Wednesday, September 27

Moto nyumba za polisi wadhibitiwa


Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema familia 13 zenye watu 44 zimeathiriwa kwa moto ulioibuka kwenye nyumba za askari polisi usiku huu.
Amesema taarifa za awali zinasema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme na uchunguzi unaendelea.
Gambo amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa  katika tukio hilo.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba amesema moto huo umeshadhibitiwa.                       
“Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Amesema taarifa kuhusu tukio hilo zimewafikia kwa kuchelewa.                       
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema hali ni shwari na hakuna wizi uliotokea.
Amesema tukio hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia  walioathiriwa.

No comments:

Post a Comment