Katibu wa wizara ya nguvu kazi Maryam El-Maawy ambaye alishambuliwa na alshabab amefariki akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
Ikulu ya rais nchini Kenya imethibitisha kifo cha El-Maawy.
Bi El Maawy alifariki nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu kufuatia shambulio la wapiganaji wa al-Shabab manmo julai 13.
Msemaji wa Ikuku manoah Esipisu alithibitishja kifi cha bi Maawy kwa taifa lakini akasema kuwa maelezo yatatolewa baadaye.
Alshabab walimpiga risasi na kumjeruhi katibu hiyo katika bega na miguu baada ya kumteka nmyara katika eneo la Milihoi katika baranara ya Mpeketoni Lamu.
Mpwa wake ambaye alikuwa akijifunza urubani na ambaye walikuwa pamoja alifariki wakati wa shambulio hilo lakini Bi Maawy aliokolewa na kundi la wanajeshi wa Kenya KDF pamoja na wale wa GSU.
Kundi la maafisa wa usalama lilimkimbiza katika hospitali ya Mpeketoni.
- Al-Shabab lakiri kuvamia kituo cha polisi Kenya
- Al-Shabab washambulia mji wa El Wak karibu na mpaka wa Kenya
- Kifo cha waziri Somalia: Mkaguzi wa hesabu afutwa kazi
- Filamu ya Kenya yashinda tuzo ya Oscars
Baadaye alisafirishwa hadi mjini Nairobi kwa matibabu.
Wakati wa shambulio hilo, wapiganaji hao walidhibiti gari alimokuwa katibu huyo ambalo lilikuwa na watu sita kabla ya kutoroka katika kichaka.
Ndege ya KDF ililifuata gari hilo na kufanikiwa kumuokoa afisa huyo.
Maafisa wawili wa polisi pia walifariki wakati wa shambulio hilo huku wengine wawili wakitekwa na wapiganaji hao.
Siku ya shambulio hilo, katibu huyo alikuwa amehudhuria mkutano kuhusu bandari ya Lamu, barabara ya Sudan kusini, Ethiopia katika kituo cha Huduma mjini Lamu akielekea Witu.
No comments:
Post a Comment