Wednesday, September 27

TANZANIA YASIFIWA UN KWA MAGEUZI YA RAIS DKT MAGUFULI-DKT MAHIGA

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAJAJI NA MAHAKIMU WAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.


Waziri wa Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ally Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mkutano Mkuu wa Majaji na Mawakili uliokuwa ukifanyika jijini Dar es Salaa kuanzia Septemba 25-28, 2017 Ambpo alifunga Mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Mhe. Jaji Ignas Kitusi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunga mkutano Mkuu wa Majaji na Mawakili wa wanachama wa Jumuiya ya Madola.
 Wawakili na Majaji wakiwa katika Mkutano wa mwaka ya wanachama wa Jumuiya ya madola jijini Dar es Salaam leo.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RAIS wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania, Jaji Ignas Kitusi amesema, Serikali inamchango mkubwa katika kuiwezesha mahakama  kutimiza majukumu yake ili iweze kusonga mbele katika maendeleo, 
huku majaji na mahakimu wakizungumzia miiko ya utendaji kazi mahakama.

Jaji Kitusi amesema hayo leo wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa mwaka wa majaji na mahakimu wa Jumuiya ya madola uliomalizika leo jijini Dar es Salaam.

amesema kuwa,  katika mkutano huo wamejadili mbalo mbali moja wapo zikiwa ni changamoto wanazokutana nazo mahakimu na Majaji zikiwepo changamoto za kimtandao, usafirishaji wa binadamu ambayo pia ni changamoto.

Amesema ili kujua kama kila mwanachama wa mkutano huo amezingatia maazimio waliyofikia, mkutano mwingine mkubwa utafanyika nchini Australia ili kujipima ambapo moja kati ya maazimio waliyofikia ni  kuzingatia miiko ya kazi na kiutendaji kwa ujumla, "kwani  kila nchi imetengeneza sheria na vitabu vyake vya kanuni na maadili vinavyoongoza majaji na mahakimu.

Aidha amesema kuwa, katika mkutano huo pia wamezungumzia changamoto za ucheleweshaji wa mashauri na kuongeza kuwa kwa kuiga nchi mbali mbali ambazo zimefanya vizuri katika sekta hiyo, ni wazi kuwa nchi ambazo ziko nyuma zitaiga mfano Wa nchi hizo ili kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani.

. Changamoto ya kifedha ambayo inahitaji ushiriki Wa serikali katika kuwezesha mahakama kutimiza majukumu yaliyopo, maadili, rasilimali watu.

alisema kuwa, kuna changamoto nyingi zinazowakabili mahakimu au majaji zikiwemo za kimaadili na kutoa wito kwa Jamii nzima kuiacha mahakama ifanye kazi bila kuiingilia na pia majaji na mahakimu wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na ushahidi bila kuruhusu kuingiliwa na vishawishi kwa namna yoyote.

Aidha alisema, Serikali inaowajibu wa kuangalia kazi za majaji na mahakimu kwani kazi zao mara nyingine zinawaweka hatarini, na ni jukumu la serikali kutoa hali ya usalama kwao Ili waweze kusikiliza kesi zao bila ya kuwa na wasiwasi na usalama wa maisha yao.

WATANZANIA KIZIMBANI KWA KUSAFIRISHA RAIA WA ETHIOPIA, NA RAIA HAO KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.



 Wahamiaji Haramu wakisubiri kusomewa mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali leo jijini Dar es Salaam Katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu.
 Wahamiaji 40 kutoka Ethiopia  wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam leo na kukutwa na mashtaka ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.
 Wahamiaji haramu wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kuwasiri tukoka walipokuwa wamehifadhiwa.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. 

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii. 
WATANZANIA wawili, Ibrahim Abdallah dereva wa gari aina ya Nissan Civilian namba T 669 DJH na kondakta  Christopher Steven wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha binadamu kimagendo ambao raia 31 wa Ethiopia.

Aidha raia hao 31 wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano ya kuingia nchini kinyume cha sheria bila ya kuwa na kibali.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Novatus Mlay amedai Septemba 25, mwaka huu, huko Tuangoma wilaya ya Temeke watanzania hao walikutwa wakiwasafirisha raia hao 31 wa Ethiopia  kimagendo na kuwaingiza nchini kwa nia ya kuwapitisha na kuwasaidia kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini.
Hata hivyo, watanzania hao wamekana kuhusika na kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11, mwaka huu huku upande wa mashtaka ukieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku watuhumia hao 31 wa Ethiopia wakikubali mashtaka yote waliyosomewa na kesi iendelea Oktoba 11, 2017 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Wakati huo huo, watanzania  watatu akiwamo dereva wa kampuni ya Dangote Cement Ltd, Khalid Abdallah, Hussein Hamad Hassan na Jumanne Mtambo pamoja na wahamiaji nane raia wa Ethiopia wamesomewa mashtaka matano likiwemo shtaka la kusafirisha kimagendo binadamu na kuingia nchini kinyume cha sheria.

Wakili Mlay amedai mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kuwa, wahamiaji Solomon Ertiso, Gazahegn Tiroro , Haire  Latso, Thadius Lilanso, Dawit Habtam, Deznet Godebo, Feraru Gurana na Elioj Akola, Septemba 20,2017 katika eneo la Kongowe Mbagala walikamatwa wakiingia nchini bila ya kuwa na kibali.

baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao wote walikubali kuyatenda  makosa hayo huku  watanzania hao ambao wanakabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu wanao wanadaiwa kuwasafirisha kimagendo wahamiaji hao haramu.

Mlay alidai kuwa siku hiyo ya tukio ya Septemba 20, 2017  huko Mbagala Kongowe Khalid, Hussein  na Jumanne wakiwa raia wa Tanzania  walikutwa wakiwasafirisha wahamiaji hao haramu kimagendo.

Alidai kuwa raia hao watatu wa Tanzania waliwasafirisha  kimagendo wahamiaji hao haramu kwa kutumia gari yenye namba za usajili T 961 DKA mali ya kampuni ya Dangote Cement Ltd kwa kuwatoa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini.

Pia washtakiwa hao, kuwa siku hiyo walikutwa wakisaidia kuwasafirisha wahamiaji hao ambao ni raia wa Ethiopia kimagendo  kwa kuwaingiza ndani ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania hao wamekana tuhuma hizo na kesi hiyo itaendelea Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa huku Octoba 11 Raia hao wa Ethiopia watasomewa maelezo awali baada ya kukubali kutenda makosa hayo.

Afisa wa serikali ya Kenya aliyeshambuliwa na al-Shabab afariki

Maryam El MaawyHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionMaryam El Maawy
Katibu wa wizara ya nguvu kazi Maryam El-Maawy ambaye alishambuliwa na alshabab amefariki akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
Ikulu ya rais nchini Kenya imethibitisha kifo cha El-Maawy.
Bi El Maawy alifariki nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia shambulio la wapiganaji wa al-Shabab manmo julai 13.
Msemaji wa Ikuku manoah Esipisu alithibitishja kifi cha bi Maawy kwa taifa lakini akasema kuwa maelezo yatatolewa baadaye.
Alshabab walimpiga risasi na kumjeruhi katibu hiyo katika bega na miguu baada ya kumteka nmyara katika eneo la Milihoi katika baranara ya Mpeketoni Lamu.
Mpwa wake ambaye alikuwa akijifunza urubani na ambaye walikuwa pamoja alifariki wakati wa shambulio hilo lakini Bi Maawy aliokolewa na kundi la wanajeshi wa Kenya KDF pamoja na wale wa GSU.
Kundi la maafisa wa usalama lilimkimbiza katika hospitali ya Mpeketoni.
Baadaye alisafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu.
Wakati wa shambulio hilo, wapiganaji hao walidhibiti gari alimokuwa katibu huyo ambalo lilikuwa na watu sita kabla ya kutoroka katika kichaka.
Ndege ya KDF ililifuata gari hilo na kufanikiwa kumuokoa afisa huyo.
Maafisa wawili wa polisi pia walifariki wakati wa shambulio hilo huku wengine wawili wakitekwa na wapiganaji hao.
Siku ya shambulio hilo, katibu huyo alikuwa amehudhuria mkutano kuhusu bandari ya Lamu, barabara ya Sudan kusini, Ethiopia katika kituo cha Huduma mjini Lamu akielekea Witu.

Moto nyumba za polisi wadhibitiwa


Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema familia 13 zenye watu 44 zimeathiriwa kwa moto ulioibuka kwenye nyumba za askari polisi usiku huu.
Amesema taarifa za awali zinasema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme na uchunguzi unaendelea.
Gambo amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa  katika tukio hilo.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba amesema moto huo umeshadhibitiwa.                       
“Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Amesema taarifa kuhusu tukio hilo zimewafikia kwa kuchelewa.                       
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema hali ni shwari na hakuna wizi uliotokea.
Amesema tukio hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia  walioathiriwa.

Nyumba za polisi Arusha zinawaka moto


Familia zaidi ya 10 za askari  wanaoishi katika nyumba za polisi Kata ya Sekei mkoani Arusha zimewaka moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Kazi ya kuzima moto huo inaendelea. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pia yupo eneo la tukio.

WATANZANIA WAMETAKIWA KUENZI UTAMADUNI WETU KUKUZA FURSA ZA UTALII WA KIUTAMADUNI


Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu

Watanzania wametakiwa kuenzi mila na desturi ambazo ni chanya wazitunze na kuzitumia ili kujenga jamii yenye maadili mema nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom wilaya Mbulu mkoani Manyara ambapo amejionea utajiri wa kiutamaduni wenye fursa za utalii wa kiutamaduni.

“Nimetembelea nyumba za asili zilizopo hapa katika kituo hiki nimefurahishwa sana na utajiri wa kiutamaduni uliopo hapa, wazee walizingatia maadili katika kuwalea watoto wao kulingana na mila na desturi zao, ni vema tuenzi utamaduni wetu, huo ni msingi wa maadili mema ya jamii” alisema Naibu Waziri Wambura

Akitolea mfano wa maadili mema yanayopaswa kurithishwa aliyojionea katika kituo cha 4CCP na namna ambavyo watoto waliheshimu nyumba za wazazi wao, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzani suala la ulevi na utumiaji wa tumbaku kwa vijana ilikuwa ni mwiko hadi kijana afikie umri wa utu uzima ambapo anaweza kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yake yenye kuwa na tija kwa familia.

“Kabla ya kuoa kijana alikuwa haruhusiwi kutumia tumbaku na kunywa pombe, bali kijana akioa na kuwa na watoto wawili kwa mujibu wa mila za makabila ya yaliyopo Mbulu aliruhusiwa kuingia katika kundi la watu wazima na kuruhusiwa kutumia vitu mbalimbali ikiwemo tumbaku na kinywaji cha pombe. Hapa kuna jambo la Watanzania kujifunza na kutunza ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili” alisema Naibu Waziri Wambura.

Mila za jamii zilizo njema zinapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili ziweze kusaidia vijana na jamii kwa ujumla kuweka mawazo yao katika shughuli za maendeleo pamoja na kupatia familia zao mahitaji ya kila siku.

Naibu Waziri Wambura alisisitiza kuwa mila hizo hazitakiwi kuachwa bali zainatakiwa kuenziwa, kutunzwa, kuendelezwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya sasa ziweze kuchangia katika kukuza utalii wa kiutamaduni ambao ni moja ya vyanzo vya mapato kwa wanajamii na taifa kwa ujumla.

Aidha, Naibu Waziri Wambura alisema kuwa wilaya ya Mbulu ni tajiri katika masuala ya utamaduni na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni mdau muhimu katika sekta ya michezo na utamaduni ambazo zinapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha la utamaduni kila mwaka ambapo mwaka huu lilifanyika tarehe 21 hadi 23 mwezi Septemba na inaedelea kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hatua inayopelekea makabila yote kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani ya nchi.

Mbunge huyo aliyataja makabila yanayotokana na makundi makuu manne yanayopatikana wilaya ya Mbulu kuwa ni pamoja na Wairaqw ambao ni jamii ya Wakushi, Wahadzabe jamii ya Khoisan, Wanyiramba na Wanyisanzu jamii ya wabantu na Wadatooga jamii ya Kiniloti.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amemhakikishia Naibu Waziri Wambura kuwa wilaya hiyo itaendelea kuenzi sekta ya utamaduni kwa kuwa na tamasha la utamaduni linalokutanisha makabila yote wilyani humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani ambayo hufanyika mwezi Mei tarehe 21 kila mwaka.

Hatua hiyo inatokana na Tanzania kusaini mkataba wa azimio la Umoja wa Mataifa (UN) kuenzi utamaduni na kuheshimu tamaduni za watu wengine chini unaosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwaka 2002 Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha maadhimisho ya siku ya Utamaduni Duniani kutokana na kuongezeka kwa migogoro, mapigano na kupotea kwa maisha ya watu na mali zao iliyokuwa inatokea sehemu mbalimbali duniani mwishoni mwa miaka ya 1990.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwasili Wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura kuongea na wananchi waliokuwa katika tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Baadhi ya Washiriki wa tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom, wilaya ya Mbullu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akitoka ndani kujionea moja ya nyumba za asili ya Wabantu Wanyiramba na Wanyisanzu iliyopo Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akicheza ngoma na washiriki wa tamasha la utamaduni alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kulia) akipata maelezo ya utamaduni wa kabila la Wadatoga katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasichana wa kabila la Datoga na kusisitiza Watanzania kuenzi utamaduni wetu kwa kuurithisha kwa vijana wetu. Wa nne kushoto ni Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu)

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSTUKIZA HOSPITALI YA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na maafisa wa Jeshi hilo alipowasili Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia), akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, alipofanya ukaguzi wa ghafla katika hospitali hiyo kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha Afya (SACP) Paul Kasabago, alipofanya ukaguzi wa ghafla katika Hospitali ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa, kwa lengo la kuzungumza na uongozi na kujionea namna ya utoaji wa huduma za afya kwa wateja.

ASILIMIA 95 YA MIRADI YA KUBORESHA UMEME WA TANESCO DAR ES SALAAM IMEKAMILIKA:MHANDISI MGAYA


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema, tayari asilimia 95 ya uboreshaji miradi ya umeme katika jiji la Dar es Salaam, imekamilika.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi, Mahende Mgaya, (pichani juu), amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Septemba 27, 2017 na kwamba ifikapo Desemba mwaka huu wa 2017, wananchi na wakazi wa Dar es Salaam wataona ile hali ya kukatika kwa umeme, mara kwa mara imebadilika.

“Tulikuwa na jumla ya miradi mipya 18 ya kuboresha vituo vya umeme jijini Dar es Salaam ili viweze kutoa umeme wa kutosha na wa uhakika, hadi sasa, vituo vinane vimekamilika kabisa na vinafanya kazi, vimebaki vituo 10 ambavyo navyo viko katika hatua za mwisho za kukamilika, na ifikapo Desemba, 2017 vituo vyote 18 vitakuwa vinafanya akzi.” Alitoa hakikisho Mhandisi Mgaya.

Alisema, kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na idadi ya watu jijini Dar es Salaam, mahitaji ya nishati ya umeme nayo yameongezeka na hivyo Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliamua kuchukua hatua za haraka kuboresha vituo vyake vya umeme ikiwa ni pamoja na kujenga vipya ili kukidhi mahitaji halisi ya umeme.

“Wafadhili kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB, World Bank, Finland, na Japan), walijitokeza na kufadhili miradi hiyo.”Alifafanua.

Kazi hiyo ya kuboresha vituo hivyo ambavyo ni pamoja na Mbagala, Kurasini, Kigamboni, Ilala Mchikichini, Kisutu, Mikocheni, Gongolamboto, na maeneo mengine imekuwa ikifanyika tangu miaka miwili iliyopita lakini kutokana na matatizo ya hapa na pale, ikiwa ni pamoja na mapingamizi ya wananchi kuzuia utekelezaji wa miradi hiyo, na wakandarasi, kumepelekea ucheleweshaji.

Maeneeo ambayo yamekuwa yakiathirika zaidi na hali hiyo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ni pamoja na Wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kinodnoni.

“Nichukue fursa hii kuwaomba radhi wananchi, hususan wateja wetu, kutokana na hali hii ya kukatika kwa umeme, lakini napenda pia waelewe kuwa hali hiyo inatokana na kazi ambayo tumekuwa tukiifanya, na mara nyingi umeme tunakata siku za weekend, kwa vile shunguli nyingi za kiofisi zinakuwa zimepungua na hivyo inakuwa fursa nzuri kwetu kufanya kazi.” Alifafanua Mhandisi Mgaya.

Alisema, wananchi wanataka umeme, tena ulio bora na wa uhakika, ndio maana TANSCO imeamua kuchukua hatua madhubuti za kuboresha na kujenga vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme ikiwa ni pamoja na kujenga lini mpya za kusafirisha umeme.“Hatu hizi zote lazima ziwe na changamoto za hapa na pale, lakini kwa kiasi kikubwa TANESCO inaelekea kulitatua tatizo hilo la umeme jijini Dares Salaam na Mkuranga.”. Alisisitiza.

Wakandarasi na mafundi wa TANESCO wakiwa kazini Moja ya vituo ambavyo vimefungwa mitambo mipya ili kuboresha upatikanaji wa umeme jijini Dar es Salaam. Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kisutu.

MHE KINGU AWAOMBEA MAJI WAKAZI WA JIMBONI KWA LISSU


Na Mathias Canal, Singida

Pamoja na Changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika Jimbo la Singida Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida lakini uhaba wa  upatikanaji wa huduma ya maji ni kikwaz kikubwa kwa wananchi kwani wanatumia umbali na muda mrefu kutafuta maji.


Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu ametoa ombi hilo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.

Mhe Kingu alisema kuwa Jimbo lake lina changamoto ya maji ambayo kwa kiasi kikubwa serikali inaendeleza juhudi za kuzitatua, huku akisema kuwa katika Jimbo jirani la Singida Mashariki linaloongozwa na Mhe Tundu Lissu hali ni mbaya zaidi katika upatikanaji wa miundombinu ya maji kwa wananchi wake.

Alisema kuwa hivi karibuni alipita katika jimbo hilo na kujionea adha inayowakumba wananchi jambo amablo lilimfanya kujipanga kuwaombea maji wananchi hao katika kipindi cha Bunge lijalo. Alisema kuwa wananchi hao wamebaki wakiwa utadhani hawana muwakilishi wa Jimbo kwa kipindi cha miaka 10 jambo ambalo linafanya kuteseka na huduma za utafutaji maji kwa kutumia muda mwingi na umbali mrefu.

Aidha, Mhe kingu alisema kuwa pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji Katika Jimbo la Singida Mashariki lakini pia jimbo hilo linakumbwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu ambayo ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa, Nyumba za walimu, Maabara, Matundu ya vyoo na mabweni.

Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha mkakati wa pamoja wa kuanzisha Mfuko wa Elimu Ikungi utakaowashirikisha wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi waweze kuongeza ufaulu.

Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Singida ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji upatikanaji wa maji.

Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Ikungi mara baada ya kupita Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielekea Manispaa ya Singida kwa ajili ya mapumziko, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) akimfatilia kwa makini Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Wilaya ya Ikungi, Mwingine ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Elieza

MAKAMISHNA WA UPELELEZI WA KODI AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR


Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala akisalimiana na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala kabla ya kuanza kwa mkutano wa watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
Washiriki wa mkutano huo wakianza kwa kumtanguliza Mungu kwanza. 
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa akisoma hotuba ya Kamishna Mkuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa makamshina na watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya watendaji waandamizi wa mamlaka hiyo wakati wa mapumziko ya Mkutano wa Mamlaka za mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofunguliwa jijini Dar es Salaam leo Septemba 27 2017. Kutokea (kushoto) ni Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi, Salim Kessi, Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala. 
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo. 
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo. 
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo. 

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndg. Phili Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe  Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini  Dar es Salaam. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na nyuma ya Makamu  wa Rais ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza wa Wakilishi la Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar ss Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Rodrick Mpogolo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Septemba 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.