Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ameipongeza Kampuni ya Simu Tanzania TTCL kwa juhudi kubwa inazofanya katika kuwapatia Wananchi huduma bora za Mawasiliano.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo baada ya kuitembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea.
Rais Magufuli alitembelea TTCL mara baada ya kufungua rasmi maonesho hayo na kukabidhi zawadi kwa Washindi ambapo TTCL iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Watoa huduma za Mawasiliano na Teknolojia
Katika Banda la Maonesho la TTCL, Rais Magufuli alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba ambao walimhakikishia Mhe Rais kuwa TTCL inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara yatakayoiwezesha kurejea katika nafasi yake ya kuwa Kinara wa Sekta hiyo nchini.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu TTCL Bw Waziri Kindamba alisema, anatarajia kuanza kutoa gawio kwa Serikalini mwaka huu na kumuomba Mhe Rais kuiongezea mtaji Kampuni hiyo ombi ambalo Mhe Rais alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi.
|
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba akipokea Tuzo ya mshindi wa Kwanza katika sekta ya Mawasiliano na Teknolojia kutoka Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa, katika Viwanja vya Sabasaba .
|
|
1. Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikaribishwa na wafanyakazi wa TTCL wakiongozwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba, kwenye banda la TTCL katika Viwanja vya Sabasaba . |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la shirika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipotembelea banda la kampuni
Mhe Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka kwenye banda la TTCL baada ya kutembelea banda hilo, katika Viwanja vya Sabasaba
Wafanyakazi wa TTCL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupata Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwenye sekta ya Mawasiliano na Teknolojia wa kiongonzwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mhe Omari Nundu na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba, katika Viwanja vya Sabasaba .
No comments:
Post a Comment