Friday, August 18

Mahakama yaambiwa Manji ni mgonjwa, kesi yaahirishwa hadi Agosti 25



Mfanyabiashara Yussuf Manji 

Mfanyabiashara Yussuf Manji  


Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yussuf Manji (41) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pamoja na wenzake watatu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anaumwa na amepewa mapumziko ya siku mbili.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Agosti 18 na Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa.
Wakili Wilson amedai mahakamani hapo kuwa alipata taarifa hizo za kuwa Manji anaumwa na amepewa mapumziko ya simu mbili toka kwa askari Magereza.
Hata hivyo, amedai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa kutajwa na upelelezi wake hadi sasa bado haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 25, 2017.
Manji na  wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vya kushonea sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni na mihuri.
Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Deogratius Kisinda (28), Abdallah Sangey (46) na Thobias Fwere (43).

No comments:

Post a Comment