Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde, wa kushoto akiwa katika uzinduzi wa benki ya Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mh Anthony Peter Mavunde amezitaka benki na Taasisi za Fedha kusogeza huduma zao katika maeneo ya Vijijini ili kuwafikia watanzania wengi ambao wanajihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile kilimo na Ufugaji.
Mavunde alitoa rai hiyo jana wakati wa uzinduzi wa benki ya Yetu Microfinance Bank PLC katika kata ya Mngeta,Wilaya ya Kilombero,Mkoani Morogoro kwa kuzitaka Taasisi hizo za fedha zisaidie katika utoaji wa mikopo nafuu kwa wakulima ikiwemo mikopo ya fedha taslimu,mikopo ya zana za kilimo na mashine za uchakataji wa mazao kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali kupitia uchumi wa Viwanda.
Mavunde amewataka wananchi wa kata ya Mngeta kuitumia hiyo fursa kuboresha kilimo chao kwa kulima kwa njia za kisasa na pia kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uchakataji mazao.
Aidha,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Bwana Millinga alimuelezea Naibu waziri kwamba wameshaanza mchakato wa kuwakopesha wakulima mashine za uchakataji wa mazao na watatanua wigo zaidi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment