Friday, August 18

TIB CORPORATE BANK KTK JUKWAA LA BIASHARA TANGA


Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe kulia akilakiwa na wajumbe wa Jukwaa hilo wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TSN Dokta Jimmy Yonazi wanne kushoto ni MD wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege na wakwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa. 

TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara ,Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta maendeleo.

TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali KTK Mkoa wa tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities).

TIB Corporate Bank inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati,dhamana za kibenki( bank guarantee),ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni,uwekezaji katika hati fungani,( treasury bills & Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka

Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

UCSAF IMESAINI MAKUBALIANO NA AIRTEL KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI


UCSAF imesaini makubaliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na makampuni mengine ya simu nchini kwa lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini. Hafla ma makubaliano hayo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam,

"mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Airtel tunasaini mkataba huu kwa lengo lakuendelea kutimiza mawasiliano kwa wote nchini

Singano alisema kuwa "uwepo wa mawasiliano haya vijijini utasaidia hata kutimiza malengo mbalimbali ambayo serikali imejiwekea katika kupanua uchumi wa nchi kwa ujumla, elimu, afya, uboreshwaji wa kilimo pamoja na huduma za kibenki kwa maeneo ambayo yako pembezoni.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.

 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017

ZAIDI YA MILIONI 90 KUKARABATI SHULE ZA MSINGI KATA YA MAKUBURI-KUBENEA


 Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
 Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na Wanafunziwa Darasa la Tatu wa Shule ya Msingi Makuburi wakati alipokwenda kukagua ukarabati wa Madarasa wa shule hiyo unaotokana na mfuko wa jimbo na fedha za Halmashauri ambapo jumla ya fedha zaidi ya Milioni 88 zimetolewa na Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya ubungo na Milioni 17 Kutoka Mfuko wa Jimbo wa  mbunge huyo
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaaa wa Mwongozo , James Gointamile (CCM)   akimuonesha Mbunge wa Ubungo , Saed Kubenea (CHADEMA), Baadhi ya Vigae ambavyo vilikuwa vinavuja katika madarasa matatu ya Shule ya Msingi Makuburi mara baada ya Mbunge Huyo kutoa Milioni 17 kwa ajili ya kununua bati mpya za kisasa kuezeka shule hiyo.
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akionesha Sehemu ya Paa ambayo inavuja, inatarajiwa kuzibwa hivi karibuni na Mabati amabyo yametolewa kwenye fedha za mfuko wa Jimbo
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiangalia sehemu ya Shimo la choo cha Matundu 12 kinachotaraji kujengwa na fedha za Halmashauri ya Manispaa ya ubungo mara baada ya Choo cha shule hiyo kutokuwa katika hali nzuri
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Watendaji wa Mtaa na Diwani wa kata ya Makubuli, Hanifa Chiwili kwenye darasa ambalo liko juu ya chemba ya kuhifadhia maji ya mvua ya shule hiyo hili kuzuia Mmong'onyoko kwa Madarasa Mengine
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akizungumza na Walimu wa shule ya Msingi Makuburi mara baada ya kutembelea chumba cha Walimu.

 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Akiwa katika korido za shule msingi Makuburi
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makuburi

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WATATU NA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU ARDHI

Magufuli ateua maprofesa watatu kuongoza taasisi



Rais Magufuli
Rais Maguful

Walimu 15 wafukuzwa kazi


Chamwino. Walimu 15 katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wamefukuzwa kazi baada ya kubainika kuwa ni watoro kazini.
Tume ya Utumishi na Ajira ya Walimu (TSC0 wilayani humo imefikia uamuzi huo baada ya kushughulikia mashtaka dhidi ya watumishi hao yaliyowasilishwa kwao.
Katibu wa TSC Wilaya ya Chamwino, Khalid Shaaban amesema uamuzi huo una gharama, lakini hakuna namna nyingine zaidi kufanya hivyo ili kuchochea uwepo wa nidhamu kwa walimu.

Mahakama yaambiwa Manji ni mgonjwa, kesi yaahirishwa hadi Agosti 25



Mfanyabiashara Yussuf Manji 

Mfanyabiashara Yussuf Manji  


Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yussuf Manji (41) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na wenzake watatu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anaumwa na amepewa mapumziko ya siku mbili.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Agosti 18 na Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa.
Wakili Wilson amedai mahakamani hapo kuwa alipata taarifa hizo za kuwa Manji anaumwa na amepewa mapumziko ya simu mbili toka kwa askari Magereza.
Hata hivyo, amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa kutajwa na upelelezi wake hadi sasa bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 25, 2017.
Manji na  wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vya kushonea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni na mihuri.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).

Uamuzi pingamizi kesi ya Wema kutolewa Agosti 31


Dar es Salaam. Uamuzi wa kupokea au kutopokea   kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu utatolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwisho wa mwezi huu.
Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema uamuzi huo ulipaswa autoe leo, lakini bado kuna tafiti anazifanya, hajakamilisha hivyo aliuahirisha hadi Agosti 31,2017.
Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13, 2017.
Uamuzi huo umefuatia baada ya shahidi huyo ambaye ni mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima ambaye alipima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi, kuomba kuvitoa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.
 Mulima kupitia wakili wa Serikali, Costantine Kakula aliomba kuitoa bahasha iliyofungwa juu yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya maabara 291 ya 2017  ambayo ndani yake kulikuwa na msokoto na vipisi viwili vya bangi mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.
Hata hivyo wakili wa Wema, Tundu Lissu alipinga kisipokewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.
Kutokana na hoja hizo, Hakimu Simba alisema Agosti 18, 2017 atatoa uamuzi juu ya hoja hizo na kesi hiyo pia inaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Watumishi wa Umma Watakiwa Kubadilika


Frank Mvungi - Maelezo.

Serikali imewataka watumishi wa umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo yanayofanywa kwa kushirikina na wadau wa maendeleo.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa mipango,bajeti na kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Katavi, Rukwa na kigoma, Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya serika ni kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika kuwahudumia wananchi.

“Mfumo huu sio wa majaribio hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika mkoa na halmashuri na kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi ambao hawakushiriki katika mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji uwajibikaji wa pamoja” alisisitiza Chote.

Akifafanua Dkt. Chote amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa lakutumia weledi na ujuzi waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo yao ili azma ya serikali kutoa huduma bora itime. 

Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago amesema kuwa vituo zaidi ya elfu 22,000 vya kutolea huduma vitaunganishwa katika mfumo huo wa Kitaifa hali itakayofanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kwa kuwa na mifumo bora yakutolea huduma.

“Nashukuru PS3 kwa ushirikiano uliopo kati yake na TAMISEMI na umewezesha kutekelezwa kwa miradi yenye tija hasa kwa wananch”.Alisisitiza Rwamiago.

Akifafanua Rwamigo amesema kuwa watumishi katika Mikoa na Halmashuri lazima waoneshe kwa vitendo namna tofauti ya kutekelza majukumu yao kwa kutumia mfumo huo wa kielektroniki ulioboreshwa ambao ni (web based).

Mradi wa PS3 unalenga kushirikiana na Serikali katika kuboresha matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwemo fedha, rasilimali watu na mifumo katika ngazi ya kutolea huduma kama vile vituo vya Afya,Zahanati,Hosipitali na katika sekta ya elimu.

Kutokana na maboresho na kurahisishwa kwa Teknolojia,mfumo huu mpya wa PlanRep umefanywa kuwa ‘web based’ hivyo utawezesha Halmashuri kuingiza taarifa za Mipango na Bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa kwenye mfumo mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI na hatimaye kuingizwa kwenye bajeti kuu ya mwaka husika.
 Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma akisisitiza  jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.
 Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akizungumzia umuhimu wa mfumo huo katika kuleta mageuzi ya kiutendaji kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
 Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka PS3 bw. Desderi Wengaa akizungumza wakati wa hafla ya Kufunga mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma. (Picha na Frank mvungi-Maelezo)

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII


Na Pamela Mollel-Arusha 

WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama
amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini
katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza
Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake
kupitia msanii Mrisho Mpoto. 

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane. 

Alisema kuwa wasanii wananafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na
kuendelea kuitangaza Tanzania endapo watatumiwa kama mabalozi kupitia
umaarufu wao jambo ambalo litasaidia pia kuiingizia nchi kipato kupitia
watalii. 

Naye Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto aliwapongeza watanzania kuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao katika maonesho hayo ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo hivyo kuwaandaa watoto hao kuwa wahifadhi kwa baadae. 

“Mfano mzuri ni hili la punguzo la shilingi elfu 50 lililotolewa ili
watanzania waweze kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tumeona watu
walivyochangamkia na kwenda kutembelea Ngorongoro hivyo ni jambo zuri
na la kupongezwa kwa watanzania na ninaomba waendelee kutembelea
hifadhi zetu”alisema Mpoto. 

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter
Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania. 

Aidha aliwaomba watanzania wengine kuendelea kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwemo Ngorongoro kwakuwa gharama wanazotoza ni ndogo kwao ukilinganisha na wageni toka nje ya nchi hivyo ni fursa nzuri kwao
kuitumia na kuwa mabalozi wa hifadhi kwa wengine.



WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane 


 
Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa
na watanzania.

MTOTO ALIYEUNGUA MIKONO SASA KUREJEA DARASANI


Mtoto aliyeungua na kushindwa kuendelea na masomo mkoani Mtwara ametibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na sasa anaweza kuendelea na masomo pamoja na kufanya shughuli zake za kawaida.

Mtoto huyo aliungua moto baada ya kusukumwa na mwenzake shuleni na hivyo kuungua mikono yote miwili na kusababisha vidole kujikunja na kushikamana.Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari bingwa walifanyia upasuaji na sasa amepona.

Daktari Bingwa wa Upasuaji, Ibrahimu Mkoma amesema mtoto Mwanahidi Hamisi aliungua miaka saba iliyopita na mikono yake kuadhirika na kushindwa kufanya kazi yoyote.

Amesema mwaka 2015 mtoto huyo alifanyiwa upasuaji mkono wake wa kulia katika Hospitali ya CCBRT na kwamba sasa anaendelea vizuri.Dk Mkoma amesema Juni 7, 2017 Muhimbili ilimpokea mtoto huyo na baada ya kufanyia uchunguzi walimfanyia upasuaji mkono wa kushoto na kunyoosha viungo katika vidole vyake ambavyo vilikuwa vimejikunja.

“Baada ya kuungua moto vidole vyake vilishikana na viungo kujikunja, lakini tumefanikiwa kuvinyoosha viungo hivyo na sasa Mwanahidi anaendelea vizuri na matibabu,” amesema Dk Mkoma.Amesema mtoto huyo sasa anaweza kufanya kazi mbalimbali kama kufua na kwamba anaweza kundelea na shule tofauti na awali baada ya kuungua.

Mama wa mtoto huyo, Amina Mohamed Mkadengile ameambiwa kwamba anapaswa kumfanyia mazoezi mtoto wake ili aimarike zaidi.“Daktari amenielekeza jinsi ya kumfanyia mtoto mazoezi, nitakuwa nafanyia mazoezi katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Nawashukuru sana

JAFO AAGIZA MKANDARASI WA MRADI WA MAJI ITISO ASAKWE


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi kumtafuta mkandarasi wa mradi wa maji Itiso ili akamilishe mradi huo haraka kabla ya kuchukuliwa hatua.

Akizungumza leo katika ziara yake ya kukagua mradi huo, Jafo amesema mkandarasi huyo kutoka kampuni ya Audancia anatakiwa kurudi eneo la mradi haraka kukamilisha kama mkataba wake unavyoelekeza.

“Mmtake arudi haraka hapa kwenye eneo la mradi au kama ikishindikana achukuliwe hatua za kisheria kwa kukamatwa na polisi na kupelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kutekeleza mkataba,”amesema Jafo. 

Amesema Mkandarasi huyo ametoweka eneo la mradi huku akiwa amefunga mabomba yenye ubora wa chini kwenye njia kuu (Main line) kinyume cha mkataba.Ameeleza kuwa mkandarasi huyo amelaza mabomba ya Class B(PN 6) badala ya bomba za Class C(PN10) jambo ambalo 

limesababisha mradi huo kushindwa kufanyakazi kwa kuwa mabomba yaliyofungwa yameshindwa kuhimili msukumo wa maji.Kadhalika, Jafo pia ameagiza mkandarasi mshauri wa mradi huo O&A Company LTD kutafutwa kwani ameshindwa kusimamia mradi huo ipasavyo na kuruhusu kazi hiyo ifanyike kinyume cha mkataba na kuruhusu mkandarasi atoke eneo la mradi wakati vituo vinne havitoi maji kati ya vituo kumi vya mradi. 

Hata hivyo Jafo ametoa onyo kwa wakandarasi washauri na wakandarasi wa ujenzi wa maji ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao kwamba hivi sasa kazi zilizo chini ya Ofisi ya Tamisemi watazisikia kwenye bomba.

“Tutakuwa tumebaini makampuni yote yanayofanya kazi kwa ubabaishaji na kutoyapatia kazi tena za usimamizi na ujenzi katika halmashauri zote,”amesema Naibu Waziri Jafo.

Jafo ameagiza kasoro zote za mradi huo zirekebishwe na ifikapo Septemba 15, mwaka huu mradi huo uwe umekamilika.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi nakutoa maelekezo watendaji wa Halmashauri ya Chamwino katika mmoja ya kituo cha kuchotea maji kwenye mradi wa maji Itiso. 
Mbunge wa Chilonwa Joel Mwaka akimkaribisha Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo kuzungumza na wananchi katika mradi wa maji Itiso.

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA CHAZINDUA MTAALA MPYA WA GESI NA MAFUTA


Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo amekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwa uamuzi wake wa kushirikiana na Chuo cha Camosun cha nchini Canada kuandaa mtaala wa ufundi bomba,gesi na mafuta katika ngazi ya Diploma.

Akizindua mtaala huo ambao ni kwanza na aina yake nchini alisema utaisadia serikali kuwapata vijana wengi wenye utaalamu wa sekta ya mafuta na gesi nchini katika ngazi hiyo ambayo imenekana kuna pengo kubwa nchini.

“Mafunzo haya yatasaidia sana kuwapata wataalamu wetu na itaipunguzia serikali mzigo wa kuwaajili wataalamu wa kigeni ambao ulipwa fedha nyingi za kigeni,”alisema

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika amesema baada ya kutambua mahitaji makubwa ya wataalamu wa fani hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita walikua wakiaanda mtaala kwa ushirikiano na Chuo cha Camosun na mafanikio yamepatikana.

Alisema kozi hiyo ni nyumbufu itakayowawezesha wanafunzi kufanya kazi baada ya kumaliza mwaka wa kwanza na baadaye kuendelea na masomo jambo ambalo litakua likiwapa maarifa kwa vitendo zaidi badala ya nadharia pekee.

Mmoja wa wanafunzi wanaosoma kozi hiyo ambayo imegharamiwa na serikali ya Tanzania,Latifa Mkombo amesema wanaishukuru serikali kwa kutoa ufadhili huo na kuahidi kusoma kwa bidii kwaajili kuingia katika ajira za gesi na mafuta.



Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi katika chuo
cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Camosun nchini Canada,Sherri Bell na kulia ni Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika. 



Afisa wa kitengo cha biashara katika ubalozi wa Canada nchini,Anita
Kundy akisoma hotuba yake,kushoto ni Mshauri wa ufundi kutoka nchini Canada,Dk Alan Copeland. 



Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo akionesha nakala ya mtaala mpya wa kozi ya ufundi bomba,mafuta na gesi uliozinduliwa
katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC) 



Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi nchini(TVET)Wizara ya Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Mhandisi Thomas Katebalirwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi huo. 



Baadhi ya wanafunzi wa mwanzo wa kozi ya ufundi bomba na utaalamu wa gesi na mafuta katika Chuo cha ufundi Arusha 




Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Hagnery Chitukulo(wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Chuo cha
Camosun,Victoria nchini Canada na Chuo cha ATC. 

Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani


Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameeleza kuwa ukomo wa kuunganishia umeme wateja walioomba kuunganishiwa huduma hiyo kwa muda mrefu ni Agosti 30, 2017 na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) atakayeshindwa kutimiza agizo hilo atashushwa cheo.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kuzindua mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Mtwara.

"Unakuta kuna wateja wameomba kuunganishiwa umeme miezi kadhaa iliyopita lakini mpaka sasa hawajaunganishwa wakati vifaa vipo, kwa hili lazima tuchukue hatua kwa Meneja kama ni wa wilaya, mkoa, Kanda au Mkurugenzi atayechelewa kuunganishia wateja Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa muda wa kumuunganishia mteja Umeme mara anapolipia huduma hiyo ni Siku Saba na si vinginevyo."Natambua kuna maeneo ambayo TANESCO mnafanya kazi vizuri lakini katika hili tutawajibishana," alisisitiza Dkt. Kalemani.

Wakati huohuo. Dkt. Kalemani aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa watu wote wanaofanya kazi ya kutandaza nyaya za umeme ndani ya nyumba wawe wanatambulika na Shirika hilo ili kuondoa tatizo la vishoka kufanya kazi hiyo pasipo ufanisi na baadaye kuleta madhafa kama ya moto.

Vilevile aliwataka watendaji hao kutokukaa maofisini na badala yake wawafuate wananchi sehemu walipo, suala ambalo litafanya Shirika hilo kuongeza idadi ya wateja na kuwaondolea wananchi kero ya kutembea kwa umbali mrefu kufuata huduma TANESCO.

Kuhusu usimamizi wa mradi wa usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu ambao umeshaanza kutekelezwa nchini, Dkt Kalemani aliwataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa wanawasimamia wakandarasi wanaofanya kazi hiyo usiku na mchana ili mradi ukamilike ndani muda uliopangwa.

Aidha Dkt. Kalemani alitoa maagizo mbalimbali ambayo yanapaswa kutekelezwa na wakandarasi wote waliopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini katika Mradi wa Awamu ya Tatu.

Naibu Waziri aliwaagiza Wakandarasi hao kutoajiri wakandarasi wasaidizi wanaotoka nje ya eneo lao la kazi ili wananchi wanaotoka katika maeneo hayo wapate ajira na kutoa huduma mbalimbali kwa wakandarasi hao na hivyo kujiongezea kipato.

Pia aliwataka wakandarasi hao kutokuruka kijiji, kitongoji, sehemu zinazotoa huduma muhimu kama mitambo ya maji, Shule, vituo vya afya na sehemu za biashara, na nyumba ambazo tayari zimeshafanyiwa malipo ya kuunganishwa na huduma ya umeme.

" nisingependa kusikia Kituo cha Afya, Shule au Mitambo ya Maji imerukwa na haijawekewa Umeme hivyo nichukue nafasi hii kuwashauri watendaji wa Halmashauri nchini kutenga fedha kwenye Bajeti zao kwa ajili ya kutandaza nyaya za Umeme kwenye sehemu hizo ili wakandarasi waweze kuingiza Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Vilevile, Dkt. Kalemani aliwataka wakandarasi hao kutoa malipo kwa wakandarasi wadogo ndani ya wakati ili kuepusha mradi huo kusuasua na kuwacheleweshea huduma wananchi.



Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Ruvuma.