cha uaminifu mbele ya  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akizungumza na askari wa ulinzi binafsi wa kampuni ya Suma JKT wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya sita kwa askari wapya wa kampuni hiyo iliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT). na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri katika mapambano ya rushwa katika kazi yao na hasa katika ofisi watakazopangiw akufanya kazi
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suma Jkt Guard Limited, Meja Alfred Mwaijande akizungumza kabla ya kukamribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari wa kundila sita wa Suma jkt
 Kaimu Mkuu wa chuo cha Uongozi JKT Kimbiji .Meja Josephat Songita akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya askari wa Suma Jkt Guard kundi la Sita
 Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Mafunzo wa Suma Jkt Guard ,Luteni Albert Masawe akizunguma namna mafunzo hayo yalivyoendeshwa kwa mgeni rasmi
 Askari wa Jeshi la Kujenga taifa akipiga ngoma wakati akiongoza gwaride la askari wa Suma Jkt Guard
 Askari wa kundi la sita wanaomaliza  mafunzo ya ulinzi binafsi kundi lasita la Suma Jkt Guard wakipita kwa mwendo w aukakamavu
 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
    Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu  akiwasili katika uwanja wa kufunga kozi
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akiwa katika picha ya pamoja na askari wa ulinzi binafsi wanaomaliza mafunzo yao 

MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao. 
Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati 



Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.

Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.

Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.

"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti

Wenyeviti hao waliwataka viongozi wa Manispaa ya Iringa kutoa kwa haraka vibari vya ujenzi maana kumekuwa na ukilitimba mwingi kitu kinachosababisha ujenzi holela wa makazi kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa hivyo viongozi wanapaswa kuwa makini na mikakati madhubuti kwa kuwa wananchi wanataka kujenga nyumba zao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Sweetbert Maro alisema kuwa kweli posho wanazopewa wenyeviti wa mitaa ni ndogo hivyo uongozi wa halmashauri ya manispaa imejipanga kukaa pamoja wenyeviti kujadili jinsi gani ya kuongea posho hizo kulingana na majukumu wanayoyafanya kuiwakilisha serikali.

"Mnafanya kazi kubwa mno lakini mnapewa posho kiduchu hivyo tutakaa na kulijadili hili swala kwa kina kwa kuwa bila wenyeviti wa mitaa halmashauri haiwezi kupata maendeleo na kukuza mji kwa nguvu zote hivyo tunawaomba wenyeviti muendelee kufanya kazi wakati swala la posho linashughulikiwa"alisema Maro

Maro alisema kuwa atamshauri Mkurugenzi kutafuta muda muafaka wa kukaa pamoja wenyeviti wote wa mitaa 192 ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kuzijua changamoto na jinsi gani ya kuzitatua maana leo hii mkutano huu ulikuwa wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.

Aidha Maro aliwataka wenyeviti wa mitaa kuwabana maafisa watendaji wa mitaa maana uongozi wa halmashauri umekuwa ukitoa posho kwa wakati kulingana na agizo la serikali na kufuata sheria ya ugawaji wa posho kwa walinzi wa amani kwenye mitaa yako.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa kuna kero nyingine atazipeleka bungeni ili kuweza kupatiwa ufumbuzi zaidi na kuzitafutia njia za kuzitatua maana kwa ngazi ya Manispaa wameshindwa kuzitatua.

Kabati aliwaahidi wenyeviti wote wenye kero za ngazi ya manispaa atahakikisha zinatatuliwa kwa wakati lakini amewahakikishia kuwa ataitembelea mitaa yenye kero ambazo zipo kwenye uwezo wake atazitatulia huko huko kwenye mitaa.Wenyeviti hao walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kuwakutanisha na viongozi wa halmashauri na kusikiliza kero zao kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ambao utaongeza tija ya kuleta maendeleo kwenye mitaa hao.

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017.

 Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.

“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.

Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.

TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.

“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo. 
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake. 
Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

Tanzania yatoa makataa kwa wakimbizi wa Burundi nchini humo

Wakimbizi wa Burundi walioingia Tanzania
Image captionWakimbizi wa Burundi walioingia Tanzania
Serikali ya Tanzania imelipatia shirika la wakimbizi duniani UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali yenyewe itafanya zoezi hilo yenyewe.
Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba ametoa agizo hilo siku ya Alhamisi alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kambi ya Nduta Magharibi mwa Tanzania ambayo ni moja ya kambi zinazohifadhi wakimbizi wengi wa Burundi.
Tanzania ndio nchi inayoongoza Afrika Mashariki kwa kuhifadhi wakimbizi wengi kutoka Burundi.
Bwana Nchemba amewashutumu maafisa wa UNHCR kwa kuchelewesha zoezi hilo la kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea nchini kwao kwa hiari.
Tanzania yatahadharisha wahalifu waliotoka Burundi
Zaidi ya wakimbizi elfu 8 kati ya laki moja ishirini na sita elfu katika kambi ya Nduta, ambayo Waziri Nchemba aliitembelea, wanasemekana kuwa wamejiandikisha kurejea kwao Burundi kwa hiari.
Na sasa bwana Nchemba ameonya kwamba ikiwa UNHCR haitaanza zoezi la kuwarudisha wakimbizi hao, basi serikali italazimika kufanya yenyewe na kwamba itaomba magari kutoka jeshini ili kutekeleza zoezi hilo.
Akizungumza katika chumba kilichojaa wakimbizi, waandishi wa habari na maofisa wa serikali na UNHCR wenyewe, Waziri Nchemba alitoa agizo kwamba ndani ya siku saba UNHCR iwe imetenga magari ya kubeba watu na chakula kilichokuwa kimepangwa kutumika hapo kambini tayari kwa safari
Lakini UNHCR wenyewe wanasema wanataka kujiridhishia kwamba hali ya usalama nchini Burundi inaridhisha kabla haijaanza kuwarudisha wakimbizi hao
Afisa wa UNHCR Kibondo amenukuliwa na vyombo vya habari hapa Tanzania akisema shirika hilo linaendelea kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania yenyewe lakini hata Burundi pia kuhusiana na swala hilo
Kikomo hicho cha muda cha serikali ya Tanzania kinakuja mwezi mmoja tu baada ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutembelea Tanzania na kuwasihi wakimbizi wa Burundi kurejea nyumbani.
Aliwahakikishia kwamba hali ya usalama nchini mwao ni ya uhakika
Mwenzake wa Tanzania Rais John Magufuli aliuunga mkono wito huo na kuwataka wakimbizi hao kurejea kwao na kuijenga nchi yao.
Hata hivyo Rais Magufuli alipingwa vikali na wanaharakati wa haki za wakimbizi na binadamu kwa ujumla kwamba wito wa kuwataka wakimbizi kurejea kwao haufai kwasababu taarifa zinazotoka nchini Burundi zinasema kwamba hali ya usalama nchini humo haijaimarika na kwamba wakimbizi wengi bado wanakimbilia nchi jirani
Wimbi kubwa la wakimbizi lilianza kuingia nchini Tanzania kufuatia machafuko mapya baada ya Rais Nkurunzinza kutangaza azma yake ya kutaka kuendelea kubaki madarakani - na ambapo katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Nkurunziza alichaguliwa kuendelea kuwa rais.

Yingluck Shinawatra atorokea Dubai

Yingluck Shinawatra

Image captionYingluck Shinawatra
Taarifa kutoka Thailand zinasema aliyekuwa waziri mkuu Yingluck Shinawatra ametorokea Dubai baada ya kukosa kufika mbele ya mahakama kusomewa hukumu mjini Bangkok.
Vyombo vya habari nchini vinasema alitorokea kupitia Cambodia na Singapore, kabla ya kusafiri hadi katika taifa hilo la ghuba ambako kakake Thaksin - waziri mkuu wa zamani pia, anaishi uhamishoni.
Yingluck Shinawatra alikuwa anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 gerezani iwapo angepatikana na hatia ya uhalifu kutokana na kuzembea kazini katika kesi kuhusu mpango wa ruzuku kwa wakulima wa mpunga unaosemakana kuchangia ushindi wake katika uchaguzi.

Chama cha MPLA chashinda uchaguzi wa ubunge Angola

Aliyekuwa waziri wa ulinzi Joao Lourenco

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAliyekuwa waziri wa ulinzi Joao Lourenco
Chama tawala cha Angola MPLA kimeibuka mshindi wa uchaguzi wa wabunge, matokeo ya awali ya yameonyesha.
Chama hicho kilipata asilimia 61 ya kura zilizopigwa siku ya Jumatano , kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Chama cha UNITA kilichopata asilimia 27 kimepinga matokeo hayo.
Uchaguzi huo unakamilisha utawala wa rais Jose Eduardo Dos Santos.
Uchaguzi huo unakamilika siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi Agosti kutokana na kucheleweshwa kusambazwa kwa makaratasi ya kupigia kura katika zaidi ya vituo kumi vilivyopo maeneo ya mashamabani.
Hatahivyo chama tawala cha MPLA kimechukua uongozi mkubwa wa hadi asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa.
Image captionKaratasi la kupigia kura nchini Angola
Ushindi wa MPLA unamaanisha kwamba urais unakabidhiwa aliyekuwa waziri wa ulinzi Joao Lourenco ambaye aliteuliwa kuwa mrithi wa Dos Santos.
Hatahivyo Dos Santos ambaye utawala wake wa miaka 38 unamweka kuwa kiongozi wa pili aliyetawala kwa muda mrefu duniani ataendelea kudhibiti chama hicho.
Siku ya Alhamisi, Chama cha Unita ambacho mgombea wake Isias Samakuva amkeuwa mpinzani mkuu wa Lourenco, kimesema kuwa kimefanya hesabu yake ya kura ambapo matokeo yake ni tofauti na yale yaliotolewa na tume ya uchaguzi.
Chini ya mfumo wa kupiga kura wa Angola, raia walitakiwa kuchagua mgombea na chama chake katika uchaguzi huo.
Chama cha MPLA ndio chama cha kipekee kilichotawala taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ureno 1975.
Huku Dos Santos akijiuzulu kama rais, wanawe bado wanashikilia nafasi muhimu za utawala.