Hadi sasa ni mchezaji mmoja tu, Victor Lindelof aliyesajiliwa kati ya wanne ambao Jose Mourinho alikuwa akiwataka Old Trafford
Imeripotiwa kuwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho amekerwa na uzito wa klabu hiyo kuingia kwenye soko la usajili majira ya joto.
Mchezaji mmoja tu hadi sasa amewasili Old Trafford usajili wa majira ya joto, Mswidi Victor Lindelof ambaye ni beki wa kati kutoka Benfica.
Inafahamika kuwa Mourinho pia anamtaka Alvaro Morata wa Real madrid, Ivan Perisic wa Inter Milan na Nemanja Matic wa Chelsea, lakini hakuna hata mmoja aliyetolewa ofa kati ya wachezaji hao watatu.
Kwa mujibu wa The Sun, Mourinho alitaka wachezaji wapya wanne wasafiri na kikosi chake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya Marekani wiki ijayo, na kocha huyo amevunjika moyo kutokana na makamu mwenyekiti kukosa uharaka wa kusajili.
Imedai kuwa Manchester United wanakaribia kumsajili Matic, lakini kuhusu uhamisho wa Morata na Perisic bado hakijaeleweka kwani Real Madrid na Inter Milan zinapambana kuwashawishi wachezaji hao kubaki.
Man United wataikabili LA Galaxy, Real Salt Lake, Manchester City, Real Madrid na Barcelona katika kipindi cha maandalizi ya msimu mpya ziarani Marekani.
No comments:
Post a Comment