Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Brigedia Jenerali Charo Yateri amesema kuwa jitihada na juhudi zinazofanywa na vijana wake ndicho kitu kikubwa kilichopelekea kupata tuzo ya masuala ya Kilimo na ufugaji.
Tuzo hiyo walikabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Brigedia Jenerali Yateri alisema kuwa, mbali na kujihusisha na masuala ya ufugaji na kilimo amvapo wana dhana mbalimbali wanazozitumia ikiwemo Kilimo cha umwagiliaji pia wanajihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ya kuwaweka.
Pmaoja na hilo, SUMA JKT wamejikita zaidi katika utengenezaji wa samani za ndani kama makabati, vitanda, samani za maofisini na vitu mbalimbali pia wanatengeneza nguo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Brigedia Jenerali Charo Yateri akizungumza na Globu ya Jamii mara baada ya kupata tuzo katika masuala ya Kilimo na ufugaji waliyokabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzin wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Dhana mbalimbali za Kilimo zinazotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji vinavyotumika na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), dhana hizo ziliweza kuwekwa wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Baadhi ya wananchi wakiangalia Mabwawa ya Samaki yanayotumiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa ajili ya ufugaji ambapo kila tenki moja linachukua samaki 100 wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Wananchi wakiangalia mabanda ya kuku wanaofugwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Samani zinazotengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) zikiwa katika banda lao wakati wa ufunguzi maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
No comments:
Post a Comment