Sunday, August 13

Tamko la Trump kuhusu kuingilia kijeshi Venezuela lashutumiwa

Venezuela's Presidente Nicolas Maduro gestures as he speaks during a session of the National Constituent AssemblyHaki miliki ya pichaREUTERS
Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Amerik kusini Mercosur umemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kusema kwamba anafikiria uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Venezuela.
Argentina imesema mashauriano na diplomasia ndizo njia pekee za kuendeleza demokrasia Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela amesema tamko la Trump lilikuwa la uchokozi na la kuikosea heshima nchi hiyo na kwamba linatishia kuvuruga uthabiti Amerika kusini.
Maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambayo yamekuwa yakiendelea tangu Aprili yamesababisha vifo vya watu 120.
Bunge jipya shirikishi la Rais Nicolas Maduro, ambalo lina mamlaka ya kufanyia marekebisho katiba na linaweza kubatilisha maamuzi ya bunge la kawaida linalodhibitiwa na upinzani, limeshutumiwa sana na wengi.
Mercosur - ambayo hujumuisha Argentina, Brazil, Paraguay na Uruguay - ilisimamisha uanachama cha Venezuela wiki iliyopita.
Nchi nyingine za Amerika kusini pia zimemshutumu Trump, zikiwemo Mexico, Colombia na Peru, na kueleza kwamba tamko hilo la Trump linaenda kinyume na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Peru imekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Maduro.
Ijumaa, Peru ilimfukuza balozi wa Venezuela baada ya serikali ya Venezuela kutoa jibu lisilo la kuridhisha kwa nchi za kanda hiyo ikijitetea kuhusu bunge shirikishi.
Opposition activists protest in CaracasHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski ametoa wito kwa Maduro kujiuzulu na kumuita dikteta.
IJumaa jioni, Bw Trump aliambia wanahabari kwamba Marekani ina "njia nyingi za kutumia Venezuela, ikiwemo kuingilia kijeshi iwapo hali itabidi".
"Watu wanateseka huko na wanafariki dunia," aliongeza.
Marekani ilimuwekea vikwazo Maduro hivi majuzi na kumuita dikteta.
man protests against maduroHaki miliki ya pichaJUAN BARRETO
Image captionMaandamano yameshuhudiwa Venezuela tangu Aprili

No comments:

Post a Comment