Sunday, August 13

Japan imepeleka mtambo wa kutibua makombora

Mtambo wa kutibua makombora wa Marekani Thaad ukipelekwa Korea Kusini
Image captionMtambo wa kutibua makombora wa Marekani Thaad ukipelekwa Korea Kusini
Japan imepeleka mtambo wa kutibua makombora magharibi mwa taifa hilo kufuatia tishio la Korea Kaskazini kwamba itarusha kombora la masafa marefu katika kisiwa cha Guam nchini Marekani.
Mtambo huo kwa Jina PAC3 (Patriot Advanced Capability-3) umepelekwa katika eneo la shimane, Hiroshima na Kochi ambapo Pyongyang inasema kombora lake litapaa kabla ya kuanguka katika maji ya Guam.
Mtambo wa kutibua makombora wa Marekani Thaad ukipelekwa Korea Kusini
Image captionMtambo wa kutibua makombora wa Marekani Thaad ukipelekwa Korea Kusini
Jeshi la kulinda baharini la Japan limeripotiwa kutuma mtambo wa kutibua makombora katika bahari ya Japan likiwa na mfumo wa kufuatilia makombora ya masafa marefu.

Tamko la Trump kuhusu kuingilia kijeshi Venezuela lashutumiwa

Venezuela's Presidente Nicolas Maduro gestures as he speaks during a session of the National Constituent AssemblyHaki miliki ya pichaREUTERS
Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Amerik kusini Mercosur umemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kusema kwamba anafikiria uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Venezuela.
Argentina imesema mashauriano na diplomasia ndizo njia pekee za kuendeleza demokrasia Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela amesema tamko la Trump lilikuwa la uchokozi na la kuikosea heshima nchi hiyo na kwamba linatishia kuvuruga uthabiti Amerika kusini.
Maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambayo yamekuwa yakiendelea tangu Aprili yamesababisha vifo vya watu 120.
Bunge jipya shirikishi la Rais Nicolas Maduro, ambalo lina mamlaka ya kufanyia marekebisho katiba na linaweza kubatilisha maamuzi ya bunge la kawaida linalodhibitiwa na upinzani, limeshutumiwa sana na wengi.
Mercosur - ambayo hujumuisha Argentina, Brazil, Paraguay na Uruguay - ilisimamisha uanachama cha Venezuela wiki iliyopita.
Nchi nyingine za Amerika kusini pia zimemshutumu Trump, zikiwemo Mexico, Colombia na Peru, na kueleza kwamba tamko hilo la Trump linaenda kinyume na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Peru imekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Maduro.
Ijumaa, Peru ilimfukuza balozi wa Venezuela baada ya serikali ya Venezuela kutoa jibu lisilo la kuridhisha kwa nchi za kanda hiyo ikijitetea kuhusu bunge shirikishi.
Opposition activists protest in CaracasHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski ametoa wito kwa Maduro kujiuzulu na kumuita dikteta.
IJumaa jioni, Bw Trump aliambia wanahabari kwamba Marekani ina "njia nyingi za kutumia Venezuela, ikiwemo kuingilia kijeshi iwapo hali itabidi".
"Watu wanateseka huko na wanafariki dunia," aliongeza.
Marekani ilimuwekea vikwazo Maduro hivi majuzi na kumuita dikteta.
man protests against maduroHaki miliki ya pichaJUAN BARRETO
Image captionMaandamano yameshuhudiwa Venezuela tangu Aprili

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria asema aendelea kupata nafuu

BuhariHaki miliki ya pichaRAIS WA NIGERIA / BAYO OMOBORIOWO
Image captionPicha iliyopakiwa kwenye akaunti ya Twitter ya rais Buhari @NGRPresident ilimuonesha akiwa anatabasamu akiwa na kadi ya kumtakia uponaji wa haraka
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ambaye anatibiwa jijini London kwa ugonjwa ambao bado haujatajwa, amezima kimya kirefu na kuzungumza.
Kwa njia ya taarifa, Bw Buhari amesema kuwa "matibabu yanendelea vyema, huku afya yake ikiimarika pakubwa".
Hata hivyo, Rais ameongeza kusema kuwa, hata ingawa anajihisi tayari kurejea nyumbani, madkatari bado wanamhudumia, huku akisema sasa ameanza kuzoea kufuata amri na maagizo badala ya kutoa amri
Kimya chake cha muda mrefu, kimezua malumbano kuwa, anafaa arejee Nigeria ama ajiuzulu kiti cha urais.
Uvumi kuhusiana na afya ya Bwana Buhari, umedumu kwa muda mrefu, tangu alipokwenda jijini London kwa matibabu, mwezi Juni mwaka jana.
Makamu wa Rais Yemi Osinbajo, amekuwa akitawala Nigeria muda huu wote Buhari akiendelea na matibabu.

Uchaguzi Kenya: Kofi Annan amtaka Odinga kutumia njia za kisheria

Kofi Annan

Image captionKofi Annan alikuwa mpatanishi mkuu mzozo wa baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, ametoa wito kwa walioshindwa kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki.
Bw Annan alikuwa mpatanishi mkuu baada ya ghasia kuzuka baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 uliokumbwa na utata.
Bw Mwai Kibaki alitangazwa mshindi wakati huo lakini Bw Raila Odinga na chama chake cha ODM wakapinga matokeo hayo.
Katibu mkuu huyo wa zamani wa UN amempongeza Bw Kenyatta kwa ushindi wake na pia akamsifu Bw Odinga kwa kuendesha kampeni yake kwa njia ya amani.
"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," amesema Dkt Annan kupitia taarifa.
"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi awali."
Upinzani umekuwa ukidai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na matokeo kuchakachuliwa kumfaa Rais Kenyatta.
Alhamisi, muungano wa upinzani National Super Alliance (NASA) ulidai Bw Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na kuitaka tume hiyo kumtangaza kuwa mshindi.
Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambayo ni asilimia 54.27 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74.
Maajenti wakuu wa NASA waliondoka ghafla kikao cha tume hiyo cha kuafikiana kuhusu matokeo hayo kabla ya kutangazwa kwa Bw Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi huo Ijumaa usiku.
Naibu ajenti mkuu wa muungano huo James Orengo, amesema muungano huo hautaenda kortini. Amesema hawana imani na idara ya mahakama kwamba itashughulikia malalamiko yao kwa njia ya haki bila mapendeleo.
Bw Annan pia ametoa wito kwa Rais Kenyatta, ambaye alitangazwa mshindi wa urais Ijumaa afanye juhudi kuunganisha tena taifa.
Kiongozi huyo amesikitishwa na mauaji ambayo yametokea kwenye makabiliano kati ya waandamanaji waliokuwa wanapinga matokeo na polisi.
Amesema anatumai hakutatokea mauaji zaidi.
"Amani, uthabiti na ustawi vinategemea viongozi wa kisiasa Kenya. Wanafaa kuwa makini sana katika mambo wanayosema na vitendo vyao katika hali hii ya sasa. Nawaomba wawajibike."
Naibu rais na mwakilishi mkuu wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini pia ameutaka upinzani kutumia njia za kisheria kufuatilia malalamiko yao kuhusu uchaguzi.
Uhuru Kenyatta kushoto) na Mpinzani wake Raila Odinga (kulia)
Image captionUhuru Kenyatta kushoto) na Mpinzani wake Raila Odinga (kulia)
"Sawa na ulivyofanya Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya unatarajia upinzani uheshimu matokeo na ktuumia njia za kisheria zilizopo kukata rufaa na kuwasilisha malalamiko," amesema kupitia taarifa.
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani katika mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi, katika katika maeneo ya Homa Bay, Migori na Kisumu ambayo ni ngome ya Bw Odinga magharibi mwa Kenya.
Mwanamke akijikinga KiberaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGhasia zilitokea pia mtaa wa Kibera, Nairobi
Mashirika ya kutetea haki yanasema watu kadha wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wengi wanauguza majeraha hospitalini.
MathareHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWafuasi wa upinzani wamekuwa wakikabiliana na polisi mtaa wa Mathare na Kibera jijini Nairobi na eneo la Kisumu
Tume ya Kitaifa la Haki za Kibinadamu ilisema idadi ya waliokuwa wameuawa kufikia Jumamosi jioni ilikuwa imefikia 24, ingawa idadi hiyo haijathibitishwa na shirika jingine.
Kamishna wa eneo la Nyanza Wilson Njenga Jumamosi alithibitisha kwamba mtu mmoja alifariki eneo la Maseno kilomita takriban 20 kutoka mji wa Kisumu.
Jumamosi, msichana wa miaka 10 pia alifariki baada ya kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya waandamanaji na polisi katika mtaa wa Mathare Kaskazini jijini Nairobi.
Serikali imesema hakuna mwandamanaji aliyeuawa na maafisa wa polisi na kwamba polisi hawajatumia risasi halisi kuwakabili waandamanaji.
Mwaka 2007, watu zaidi ya 1,000 walifariki na wengine 600,000 wakafurushwa makwao wakati wa ghasia za kikabila zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Uchaguzi Kenya: Upinzani waapa ''kubadilisha'' matokeo ya uchaguzi

Waandamanaji wa upinzani wamekuwa wakikabiliana na maafisa wa polisi katika mtaa wa mabanda wa Mathare jijini NairobiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWaandamanaji wa upinzani wamekuwa wakikabiliana na maafisa wa polisi katika mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi
Upinzani nchini Kenya umeishutumu serikali kwa kutekeleza 'ugaidi' dhidi ya raia wake na kuapa kubadilisha matokeo ya uchaguzi mkuu walioyataja kuwa ya 'uwongo'.
Afisa mwandamizi katika upinzani huo James Orengo amesisitiza kuwa hawatakwenda mahakamani ili kuafikia lengo lao.
Amewataka wafuasi wao kuwa watulivu na kujilinda dhidi ya 'madhara' ya serikali.
Bwana Orengo amedai kwamba takriban watu 100 ikiwemo watoto wameuawa na vikosi vya usalama vya Kenya huku miili yao ikitiwa ndani ya mifuko ya plastiki.
Alionyesha vibweta vya risasi lakini akashindwa kutoa ushahidi kuthibitisha madai hayo.
Matokeo rasmi yalionyesha kuwa rais Uhuru kenyatta alipata asilimia 54.3 ya kura huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akitaja matokeo hayo kama ''mchezo mkubwa''.
''Walijua kwamba wataiba kura .Walijua kwamba watu hawatafurahia kwa hivyo vifaa vyote vya kukabiliana na ghasia viliwekwa tayari'', alisema Orengo.
Huku ikiwa waandishi hawajaona ushahidi wa kuthibitisha mauaji hayo yanayodaiwa na upinzani, takriban watu 11 wameripotiwa kuuawa na polisi katika maeneo yanayomuunga mkono Raila Odinga.
Chumba cha kuhifadhi maiti cha kaunti ya Nairobi kilipokea miili minane.
Polisi katika eneo la dandora wakijaribu kuzima moto uliowashwa na waandamanaji
Image captionPolisi katika eneo la dandora wakijaribu kuzima moto uliowashwa na waandamanaji
Watu wengine watatu waliripotiwa kuuawa katika kisa chengine, ikiwemo mtoto wa miaka tisa aliyepigwa na risasi kwa bahati mbaya katika mtaa wa mabanda wa Mathare uliopo Jiji Nairobi.
Mtu moja pia aliuawa mjini Kisumu , ambayo ni ngome ya upinzani na eneo la ghasia za kikabilia wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, wakati ambapo takriban watu 1200 walifariki na wengine 600,000 kuachwa bila makao.
Mapema shirika la wangalizi wa uchaguzi ELOG ambalo lilikuwa na waangalizi 8,300 lilisema kuwa matokeo yake yalimpatia rais Kenyatta asilimia 54 ya kura hizo.
Lakini Bwana Orengo amekosoa uhuru wa shirika hilo.
Awali kaimu waziri wa usalama wa ndani nchini k
Kaimu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi
Image captionKaimu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi
Kenya Fred Matiangi aliwataka Wakenya kurudi katika maisha yao ya kawaida na kuwataka wale wanaotumia mitandao ya kijamii kuitumia vizuri.
Rais Kenyatta ameomba kuwepo na amani.
''Tumeona matokeo ya ghasia za baada ya uchaguzi , Najua kwamba hakuna Mkenya mwengine ambaye angependa kurudi katika ghasia hizo'', alisema.
Kabla ya matokeo hayo kutangazwa bwana Raila Odinga aliwaomba wafuasi wake kuwa watulivu, lakini akongezea kuwa hawezi kumdhibiti mtu yeyote na kwamba watu wanataka kuona haki.
Shirika la haki za kibinaadamu la Amnesty International limeitaka serikali kuchunguza mauaji hayo.

Kiongozi wa zamani wa al-Shabaab ajisalimisha Somalia

Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Image captionBwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa mwanachama wa cheo cha juu wa kundi la al-Shabaab Mukhtar Robow amejisalimsha kwa serikali.
Alijisalimisha pamoja na wapiganaji wake katika mji ulio kusini magharibu wa Hudur.
Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Mwezi Juni, Marekani iliondoa zawadi ya dola milioni tano kwa bwana Robow ambaye bado anaaminiwa kuendelea na shughuli zake kama mwanamgambo.
Al Shabab bado inathibiti maeneo makubwa ya Somalia na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Kenya.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ZIARANI WILAYA YA KASKAZINI "B" MKOA WA KASKAZINI UNGUJA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pia Kaimu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Ali Abeid Karume wakati alipowasili katika ukaguzi wa maendeleo ya Kiwanda cha Sukari cha Mahonda na kupata maelezo mbali mbali kutoka kwa Wasimamizi wa Kiwanda hicho Kampuni ya ETG  alipofanya ziara katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Nd,Tushar Mehta  alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Mawasiliano katika Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Fatma Salum Ali (kulia) wa  Kampuni ya ETG inayoendesha Kiwanda hicho wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Ndg. Tushar Mehta  (wa pili kushoto) alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mkuu wa mradi   katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Bw. Mahesh  Patel (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed.
Picha na IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa takatifu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017. Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitakiana amani na watawa wakati wa Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakijumuika na waumini wengine kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipata picha ya kumbukumbu na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Padre Vicent na baadhi ya wanafunzi shule ya Sekondari ya St. Joseph baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017

DED ILEJE AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA HALMASHAURI YAKE


Na Fredy Mgunda, Ileje: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi amefanya ziara ya kushtukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015/20 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya 
mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni 
wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6 wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawaugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mfereji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo.

Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yao.

Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo, alimwagiza mtendaji wa kata ya mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kuwa, kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani
 Songwe, Haji Mnasi akikagua mradi wa mfereji mkubwa
 wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa 
wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na
wananchi wakati wa ukaguzi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo walipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

"Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.