Sunday, July 2

RAIS DKT. MAGUFULI AIPONGEZA TTCL, YAIBUKA KIDEDEA SEKTA YA MAWASILIANO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ameipongeza Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kwa juhudi kubwa inazofanya katika kuwapatia Wananchi huduma bora za Mawasiliano. 
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo baada ya kuitembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea. 
Rais Magufuli alitembelea TTCL mara baada ya kufungua rasmi maonesho hayo na kukabidhi zawadi kwa Washindi ambapo TTCL iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Watoa huduma za Mawasiliano na Teknolojia 
Katika Banda la Maonesho la TTCL, Rais Magufuli alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba ambao walimhakikishia Mhe Rais kuwa TTCL inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara yatakayoiwezesha kurejea katika nafasi yake ya kuwa Kinara wa Sekta hiyo nchini. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu TTCL Bw Waziri  Kindamba alisema, anatarajia kuanza kutoa gawio kwa Serikalini mwaka huu na kumuomba  Mhe Rais kuiongezea mtaji Kampuni hiyo ombi ambalo Mhe Rais alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba akipokea Tuzo ya mshindi wa Kwanza katika sekta ya Mawasiliano na Teknolojia kutoka Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa, katika Viwanja vya Sabasaba .
1.      Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikaribishwa na wafanyakazi wa TTCL wakiongozwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba, kwenye banda la TTCL  katika Viwanja vya Sabasaba .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la shirika
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la kampuni

 Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka kwenye banda la TTCL baada ya kutembelea banda hilo, katika Viwanja vya Sabasaba
 Wafanyakazi wa TTCL wakiwa katika picha ya pamoja baada  ya kupata Tuzo ya Ushindi  wa Kwanza kwenye sekta ya Mawasiliano na Teknolojia wa kiongonzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba, katika Viwanja vya Sabasaba .

SHAKA AZINDUA SEMINA ELEKEZI YA UJASILIA MALI KWA VIJANA WA WILAYA YA UBUNGO




Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kuliapamoja na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kinondon ndg:Said Masanga wakionja bidhaa ya dagaa zinazookwa na wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akionyeshwa shati la batiki moja ya bidhaa zinazotengenezwa wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Leah Mbeke akizungumza

Baadhi ya Vijana walioudhuria Mafunzo ya Ujasilia Mali UVCCM Ubungo
yalio fungulia na Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika
Ukumbi wa Texaz Manzese

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza katika Semina ya mafunzo yaUjasilia mali ya Vijana yaliofunguliwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka


Baadhi ya Vijana walioudhuria Mafunzo ya Ujasilia Mali UVCCM Ubungowakishangilia

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa Tatu kulia akicheza Burudani ya Muziki pamoja na Vikundi vya Sanaa Vilivyo tumbuiza.

Kijana akipiga pushap

”Viongozi wa UVCCM Wilaya zote nchini fuatilieni Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020,Hakikisheni asilimia 5 inayotolewa na kila Halmashauri nchini zinawafikia Vijana”Aliyasema Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa Wilaya Ya Ubungo Katika Ukumbu wa Texaz Manzese

MICHUZI TV: KAULI YA RAIS DKT MAGUFULI KWA WANASIASA WASIO WAZALENDO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ameawaonya baadhi ya Wanasiasa kuacha mara moja tabia ya kuwatetea watu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam.
“Kuna mwanasiasa anazungumza kuwa hawa watu wamekaa sana lokapu (mahabusu) waachiwe wakati hawa watu wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi.
“Kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35, maaskari zaidi ya 15 na wanaohusika ni pamoja na hao lakini mtu anatoka anazungumza kwamba wamekaa mno. Unaweza ukaona ‘by implication’ kwamba huyu lazima anahusika kwa njia moja au nyingine”, alionya Rais.
Amewataka wanasiasa wa namna hiyo kujifunza kunyamaza wakati serikali inafanya kazi yake.
Aidha Rais Magufuli alieleza kusikitishwa na mmoja wa wanasiasa ambaye kimsingi hajawahi kusimama hata siku moja kulaani mauaji ya watu wasio na hatia yanayotokea lakini kwa kutaka sifa za kisiasa alisisimama hadharani kutaka wahalifu waachiwe.
Alisema hivi karibuni jeshi la Polisi lilikamata sare 5000 za jeshi na wanaohisiwa kuhusika ni pamoja na ambao tayari wanashikiliwa na vyombo vya dola lakini bado mtu anaingiza siasa kwa kuwatetea wahalifu.
Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini, amelitaka jeshi la Polisi kumhoji kwa kina mwanasiasa yeyote anayetetea wahalifu kwani anaweza kuwa nae anahusika.
“Nataka Polisi mfanye kazi zenu, hawa wanaoropoka waisadie polisi kupeleleza. Msiogope cha sura au mwendo wa mtu awe na mwendo wa spidi au pole pole atayaeleza vizuri atakapo kuwa mle lokapu.
Ameeleza kuwa yeye kama Rais moja ya majukumu yake ni kulinda usalama wa Watanzania na kuusimamia kwa nguvu zote na kwamba maendeleo yaliyopo yanakuja kwa sababu nchi ni slalama.
Amewaomba Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya nchi.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UBORESHAJI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Bandari hiyo.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Baadhi ya mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakifatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird alipokuwa akisoma hotuba yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakati wakitazama kipeperushi ya maelezo ya Mradi wa uboreshaji wa Bandari jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine waliosimama wakati Banana Zorro pamoja na Mrisho Mpoto walipokuwa wakiimbawimbo wa Aamka Tufanye kazi kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

SUMA JKT WANYAKUA TUZO YA KILIMO NA UFUGAJI BORA WA MWAKA 2017


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri amesema kuwa jitihada na juhudi zinazofanywa na vijana wake ndicho kitu kikubwa kilichopelekea kupata tuzo ya  masuala ya Kilimo na ufugaji.

Tuzo hiyo walikabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Brigedia Jenerali Yateri alisema kuwa, mbali na kujihusisha na masuala ya ufugaji na kilimo amvapo wana dhana mbalimbali wanazozitumia ikiwemo Kilimo cha umwagiliaji pia wanajihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ya kuwaweka.

Pmaoja na hilo,  SUMA JKT wamejikita zaidi katika utengenezaji wa samani za ndani kama makabati, vitanda, samani za maofisini na vitu mbalimbali pia wanatengeneza nguo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri akizungumza na Globu ya Jamii mara baada ya kupata tuzo katika masuala ya Kilimo na ufugaji waliyokabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzin wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Dhana mbalimbali za Kilimo zinazotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji vinavyotumika na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), dhana hizo ziliweza kuwekwa wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.


 Baadhi ya wananchi wakiangalia Mabwawa ya Samaki yanayotumiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa ajili ya ufugaji ambapo kila tenki moja linachukua samaki 100 wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.


Wananchi wakiangalia mabanda ya kuku wanaofugwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Samani zinazotengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) zikiwa katika banda lao wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere

Manchester United yamkera Jose Mourinho

Hadi sasa ni mchezaji mmoja tu, Victor Lindelof aliyesajiliwa kati ya wanne ambao Jose Mourinho alikuwa akiwataka Old Trafford
Imeripotiwa kuwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho amekerwa na uzito wa klabu hiyo kuingia kwenye soko la usajili majira ya joto.
Mchezaji mmoja tu hadi sasa amewasili Old Trafford usajili wa majira ya joto, Mswidi Victor Lindelof ambaye ni beki wa kati kutoka Benfica.
Inafahamika kuwa Mourinho pia anamtaka Alvaro Morata wa Real madrid, Ivan Perisic wa Inter Milan na Nemanja Matic wa Chelsea, lakini hakuna hata mmoja aliyetolewa ofa kati ya wachezaji hao watatu.
Kwa mujibu wa The Sun, Mourinho alitaka wachezaji wapya wanne wasafiri na kikosi chake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya Marekani wiki ijayo, na kocha huyo amevunjika moyo kutokana na makamu mwenyekiti kukosa uharaka wa kusajili.
Imedai kuwa Manchester United wanakaribia kumsajili Matic, lakini kuhusu uhamisho wa Morata na Perisic bado hakijaeleweka kwani Real Madrid na Inter Milan zinapambana kuwashawishi wachezaji hao kubaki.
Man United wataikabili LA Galaxy, Real Salt Lake, Manchester City, Real Madrid na Barcelona katika kipindi cha maandalizi ya msimu mpya ziarani Marekani.

Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini wazinduliwa


Changamoto ya usafiri nchini, hususan maeneo ya vijijini itakuwa historia baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzindua Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).
Amesema wakala huo utasaidia kuimarisha mtandao wa barabara za vijijini na kuwawezesha wananchi wengi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo kukuza uchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumapili  wakati akizindua wakala huo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma.
"Wakala huu tunaouzindua leo utakuwa na manufaa makubwa kwa ustawi wa nchi yetu kwa kuongeza chachu ya uzalishaji mali mashambani kutokana na urahisi wa kufika sokoni,"
"Utashusha bei ya vyakula mijini na bidhaa za viwandani vijijini kutokana na gharama za usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na bidhaa za viwandani kutoka mijini kupungua."
Waziri mkuu amesema manufaa mengine ya wakala huo ni kuboresha na kubadili hali za kimaisha na kiuchumi kwa wananchi kwani watakuwa wanasafiri kwa muda mfupi.
Pia utawezesha maeneo mengi ya nchi kufikika kwa urahisi, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wakati.
Katika hatua nyingine, waziri mkuu amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika ujenzi, ukarabati na utengenezaji wa miundombinu ya barabara ikiwemo ya rushwa katika utoaji wa zabuni.
Amesema jambo hilo halikubaliki hivyo, amewataka watendaji wa TARURA wahakikishe wanatokomeza vitendo vya rushwa vilivyokithiri kwenye utoaji wa zabuni, zitolewe kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.
Waziri mkuu amesema changamoto nyingine ni usimamizi hafifu wa mikataba ya ujenzi, ambapo ameelekeza isimamiwe vizuri na iwe ya wazi na yenye kutekelezeka.
Akizungumzia vitendo vya baadhi ya viongozi wa halmashauri kubadilisha matumizi fedha za barabara, ameagiza fedha zote zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya barabara zitumike kama ilivyopangwa.
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, George Simbachawene alisema TARURA ni muhimu kwa kuwa zinagusa wananchi moja kwa moja na ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa wananchi, hivyo kuinua uchumi wa  Taifa wenye msingi imara.
"Barabara hizi zinachochea kilimo katika ngazi ya jamii, zinaboresha ufikaji kwenye huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na masoko, hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na jamii imara kiafya, kiakili na kiuchumi."

Foleni za ulipaji kodi ya majengo TRA zayeyuka Dar

Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilizopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam zikiwa zimefungwa jana. Juzi ofisi hizo zilikuwa na foleni kubwa ya wananchi waliokuwa wakihakiki taarifa za kodi ya majengo. Picha na Said Khamis 
Siku moja baada ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuongeza muda wa ulipaji kodi ya majengo, idadi ya watu wanaokwenda kuhakiki taarifa zao za kodi katika ofisi hizo imepungua.
TRA imeongeza muda wa ulipaji kodi juzi hadi Julai 15 badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa awali.
Kupungua kwa watu katika ofisi hizo ni tofauti na juzi iliyokuwa siku ya mwisho, ambapo msongamano ulionekana katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali ilivyokuwa katika ofisi mbalimbali jijini hapa kwa siku ya juzi, gazeti hili lilitembelea Temeke, Ilala na Kinondoni jana kuangali kama kungekuwa na msongamano au la. Hata hivyo, Mwananchi ilikuta ofisi hizo hazina idadi kubwa ya watu kama ilivyotegemewa licha ya TRA kufanya kazi hadi saa kumi jioni.
Mfanyakazi wa mamlaka hiyo eneo la Mbagala ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji alisema wanafanya kazi mpaka saa kumi jioni. “Hapa sisi tunatoa huduma mpaka jioni, Juni 29 na 30 tulikusanya fomu za watu 1,222 ambazo tunazifanyia kazi kwa leo kama hivi ulivyokuta,” alisema huku akionyesha boksi lililojaa fomu hizo.
Alisema kwa kuwa muda umeongezwa wanajitahidi kufanya kazi kwa kasi zaidi ingawa juzi mtandao ulikuwa chini.
Mkazi wa Mbagala aliyekuwa akisubiri kuingia katika ofisi hizo, Ally Mbwela alisema hakuwahi kulipa kodi hadi tarehe ya mwisho ilipotangazwa kuwa ni Juni 30 na baada ya kusikia muda umeongezwa amepata fursa ya kwenda kufanyiwa uhakiki.
Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke, Gemalieli Mafie alisema wameongeza kituo eneo la Sabasaba ambapo wananchi wanaweza kufika kuhakiki taarifa zao na kupata fomu za malipo.
Pia, Mafie alisema wananchi wanaweza kupata taarifa za madai yao katika kituo hicho bila kujali walikojengea nyumba zao nchini.