Saturday, June 24

Mtoto atunukiwa zawadi ya kusafiri kwa ndege maisha yake yote


Shirika la ndege la binafsi nchini India limemtunuku safari za bure mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege moja ya shirika hilo iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea India.
Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto wakati ndege hiyo ikiwa umbali wa futi 35,000 angani.
 Kutokana na tukio hilo, shirika hilo lilimpa zawadi ya kudumu maishani, ambayo itakuwa ni kusafiri bure kwa ndege ya shirika hilo katika maisha yake yote.
Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege hiyo aina ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi ya Mumbai.
Shirika hilo liliiambia BBC kuwa mama na mtoto wake walikuwa katika afya nzuri.
Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.
Shirika hilo lilisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege zake.
Tukio kama hilo lilitokea nchini Uturuki ambapo mtoto wa kike alizaliwa katika ndege ya Shirika la Turkey Airline, Aprili mwaka huu.

Sirro aibukia Moshi mauaji ya Kibiti


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema mauaji ya polisi, viongozi na raia katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Ikwiriri ni ya muda na kusisitiza majibu yake yako mbioni kupatikana.
Sirro ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi) katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wakati wa kufunga mafunzo ya upandishaji vyeo kwa maofisa na askari 222 wa Jeshi la Uhamiaji nchini.
Kauli ya Sirro imekuja huku kukiwa na mfululizo wa mauaji ya polisi na raia katika maeneo hayo ambapo zaidi ya watu 35 wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwamo polisi 13.
Hadi sasa, licha ya polisi kufanya operesheni kubwa katika maeneo hayo, bado halijaweza kubaini chanzo cha mauaji hayo na kwa nini wanawalenga polisi na baadhi ya watu na nani wanayatekeleza.
Tukio la hivi karibuni kabisa lililotokea Jumatano iliyopita, ambapo watu wasiojulikana waliwashambulia kwa risasi na kuwaua polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani huko Kibiti.
Akizungumza katika sherehe za kuhitimu mafunzo kwa maofisa na askari hao 222 wa Jeshi la Uhamiaji, Sirro amesema japokuwa nchi ni salama, lakini inakabiliwa na kitisho cha usalama eneo hilo.
“Tuna shida Kibiti Ikwiriri lakini wanasema sisi ni wengi wao ni wachache. Tusikubali hata siku moja makabila yetu, madhehebu yetu, majimbo yetu yatugawanyishe,” amesema Sirro na kuongeza;-.
“Umoja wetu ndio nguvu yetu. Suala la Kibiti ni la muda mfupi. Tunakwenda na tutapata majibu. Hatutakubali kikundi cha watu wachache wafanye Kibiti, Ikwiriri, Rufiji yasikalike,”.
Akizungumzia changamoto zinazolikabili Jeshi la Uhamiaji, Sirro aliyekuwa mgeni rasmi amesema moja ya changamoto kubwa ni uingiaji wa wahamiaji haramu wanaopitia njia zisizo rasmi kuingia nchini.
“Hili litawezekana kwa kuimarisha intelijensia. Mnapopanda vyeo sio mfurahie tu kupanda cheo mjue majukumu yanaongezeka pia. Idadi ya mnaoenda kuwaongoza sasa itaongezeka,”amesema Sirro.
“Kazi yenu Uhamiaji na sisi polisi hazitofautiani sana na mara nyingi tumekuwa tukifanya kazi za operesheni pamoja. Changamoto tunayokutana nayo ni usimamizi wa kazi”alisisitiza na kuongeza;-
“Askari anakosea huchukui hatua. Konstebo anafikia mahali anamtuma Koplo amletee soda na anakimbia anakwenda kumletea soda. Mnaona ni sawa hii?”alihoji na kujibiwa “Hapana”.
“Heshima yetu sisi askari ni kutokuwa waoga na unakuwa sio muoga kwa sababu kazi unaifahamu, unakuwa sio muoga kwa sababu unatii sheria na unasimamia sheria na hubabaiki,”amesema.
“Ninawaelekeza suala la uoga, suala la ulegelege katika awamu hii tusiipe nafasi,”ameongeza kusema na kusisitiza maofisa hao kufanya kazi kwa weledi pasipo kuwasumbua au kuwazungusha wananchi.
Kamishina Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mafunzo hayo ni ya kwanza katika historia ya jeshi lake baada ya Jeshi hilo kufanya maboresho ya kimuundo na sheria.
“Jeshi la Uhamiaji limefanya maboresho yakiwamo ya kimuundo na sheria ili kuliingiza Jeshi la Uhamiaji katika tume ya polisi na Magereza. Hatua hii imechangia kuwepo kwa mabadiliko,”amesema.
“Uhamiaji lina askari na watumishi wasiozidi 3,000, hawatoshi kutokana na ongezeko la majukumu ya uhamiaji. Ili kufanya kazi kwa ufanisi linalihitaji kuwa na askari wasiopungua 10,000,”amesisitiza.
Kamishina Jenerali hiyo amesema Taifa kwa sasa linakabiliwa na changamoto ya wahamiaji haramu wanaoingia kupitia njia zisizo rasmi, lakini akasema wanapata ushirikiano mkubwa toka polisi.

MAVUNDE ATOA RAI KWA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA KUSOGEZA HUDUMA ZAO VIJIJINI ILI KUWAHUDUMIA WAKULIMA


 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, wa kushoto  akiwa katika uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.


Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima ikiwemo mikopo ya fedha taslimu,mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.


Mavunde amewataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.


Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.

MUFTI MKUU WA TANZANIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA AJILI YA SWALA YA EID EL FITRI


Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheakh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na waliompokea katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  akiteta jambo na Shekh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Gari maalumu kwa ajili ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Msafara wa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali   ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
Gwaride la vijana katika kumpokea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo litakalotumika kama Madrasa.
Mapokezi mwakubwa kwa Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Jengo la Ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai ambalo Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  amefika kwa ajili ya uzinduzi wake.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Furaha ya kutembelewa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali  akizindua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akiondoka baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Masjid Shafii kwa ajili ya uzinduzi.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akikata utepe kuuzindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Aliakizindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa Bakwata wilaya ya Hai,Mwl Mohamed Mbowe akisoma risala mbele ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali wakati wa uzinduzi rasmi wa msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akipokea risala hiyo
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ali akizungumza mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSA AZINDUA JUMUIYA YA WATOA HUDUMA ZA MAFUTA NA GESI TANZANIA (ATOGS)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha picha alichokabidhiwa na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 
 Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Lengo la Jumuiya hiyo ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo. Picha na Frank Shija - MAELEZO