Monday, July 3

NHIF yaibuka na ushindi Maonesho ya Sabasaba

Watoto wakifurahi baada ya wazazi wao kuwasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekuwa mshindi wa tatu kupitia kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ushindi uliotangazwa mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 41 ya Sabasaba.

NHIF inayoendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya umri wa miaka 18 kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwa ajili ya kuwahakikishia watoto hao upatikanaji wa huduma za matibabu wakati wote.

Hata hivyo mpango wa Toto Afya Kadi umekuwa kivutio kikubwa katika Maonesho hayo ambapo wananchi wengi wanamiminika bandani hapo kwa lengo la kupata huduma kwa ajili ya watoto wao.

Wakizungumza bandani hapo wananchi, wamesema kampeni hii ni mkombozi mkubwa kwa familia ambazo zina watoto na hazikuwa na fursa ya kujiunga na huduma za NHIF hapo awali.

Wamesema utaratibu huu uendelee katika maeneo mengi zaidi ili watoto wote wa Tanzania wawe ndani ya Mfumo wa kupata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya.

Akizungumzia hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Anjela Mziray, amesema kuwa NHIF imejipanga kuhakikisha inafika kila mahali kwa lengo la kuwahudumia Watanzania wote.

“NHIF tumejipanga na tunakwenda sambasamba na kasi ambayo Mkuu wetu wan chi Rais Dk. John Pombe Magufuli anaitaka hususan katika kuwahakikishia wananchi huduma za matibabu hivyo Watanzania wote tutawafikia katika maeneo yao,” alisema.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya una mtandao mpana wa vituo vya kutoa matibabu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wanachama wake.
Watoto wakifurahi baada ya wazazi wao kuwasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mmoja wa Wazazi akiwa na watoto wake ambao amewasajili katika mpango wa Toto Afya Kadi.
Dk. Edwin Mwangajilo akiwa na watoto ambao wamejiunga na huduma za NHIF.
Wazazi mbalimbali wakiendelea kufanya malipo kwa ajili ya kuwasajili watoto wao.
Huduma ya ujazaji fomu ikiendelea.
Ofisa Uanachama Mwandamizi wa NHIF, Kuhunga Msambichaka akiendelea kuhudumia wanachama katika upande wa kutoa vitambulisho.

No comments:

Post a Comment