Majaji na mahakimu nchini Uganda wameanza mgomo kufuatia tangazo la siku ya Alhamisi jioni lililotolewa na muungano wao kulingana na gazeti la daily Monitor nchini humo.
Gazeti hilo limemnukuu rais wa muungano wa majaji nchini humo {Ujoa} Godfrey Kaweesa akisema kuwa majaji wamelazimika kufanya mgomo kwasababu serikali imefeli kutoa mpango mahususi kuangazia maswala yanayowakabili mwezi mmoja uliopita.
''Kwa sababu serikali imeshindwa kuangazia maswali yetu kama ilivyoahidi'', tumeamua kufanya mgomo hadi pale hatua zitakapochukuliwa.
Kulingana na The Monitor, takriban mwezi mmoja uliopita, majaji kutoka mahakama ya juu hadi katika mahakama za mahakimu walikutana mjini Kamapala na kuamua kufanya mgomo kuanzia Agosti 23 iwapo maslahi yao hayataangaziwa.
Maafisa hao wa mahakama wanataka jaji wa hadhi ya juu , Jaji Mkuu kulipwa mshahara wa $ 15,000 huku hakimu akilipwa $ 3,000
Pia wanataka magari ya usafiri, bima ya matibabu na nyumba kulingana na Gazeti hilo.
No comments:
Post a Comment